Fursa bila mtaji bado ni tatizo

Fursa bila mtaji bado ni tatizo

Pate_15

Senior Member
Joined
Oct 26, 2013
Posts
156
Reaction score
48
Ndugu wana jf,
Kwanza napenda niwashukuru wale wote ambao wanajitolea kutangaza fursa mbali mbali za ajira na kujiajiri "Ahsanteni" Ila katika uzi huu nawaomba pia muangalie jinsi gani mta tukomboa sisi ambao tukomakini katika kutafuta njia ya kujikwamua katika umaskini..
Fursa zipo nyingi sana kitaa ila mitaji ndo tatizo kubwa sana.
Kwamfano, siku chache zilizopita nilishiriki presentation flani hapa dar,nimependa mada zao na nimevutiwa sana kufanya nao kazi/biashara ila ugumu pale kwenye mtaji wa kuanza hiyo biashara.
Inatakiwa laki moja kama mtaji wako ili kuanza nao biashara nawe huna hata shilingi elfu moja ya kula au elfu kumi ya akiba,nini kitafata kama sio mawazo mengi ya kuumiza kichwa kwa sababu njia umeiona ila unashindwa kupita kwa kikwazo cha pesa.
Tusaidieni hata njia za kupata mikopo rahisi yenye masharti mepesi hapitakua mmemaliza tatizo.
Natanguliza shukwani kwenu mtakao guswa na mungu awape wepesi wa kutusaidia zaidi,Ahsanteni.
 
Ardhi ni sehemu nzuri ya kupatia mtaji mkuu. Funga mkanda miezi kadhaa tumia jembe la mkono utapata tu mtaji si unajuwa tena mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe?
 
Ni jambo zuri na ninapenda sana kulima na nimewahi kufanya hivo na matokeo yakawa mabaya kwa miaka miwili mfululizo.
 
hao clouds hawana lolote hv unamshauri mtu ajiajiri wakati hawana kitu.wale ni wazushi hawana lolote hata fursa ziwe mia moja bila mtaji ni kumuumiza mtu kichwa.
 
Ulikuwa umelima zao gani? nini kilipelekea matokeo mabaya?

Mwaka wa kwanza nililima mpunga sikufanimiwa kwasababu hapakuwapo na mvua ya kutosha..
Mwaka ulofuata niliamua nilime mahindi, yakaliwa na wadudu 'viwavi' bado ikawa tatizo.
 
Ulichaguwa mazao mabaya sana kwa maana ya gharama na hata uangalizi wake na hata faida yake ni ndogo. Safari hii kalime kati ya matikiti maji, alizeti, vitunguu saumu, vitunguu maji au tangawizi. Lima ekari moja tu. Usisubiri mvua, tafuta sehemu uwe unamwagilia kwa ndoo.
 
Maeneo ambayo niliyatumia ni milki ya wazazi wangu hivyo sikutozwa ila nikitaka kilimo hicho inabidi niangalie maeneo yalio na mto au bwawa kwa urahisi wa kumwagilia hivyo bado tatizo lita kuwa ni lile lile la mtaji kwa sababu mwenye ardhi atahitaji chochote kitu ndipo akuruhusu utumie chake....bado shida mkuu
 
Fanya kazi ya udalali au affiliate marketing kwa muda kisha ukipata mtaji utaenda kulima.
 
Uzoefu wa hiyo kitu nao ni shida, nko dar lakin najaribu kufanya mipango ili nipate inshu ambayo itanipatia kipato hivyo hata kama ww anachochote cha kunishirikisha ntakushukuru.
 
Mwaka wa kwanza nililima mpunga sikufanimiwa kwasababu hapakuwapo na mvua ya kutosha..
Mwaka ulofuata niliamua nilime mahindi, yakaliwa na wadudu 'viwavi' bado ikawa tatizo.
Hauko makini, unatakiwa ufate utaratibu wa kilimo bora na kabla ya kulima unatakiwa uwe na basic needs kama mbegu bora, madawa ya kuulia wadudu, na hakikisha upatikanaji wa maji kwa ajili ya kumwagilia( nafahamu labour na land kwa TZ sio tatizo sana), sio unakurupuka tu na pia ningekushauri mjiunge kwenye vikundi ndo kwa pamoja mnaweza mkapata mkopo sio wewe kama wewe....anza na hilo kwanza
 
Nimependa....ila kwa sasa niko dar es salaam kunamambo nafuatilia na ntafanya hivyo pindi nikirudi mkoa..sijui nitakua sijachelewa.
 
Back
Top Bottom