Funzo muhimu sana kutokana na zama tulizopo hasa 21st century

Ibnuyawar

Member
May 6, 2020
49
149
Kulikuwa kuna ndugu wawili mwanamke na mwanaume, lakini hawa ndugu walikua ni mayatima wazazi wao walishafariki.

Sasa kwa bahati mzuri huyu wa kike akapata mume akaolewa na akabahatika mtoto mmoja wa kiume.

Baada ya muda fulani pale kijijini pakatokezea ugomvi mkubwa, mpaka mume wake na kakaake pamoja na mwanawe wakaenda kugombana na bwana fulani pale kijijin na katika kugombana mpaka ikafikia hatua yule bwana wakamuua.

Alipofariki yule bwana kesi ikapelekwa mahakamani, na baada ya kusomwa kesi yao jaji akaamua kua wote watatu wauliwe, (mume, kaka na mtoto).

Sasa yule dada akamwambia jaji “ ikiwa umeamua kumuua mume wangu na kaka yangu na mwanangu basi na mimi pia haina haja ya kuishi tena hapa duniani, bora na mimi niuliwe tuu.

Jaji akajibu: Sikiliza nimekuonea huruma chagua mmoja kati ya hawa watatu ili asiuliwe na wawili watauliwa.
Dada akasema: Sawa ila naomba unipe masaa24 nifikirie zaid wa kumchagua, jaji akakubali.
Yule dada akarudi nyumbani, shemegi zake wakamwambia, usikubali mume wako auliwe sababu ndie anaekutizama na kukusaidia kwa kila kitu.

Wakaja wengine kumshauri wakamwambia, usikubali mtoto wako auliwe sababu huna mtoto mwengine. Yule dada akanyamaza kimya hana la kusema akabaki na lake rohoni tu mpaka siku ya hukumu ilipofika. Akaulizwa sasa unataka nani asiuliwe? Akajibu mimi namtaka kaka yangu, akaulizwa tena mume je?

Akajibu nasema namtaka kaka yangu. Akaulizwa tena mtoto wako jee ? Akajibu namtaka kaka angu. Sasa jaji akasema sawa nimekuskia lakini nataka unifahamishe kwa nini ukamchagua kakaako?

Mama akajibu “ewe jaji mkuu huyu ni kaka yangu na sina kaka mwengine, sasa huyu akisha kuuliwa nitapata wapi ndugu mwengine mimi? Lakini mume akifa kwa uwezo wa mungu mimi nitaolewa na mume mwengine na kwa kua nitaolewa nitazaa mtoto mwengine.

Jaji ikawa amefahamu alichokusudia yule dada, akaingiwa na iman ndani ya nafsi yake akasema : basi nimekusameheni nyote watatu.

Mazingatio:

Sikusudii kua mume ni mbaya wala mtoto wala kaka ila ni funzo kwamba, kaka yako au dadako atabaki kua ni ndugu yako tu lakini mume au mke mukiachana atabaki kua mtalaka wako au alikua mke wako tu .

Kwaio wapende ndugu zako na usiwe ni mwenye kuvunja udugu kwa hali yeyote ile.
Au wewe unaonaje?
 
Back
Top Bottom