FURSA: Huduma za Urembo, Kinyozi na Usafi nyumbani kwako

FURSA: Huduma za Urembo, Kinyozi na Usafi nyumbani kwako

FAJES

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2017
Posts
723
Reaction score
658
Mimi na kijana mwenzangu tumeamua kubuni biashara kwa mfumo wa kidijitali kuendana na kasi ya Dunia.

Mfumo wa Huduma upo hivi.

Kwanza, mpaka sasa tumekamilisha kusajili kampuni BRELA inayojihusisha na huduma tajwa hapo juu. Kuanzia wiki ijayo tunashughulikia kupata TIN na Leseni ya biashara. Baada ya hapo tutaanza kazi mara moja, Ofisi pia tumeshakamilisha na kilichobaki ni kulipia tu.

Tumetengeneza Website na Application ambazo zitatumika kwa Wateja wetu kujisajili na kuomba huduma. Huduma zetu tunamfuata mteja nyumbani kwake. Huu ndio utofauti wetu na watoa huduma wengine.

Hiyo application kufikia wiki ijayo itakuwa approved kwenye play store na watuamiaji wa Android wataweza kuipata bila shida kabisa. Baadae tunampango wa kuiingiza pia ili watumiaji wa iPhone nao waweze kuipata.

Hapo nyumbani ulipo uta-request huduma iwe huduma ya kunyolewa, usafi wa nyumbani kwako, ususi kwa akina mama, kutengeneza kucha na madikodiko mengine yote ya Urembo. Kisha vijana wetu wataalamu wa kutoa huduma wataipata request yako na kukufuata nyumbani ulipo.

Tutaanzia Dar es Salaam ila lengo ni kufikia nchi nzima na nje ya mipaka ya nchi yetu.

Watoa huduma wetu hatutawaajiri, isipokuwa wanajiajiri wenyewe kwa kujisajili kwenye platforms zetu na wao watalipia kidogo commission kwa kutumia application yetu. Sisi tutahusika zaidi kwenye matangazo kuwatafuta wateja na ubora wa huduma yenyewe.

Naombeni maoni na ushauri juu ya huduma hii.
 
Inaonesha ni wazo zuri. Muhimu hapo ni utekelezaji wake tu. Kingine ni kuwa na watoa huduma wa uhakika na wanaoendana na ubora mnaotaka nyinyi.
 
Muweke na kipengele cha scrub mnatuma mdada mkalii anifanyie usafii wa kichwa na uso, itapendeza sana
Ilikuwa tuweke na huduma ya massage. Ila kutokana na kiwango cha ustaarabu wetu hapa Bongo na ukata wa maisha, tukaona tutawaingiza dada zetu kwenye tusichokitarajia na kuharibu brand ya kampuni.

Hizo huduma bado tunazitafakari kwa kina namna tunavyoweza kuzitoa kwa mazingira ya nyumbani kwa mtu. Kwakweli tunaiona changamoto mbeleni licha ya ukweli kuwa ni huduma zinazoweza kuingiza pesa nzuri.
 
Kitu ni nzuri msisahau kujimarket vizuri..afu muweke wadada wazuri kwa ajili kuja kuosha vyombo.

All the best
 
Mtuletee majambazi yaje yatukabe majumbani. Hao vijana unajuaje kuwa sio majambazi kwa mgongo wa nyuma?
Suala la ulinzi wa watu na Mali zao ni jukumu la Jeshi la Polisi. Kama jamii yetu imetawaliwa na vibaka na majambazi kama unavyosema basi hatuko salama wote bila hata ya huduma hii.
 
Mtuletee majambazi yaje yatukabe majumbani. Hao vijana unajuaje kuwa sio majambazi kwa mgongo wa nyuma?
Watoa huduma wetu watakuwa na mikataba ya kushirikiana kazi na sisi. Tutawafanyia recruitment na training. Kisha tunawapa terms and conditions. Mojawapo ya policy katika kazi zetu ni uaminifu na shughuli zote zifanyike ktk mazingira ambayo si hatarishi kwa mtoa huduma na mteja wetu. Watakuja na barua za utambulisho kutoka mtaani kwao na watafanya kazi mtaani kwao hukohuko wanakojulikana.
 
Back
Top Bottom