Furnitures, Nitazipata wapi Dar?

BelindaJacob

Platinum Member
Joined
Nov 24, 2008
Posts
6,494
Reaction score
4,076
Wasalaam wanaJF,

Natafuta duka au kampuni inayouza furniture (yaani viti, meza ya chakula/kahawa, makabati ya nguo ya vyumbani) jijini Dar-es-salaam.

Nitashukuru mkinitajia kampuni zanye sifa na bidhaa nzuri il niweze kuona na hatimaye kununua bidhaa zao. Ikiwezekana wawe wanatengenezea makabati nyumbani kwa mteja.

Asanteni,
Belinda!!
 
Muone dada mmoja anaitwa sachegues yupo istagram anafanya furniture nzuri sana au furnituresolution ukiingia IG utawa wengi
 
Mkuu Keko ndio kila kitu kuhusu mambo ya fenicha kuanzia keko magurumbasi hadi keko bora,ila jaribu kwenda na mtu anayejua mbao vizuri usije ukauziwa kitanda cha muembe 4 kwa 6 baada ya mwezi kitanda kinatanuka na kuwa 6/6
 
Kuna aina tatu za furniture za kichina,ready made keko ambazo hazidumu maana hutumia hata mti wa muembe na za kutoa order kwa fundi ambazo huwa zina dumu sana na ni design yako
 
Kuna aina tatu za furniture za kichina,ready made keko ambazo hazidumu maana hutumia hata mti wa muembe na za kutoa order kwa fundi ambazo huwa zina dumu sana na ni design yako

Hapo kwenye kutoa order kuna mawili!
1:Unaweza kupata fenicha unayotaka kwa wakati pia nje ya wakati unaotaka
2:Unaweza ukadhulumiwa kabisaa maana mafundi kwa story hawawezekani hata kidogo,ingekuwa mafundi wote wanafungwa kwa ajili ya udanganyifu basi usingeona mafundi mtaani
 
Asanteni wapendwa kwa kujibu hapo juu.

Yaani wasiwasi wangu mkubwa ni kufanyiwa kazi mbovu ilhali umegharamia na kuaminishwa bidhaa ni imara. Halafu makabati mengine nimeyaona hata kufunga vizuri hayafungi yanakata viuno..hivi ni kwa nini?
 
tutafute tupo tabata tunatengeneza sofa za kisasa makamabati ya kila aina ya kisasa na meza vitanza vya kisasa vyenye quality ya urope na usa na sio quality ya keko njoo ufurahie nyumba yako nicheki whatsap 0715426668
 
Mkuu Keko ndio kila kitu kuhusu mambo ya fenicha kuanzia keko magurumbasi hadi keko bora,ila jaribu kwenda na mtu anayejua mbao vizuri usije ukauziwa kitanda cha muembe 4 kwa 6 baada ya mwezi kitanda kinatanuka na kuwa 6/6

kwi kwi kwiiii
 
Sawa nitamcheki Sacheques @ Instagram - mke wa mtu & rubii

Mdau uliyesema kuhusu waturuki, wengi wao nimewaona mikocheni..bei juu ila naona bidhaa na huduma zinaridhisha sana. Shukrani alikhalef

Asante mkuu nitajitahidi nitembelee ofisi zenu, je hamna tovuti nipate kupitia kazi zenu kabla sijawatembelea? kasuku mtu?

Sawa sawa..nitakuwa muangalifu nikipita huko maeneo ya keko wakuu KakaJambazi Mtoto Tajiri & BONGOLALA
Belo asante, nimeipitia hiyo tovuti ya Fancy Home Decor. Naendelea kucheki kazi zao nipate mwangaza.

Home Shopping nitawacheki pia, asante sana Zamiluni Zamiluni
 
Last edited by a moderator:
Belinda,

Longtime.

Kwenye furniture, kuna mambo matatu makuu ya kuzingatia.
1. Look/finishing, 2. Quality 3. Price.

  1. Tukianza na look, yaani muonekaniko, furnitures nyingi ready made za Mchina zina good na good furnishing ila hazina quality kwa sababu zimetengezwa na MDF materials ambapo sasa hadi Keko nao wanatumia kwa sababu they are cheap!. Kufuatia umasikini wa Watanzania, hizi MDF ndizo kimbilio la wengi, na hata ukifika ofisi nyingi hata za heshima, office furnitures zao ni ready made za MDF ambazo they are just good looking lakini hazidumu. Kuna Watu wenye nafasi zao na uwezo wao, lakini bado wana opt for MDF kwa sababu wameamua hawataki furniture za kudumu sana ili baada ya muda wawe wanabadilisha, that being the case, wana opt for cheap imported furnitures za China, unaweza kwenda kwenye yale maduka lukiki ya furniture au hata Keko.
  2. Tukija kwenye Quality, hii inategemea ni mbao gani unaipenda ila the best quality ya mbao za furniture ni mti wa Mninga. Watanzania tunajitahidi sana kutengeneza furniture nzuri za Mninga ila tunaangusha na finishing kwa sababu finishing yetu inafanywa kwa mikono, hand finishing!. Sasa yameingia makampuni ya wenzetu ambao wanatengeneza furniture hizi hizi za Mninga, ila wanafanya finishing na mashine, hivyo ukiziona zinaonekana kama ready made!. Kuna Wachina wanaitwa Ocean Kiss Furniture duka lao liko pale Victoria opposite na jengo la GEPF na kiwanda chao kiko Shekilango pale Millenium Business Park, kiukweli sijaona duka lolote la kushindana na hawa Wachina kwa finishing. Wengine ni Wazungu fulani wako Mikocheni njia ya Coca Cola, kiwanda chao hapo nje wameweka alama ya kiti kikubwa cha mbao. Hawa Wazungu tatizo lao, ni mpaka uweke order na inakubudi kusibiri kwa 60 days, kwa sababu ukiisha weka order ndipo wananunua mbao na kuzikausha na kuzitreat for 30 days kwenye mashine zao, ndipo waanze kutengeneza, ila finishing product yao ni kama ulaya!.
  3. Mwisho ni suala la gharama, good things costs money!. Kama umejaaliwa uwezo, na unahitaji really good stuff, nenda duka linaitwa Cleopatra, liko Nyerere Road baada ya Hyundai, mule wameweka imported classic furniture kama kwenye nyumba za wafalme, wanaangiza furnure zao kutoka Egypt na Uturuki ambazo ni za mbao kweli na kazi yote ni hand made ila tatizo bei!. Mfano kuna sitting room set inayomatch na dining set inauzwa M.45!. Kiukweli nyumba yako unaweza kuigeuza a palace!. Na hata kama huno hizo M.45 sio mbaya kupita na kuangalia tuu, kwa sababu bila ku wish, you can never get!. Mtu mwingine anayeteta funiture nzuri, ni dada mmoja anaitwa Lydia, yeye ana import from US kwa kutumia Catalog mbalimbali ikiwemo Peter Justinten. Yeye yuko Mikocheni Opposite KFC, kibao kimeandikwa All Americans.
Pasco
 

Longtime kweli mkuu..ila salama kabisa, majukumu tele.

Asante sana kwa mchango wako kuhusiana na hii mada..umenifungua macho kweli. Naifanyia kazi hili suala kati ya May na June, hivyo nilipenda nijipange ipasavyo na kama kawaida JF hukosi mawazo na michango murua kama huu wa kwako. Shukrani tele Pasco.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…