Fursa hazidumu; Wewe ni Asset! Jitumie!

Fursa hazidumu; Wewe ni Asset! Jitumie!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,059
Reaction score
79,413
FURSA HAZIDUMU; WEWE NI ASSET. JITUMIE!

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Wahenga walisema, liwezekanalo Leo lisingoje Kesho. Wahenga hao! Wakaendelea kusema bahati haiji mara mbili! Unaona mambo hayo!
Neno bahati huweza kutafsiriwa kama nafasi au fursa ya kipekee.

Katika mapigano yoyote lazima uelewe kanuni hiyo kuwa Fursa na nafasi zinakawada ya kutokudumu.

Fikiria upo ulingoni, unapigana na jinamizi, jitu mwitu msitu. Katika panga pangua, rusha ngumi kwepa, mara paap! Kama utani adui anakuachia nafasi nyeti ambayo inakuhitaji wewe kupiga, labda kakuachia Kidevu, macho, pua, au kakuachia Kende. Hapo hutakiwi kuzubaa au kujichelewesha, Piga acha uboya wewe. Usije ukafikiri adui atabaki kwenye position ileile akikusubiri wewe na ujinga wako ili umbutue.

Fursa hazidumu!

Wakati unacheza Mchezo wa Draft, kuna muda mpinzani wako anaweza akajisahau na kuelekea Kibla. Kikanuni, drafti linahitaji nafasi ili ufunge. Na mpinzani akiachia nafasi unatakiwa kubutua. Elewa mara nyingi kwenye maisha kanuni inayoweza kutumika ni One touch! Hii inamaanisha mchezaji lazima uwe Makini, kwani kila kete utakayosogeza inaweza kuwa fursa kwa mpinzani wako. One mistake a hundred goals.

Fursa hazidumu!

Umri ulionao sasa haurudi nyuma. Nguvu, akili, mwonekano,wakati hautabaki siku zote upande wako.
Kila nafasi kwako ihesabu ya thamani na Ione kama haitajirudia. Itumie kwa bidii na akiii ikuweke katika nafasi nzuri.

Elewa Fursa Moja hutengeneza fursa nyingine. Fursa huzaa fursa. Kutumia fursa zinazokujia katika njia ya maisha yako ni kutengeneza fursa zaidi. Kutotumia Fursa ulizonazo ni kuua, kuziondoa fursa zingine ambazo zingetakiwa uzipate.

Matumizi ya fursa hutokana na kutambua kuwa wewe ni Assets. Wewe unatija, wewe unavitu nyeti vyenye thamani.

Akili yako
Kipaji na karama zako.
Ujuzi na elimu yako.
Mwonekano walk
Yote hayo ni assets unazoweza kuzitumia kutengeneza fursa za kukusaidia maishani.

Elewa hatua moja huzaa hatua bilioni Moja. Hiyo tunaita uzoefu.
Hatua Moja na kuthubutu, katika kuthubutu kuna kujifunza, na kufanya. Katika kujifunza na kufanya unakuwa mzoefu na mahiri.
Katika Umahiri na uzoefu kuna Kujiamini.
Katika Kujiamini kuna Ubora, weledi na Ubunifu.

Huhitaji kuwa Taikon Master, huhitaji kuwa yeyote. Unahitaji kuwa wewe Mwenyewe.

Kwenye maisha yako, kamwe usiogope kujaribu na kufanya. Katika kujaribu na kufanya usiogope kuanguka. Katika kuanguka kamwe usiache kusimama ukiwa umejifunza.

Wengine watashindwa au walishindwa na wameshindwa Lakini sio wewe.
Kushindwa kwa wengine sio kushindwa kwako. Unapoanguka tumia kuanguka kwako kama fursa ya kujifunza ili uinuke.

Onyesha kile ambacho unacho kilichobora zaidi.

Wanaokuambia huwezi, ni mashabiki zako. Wao wala sio wachezaji. Usiache kucheza mchezo kwa kusikiliza sauti za mashabiki nje ya uwanja
Watumie wanaokubeza kama Kichocheo cha wewe kukazana zaidi.

Sisi watibeli tuna kanuni na falsafa zetu zinazotuongoza.
Kwanza, vitu vyote vizuri ni halali yetu.
Tunapenda vitu na Mambo mazuri ambayo watu waoga huviogopa.
Tunatumia Woga WA wengine kupata vitu na mambo mazuri. Woga wa wengine kwetu ni fursa ingawaje tunajua fursa hiyo haitadumu daima.

Watu wanaogopa Competition sisi tunapenda Competition.
Watu wanaogopa Wanawake wazuri sisi ndio tunaowapenda na lazima kuoa au kuzaa na mwanamke mzuri. Hiyo ni lazima.
Watu wanaogopa kuwa na wanawake wenye vipato na mamlaka. Sisi ndio tunao hao na tunawatumia kwa mambo mengine.
Vile watu wanavyoviogopa ni fursa Kwako.
Watu wanaogopa siasa sijui vyeo, Sisi ndio tunaenda hukohuko.

Hupaswi kuwa Mwoga. Wewe ni mwanaume. Haipendezi kwa Mwanaume kuwa mwoga.
Sehemu wanazoogopa wengine kwako ni fursa. Sehemu zilizojificha ndizo unatakiwa kupiga. Wanasema kupiga kwenye mshono.
Nazungumzia aina ya fursa.
Kuna Fursa kubwa(nyeti) na Fursa ndogondogo(za wazi)

Tatizo la fursa za wazi utatumia muda mrefu kujijenga. Fikiria kwenye kupigana umpige mtu ngumi ya mgongo, teke la paja, ngumi ya Bega. Unafikiri itakuchukua muda gani kumdondosha adui.

Tofauti na Fursa Nyeti. Unapiga mara moja mzigo unaitika. Na hauhitaji kupiga kwa nguvu ila itahitaji akili mingi na timing.
Fikiria kwenye ngumi umpige mtu kwenye makende, koo, macho, mwamba wa Pua, mbavu change, kwenye kiungio cha mfuniko fuvu na taya. Hapo ndio unasikia knockout, yaani pigo Moja Mtu chali.

Haya! Usijesema Taikon unamaneno Mengi.

Acha nikapate Breakfast hapa. Chapati mbili, na supu ya Kuku. Nyumbani!

Zamu yenu!

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom