Furaha Dominic leo ataendelea na Mahojiano. Je, atawataja Kupe waliomnyonya hayati Magufuli?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,966
141,974
Furaha Dominic ni mpwa wa hayati Magufuli.

Jumatatu alikuwa na mjadala katika kipindi cha The Big Agenda kinachorushwa na Star tv. Kutokana na mambo mengi aliyokuwa nayo muda wa kipindi haukutosha hivyo mtangazaji nguli Aloyce Nyanda aliahirisha hadi leo saa 3:30 usiku.

Furaha awali alielezea namna hayati Magufuli alivyokuwa amezungukwa na watu waongo, wazushi na wafitini (KUPE) waliosababisha wakati mwingine afanye maamuzi yasiyo sahihi yaliyoumiza wasio na hatia.

Pili, alielezea namna Wasiojulikana walivyomuwekea zengwe hadi akaukosa ubunge wa Kawe.

Tatu, alielezea namna mbunge wa sasa wa Kawe mh Dkt. Gwajima alivyo muongo wa viwango vya kimataifa.

Mwisho, alisema yuko tayari kuwataja KUPE wote waliomnyonya damu mjomba wake ili wasije kumharibia Rais Samia katika uongozi wake wa awamu ya 6.

Je, atawataja?

Mungu wa mbinguni mpe wepesi Furaha Dominic.

cc: Pascal Mayalla

Maendeleo hayana vyama
 
Asichokoze Nyuki…tutafungulia Mzinga kuonesha umungu mtu wake pale kwa Mkemia Mkuu wa Serikali wakati wa utawala wa Kaka wa Mama yake!
 
Back
Top Bottom