Kuelimika ama kujifunza kitu ni juzi, jana, leo na kuendelea. Inategemea na kizazi na wakati. wakati mwingine hata teknolojia.
Kwa mfano: utaratibu wa reboot pc na kuingia kwenye desktop bila kufungua windows hufahamika kwa watu wachache. (utaratibu huu hutumika pale window inapokuwa ime corrupt na mtu anakuwa hana uwezo kabisa wa kuwasha PC yake na windows recovery option zote zimeshindikana! ila mtu anataka tu kuokoa documents zake zilizo kwenye desktop ya computa yake ambazo zitapotea kama ataformat au kuweka window nyingine)
Sasa ikitokea mtu akapost maelekezo namna ya kufanya, wapo watakaosema "hii mbona ni kawaida tu ya siku zote" na wakati huo huo jambo hili litakuwa geni kabisa kwa watu wengine na watajifunza na itawasaidia sana!
Sasa basi, mtu anapoweka maada ambayo kwako sio ngeni, usione kama anapoteza muda, wako wachache ambao hawaelewi. na itawasaidia.
CHA MSINGI NI KUHESHIMU TU MAWAZO YA KILA MTU MAADAMU HAVUNJI SHERIA WALA HAKIUKI MAADILI.