Furaha yenu izidi kuimarika

Furaha yenu izidi kuimarika

Joined
Dec 1, 2018
Posts
12
Reaction score
29
Mwanafalsafa wa Ugiriki aitwae Democritus aliwahi kusema kuwa "happiness of the man should not be upon the things of the world because the things and treasures of the world come and go, rather the happiness of the man should be upon his inner dignity" Democritus alimaanisha kuwa furaha ya mtu isitegemee mali na vitu vya dunia bali itegemee hali yake ya ndani.

Nimeamua kutumia haya maneno kuwatia moyo wapinzani kuwa furaha yenu izidi kuimarika pamoja na kwamba mnateswa na kuonewa kama vile nyie ni wakimbizi katika nchi yenu huru, mnateswa na kuwindwa, mnaporwa mali zenu kila kukicha na kupigwa minada kwa vigezo vya sheria mbovu kandamizi.

Amini msiamini Mungu yupo na daima husimama na wale wanaoonewa na kukandamizwa naamini hamtakufa kabla Mungu anayeona mateso yenu hajawatetea kwa kuwapa haki zenu.

Hivyo basi muwe imara huku furaha yenu ikizidi kuonekana mbele ya watesi wenu maana furaha yenu ipo kwenye utu wenu na misimamo yenu ya haki, daima Mungu awe nanyi.
 
Yesu hapa namkumbuka alipokuwa huku Duniani akituonesha njia aliwahi kusema ".... uzima wa mtu haupo katika wingi wa mali alizonazo...."
Sure, Jesus is the saviour!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom