Rais Dk. Samia afungua
fursa kwa vijana EACOP
Na Mwandishi Wetu, Geita
Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imezidi kuwajali vijana, baada ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko kuzindua Mpango wa Uwezeshaji wa Kiuchumi kwa Vijana (YEE), ambao unagusa maeneo yanayopitiwa na mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).
Uzinduzi huo ni jitihada zinazoendelea kufanywa na Serikali katika kuhakikisha kuwa jamii zilizo karibu na miradi zinanufaika na miradi hiyo.
Akizindua mradi huo katika Kijiji cha Bukombe, wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita leo, Dk. Biteko alisema mradi huo wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi ni moja ya miradi iliyopangwa kuwezeshwa na Kampuni ya EACOP, kwa kipindi cha ujenzi na baada ya ujenzi ikiwa ni sehemu ya Uwajibikaji wa Kampuni hiyo kwa jamii.
Alisema mradi huo umepangwa kuwafikia zaidi ya vijana 12,261 ambao miongoni mwao wanawake ni 6,130; wanaume 4,905 na makundi maalumu 1,226, katika awamu ya kwanza inayohusisha Mikoa ya Geita, Kagera, Tabora na Tanga.
"Tunapozindua mradi huu hatuna budi kuwashukuru Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda.
Viongozi wetu hawa kwa nia yao ya dhati na moyo wa uzalendo wameuendeleza na kuusimamia kikamilifu mradi huu wa EACOP ambao umefikia asilimia 65, tumefikia hapa sababu ya msukumo wao wa kutekeleza mradi huu, "alisema Dk. Biteko.
WATANZANIA
WALIO NUFAIKA
Alifafanua, kuwa tangu kuanza kwa mradi wa EACOP mwaka 2022 hadi hivi sasa, jumla ya Watanzania 9,194 wamepata nafasi za kufanya kazi ndani ya mradi na hivyo kuwa fursa kwao ya kujipatia kipato, mwaka 2024 kampuni ilitoa mafunzo maalumu kwa vijana 170 na kuwapatia kazi kwenye mradi, vijana wengine 110 wapo katika masomo na wanatarajiwa kujumlishwa pia katika mradi huo.
-Ends