🔥FURSA INAUZWA; Kiwanja Cha Mita za mraba 2,400 kinauzwa milioni tatu (3), Mazungumzo yapo

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Habari,

Kwa majina ninaitwa Aliko Musa. Mimi ni mwandishi wa makala na vitabu vya uwekezaji kwenye ardhi na majengo. Ninawafikia watu kupitia mitandao yangu iitwayo UWEKEZAJI MAJENGO.

Leo ninaitambulisha huduma mpya iitwayo FURSA INAUZWA. FURSA INAUZWA ni huduma ambayo huwa ninaitoa mimi mwenyewe kupitia njia mbalimbali za matangazo.

Hali Ya Muuzaji Wa Kiwanja.

Muuzaji wa kiwanja anaishi mkoa tofauti na kiwanja kilipo. Hivyo ameona ni vyema kutumia mitandao yangu ya kuwafikia watu. Kwa sababu tayari nina programu iitwayo FURSA INAUZWA, nikamtumia fomu maalumu ya ukaguzi wa kiwanja.

Na baadaye nikaongea naye kwa njia ya simu na mambo mengine. Hivyo, ninapenda kukujulisha kuwa hii fursa sio ya kukosa kama kweli una mpango wa kumiliki kiwanja kizuri cha aina hii nipigie simu mimi Aliko Musa tuyajenge.

Kama hauna cash nipigie simu, nimekuambia ni fursa. Wapo wengi wanaomba kuwatangazia viwanja vyao ila vinakuwa havina sifa za kiuwekezaji. Kwa kiwanja kilivyo unaweza kuanza uwekezaji kwa mafanikio makubwa endapo utatumia mbinu zifuatazo;-

✓ Nyumba ya matumizi mseto (house hacking strategy).

✓ Mbinu ya kumiliki mpaka kuombea mkopo (B-R-R-R-R ya nyumba za kupangisha).

Huduma ya FURSA INAUZWA inahusisha kutangaza nyumba zinazolipa sana. Nyumba zinazozitangaza kwa njia hii hufaa sana kwa malengo haya;-

✓ Kujenga utajiri kupitia ardhi na majengo.

✓ Kutunza utajiri kupitia ardhi na majengo.

✓ Kustaafu na kipato kikubwa na endelevu kwa kila mwezi.

✓ Kujenga nyumba nzuri ya kuishi na nafasi inabaki kubwa kwa ajili ya shughuli zingine ikiwemo ufugaji na kilimo kisasa cha bustani.

Ni nadra sana kukutana na fursa hii kwenye uwekezaji wa viwanja. Kiwanja kinafaa sana kwa ajili ya nyumba za kupangisha au nyumba ya kuishi wewe na familia yako.

Kiwanja kina sifa zifuatazo;-

✓ Hati ya hakimiliki ya ardhi.

✓ Kina nyaraka zote muhimu zilizotumika kuombea hati.

✓ Kiwanja hakina historia ya mgogoro wa umiliki wa ardhi.

✓ Kipo karibu kabisa na hospitali teule ya wilaya.

✓ Kipo kwenye hali ya tambarare.

✓ Kiwanja ni kikubwa sana, unaweza kukigawa na kujenga nyumba 3 au 2 za kupangisha.

Sifa Zinginezo za Kiwanja Hicho;-

✓ Kiwanja kipo karibu na ofisi za halmshauri.

✓ Kiwanja kipo karibu na kituo cha afya cha kata husika.

✓ Kiwanja kipo karibu sana na laini ya umeme wa TANESCO.

✓ Hakuna historia ya changamoto ya maji kwenye mtaa ambapo kiwanja kinachouzwa kipo.

✓ Muuzaji amehamasika sana kuuza kiwanja hicho.

✓ Kiwanja kipo mkoani Rukwa.

Muhimu; jiunge na kundi la REAL ESTATE BEGINNERS ili upate kujifunza mbinu bora za kuwekeza kwenye ardhi na majengo ambazo zifundishi popote. Utapata ushauri na usimamizi kutoka kwangu kuhusu mambo ya ardhi na majengo.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi majengo.

Whatsapp; +255 752 413 711
 
Unajiita mbobezi halafu hata sifa kubwa ya kiwanja kama mkoa au wilaya kilipo unaficha. Kwanini tusikuhisi ni tapeli
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom