Funzo: Mapenzi imara yatakayodumu muda mrefu

shadownet

Senior Member
Aug 4, 2015
133
1,000
Umewahi kuwaona watu ambao miaka nenda rudi tangu umezaliwa umewakuta wanapendana na mpaka sasa umekuwa mkubwa wao ni vikongwe bado wanapenda na ukajiuliza “HIVI SIRI YA MAPENZI YANAYODUMU NI NINI”, Well karibu katika lesoni hii itayofafanua siri za mapenzi yanayodumu.

Kwa zama hizi kumekuwa na ongezeko kubwa la wenza kuachana aidha kwa kukimbilia divorce ama talaka zisizo na idadi, Nisingependa na wewe ndugu yangu uishie kwenye hili sokombingo ambalo limesomba wanandoa lukuki wa nchi hii., Hapa nitakupa dondoo za kukufanya uishi katika mapenzi na mwenza wako kwa muda mrefu kwa furaha tele.

USITEGEMEE 100% USHAURI WA WAZEE KUHUSU NDOA IMARA ITAYODUMU.
Mvinyo mpya unahitaji kibuyu kipya, Mambo ya kuweka mvinyo mpya kibuyu cha zamani ni savage. Enzi za babu zetu zishapita na sasa tupo kwenye zama yenye mazingira ambayo mababu zetu hawakuyaishi, Chukua ushauri wa wazee lakini usiutegemee 100% kuwa utafanya kazi katika kizazi hiki chetu cha whatsapp,ushilawadu, selfie, n.k , Mawazo ya wazee changanya na zako.​

Unaposhauriwa mawazo na hawa wazee wetu changanya na akili zako ili ujue kama ushauri unafaa, Haufai au kama kuna njia ya kuuboresha.Mfana mzee anakwambia motto wa kiume “Njia ya kuwa na ndoa ndefu oa wake watatu ili kila moja wao apate attention yako”

I swear utapotea kwa hiki kizazi, Mtoto wa kike unaambiwa na bibi”Kama unataka ndoa ndefu mtii mme wako kwa kila analokwambia” Kwa kizazi hiki ukitii kila amri wewe ni mzigo kwakweli maana hutakuwa na wazo la kutoa ambalo linaweza saidia ndoa yenu.

AMINI MOYO WAKO ,TII KICHWA CHAKO, PUUZA MATAMANIO
Kumpata mwenza bora ni zoezi la akili na moyo kukubaliana kwamba ulie mchagua ndie sahihi, Poleni washkaji zangu ambao mnavuta jiko kwa kigezo cha T*ko na kina dada mnaokubali kuolewa kisa fulani ana pesa MTAUMIA KWENYE NDOA!!!!.

Tafuta mtu ambaye ukimpigia simu kumwambia “Baby nakuja nyumbani” hio nyumbani iwe yeye na sio mali au mgegedo, All in all tafuta mtu ambae mnashare malengo na mnapendana kweli kweli.

MAONGEZI NI NGUZO YA MAPENZI, KUPIGIANA KELELE IWE MWIKO.
Hapa mawasiliano namaanisha kuongea na wala sio kupigiana kelele, Kama mtu mnapendana nakuhakikishia kitu cha kuongea naye huwa hukifikiriii sana mana unakuta tu maongezi yanendelea automatically.

Kuna mapenzi mengine yanakera!!! The so called mpenzi unamuona yupo kabisa online na anabadilisha picha lakini ukimtext yupo kimyaa, Hayo sio mapenzi ndugu huko ni kuvumiliana . Hakikisha mtu unaemtaka kuwa part of your life unaongea nae vizuri na sio kupigiana nae kelele.

SHAKE WELL BEFORE USE.
Hamjafikisha hata miezi mitano na mnataka muone wazazi wenu wawape ruksa ya kuoana, Hao wazazi wenu wenyewe wamewaona baada ya miezi tisa toka wawatengeneze, Hii ni serious problem, Mtu unae panga kuwa naye kwa miaka 40 haiingi akilini eti umemjua kwa miezi miwili tu unataka ndoa.

Wanadamu tuna siri na kibaya zaidi tumepewa akili ya kuzificha lakini muda ndo huziweka wazi, Time tells, Jaribu kufahamiana na huyo mwenza wako kwa kipindi cha mwaka moja angalau umjue vizuri nje ndani na uhakikishe uamuzi unaochukua ni mzuri, HARAKA HARA HAINA BARAKA.

ENDELEZA UTAMADUNI ULIOTENGENEZA PENZI LENU.
Huwa naccheka sana couples zinavyoanza isingizio kwamba hawawezi kufanya kitu Fulani kama enzi za uchumba kisa ndoa, Hapa ndipo penzi linaanza kuwa la kuvumiliana na sio la kufurahiana. Penzi lenu mkiwa wachumba lilijengwa kwa zawadi zawadi ndogo, Kwanini uache kuendeleza huu utamaduni uliotengeneza penzi lenu.

Kama ulikuwa unampelekea mpenzi wako vizawadi kama pipi endelea na huo utamaduni angalau kwa wiki mara moja, Kama mlikua mnapeana hugs na kisses kabla ya kwenda kazini endeleeni hata mbele ya watoto, Kama mlikuwa mnacheza mziki enzi za uchumba wenu sio mbaya kujikumbusha enzi zenu hata mkiwa chumbani peke yenu.

Kwa ufupi vizawadi na kusifiana mfano “Oh dear umependeza” ni vitu ambavyo vinatengeneza uchumba, Usiache huu utamaduni mkioana.

MUHESHIMU MWENZIO, USIRUHUSU HASIRA ZIKUTAWALE, TABASAMU NI SILAHA KALI
Heshima ni mzizi wa mapenzi, lakini hii heshima ni nini hasa???, Heshima ni mwendelezo wa kujali hisia za mwenzako, Kuwa mvumilivu kwa mapungufu aliyonayo mwenzako na mwendelezo wa tabia kama kumsifia mwenza wako . Kuna baadhi ya maneno pia yana ashiria kuheshimiana kama Ahsante, Umefanya vizuri, Pole, n.k yanweka heshima kinywani.

Uvumilivu ni kitu ambacho pia katika kuheshimiana katika mapenzi, Mapenzi ni mithiri ya kushuka na kuoanda na kitendo cha kumkimbia mwenzako katika kipindi kigumu ni ishara tosha kwamba humpendi na huwaweza kuishi nae muda mrefu wenye shida.

Chukulia mfano wimbi la vijana wa sikuhizi, Ndoa wameka miezi misita moja wao kaona upepo wa kiuchumi haupepei vizuri basi yeye anachowaza ni divorce/talaka, Hiki ni kiashiria tosha hakuna heshima ya ndoa .

Hasira zako za kwenda mbali mpaka uanze kumchunia ama kumkomoa mwenzi ni mazoea yatayogeuka kuwa tabia, Tumia akili ky=utataua tatizo ambalo linaweza kutatulika na hakikisha tabasamu iwe silaha yako kuu katika maongezi na vitendo, Mwenzio akiona unatabasamu basi jua kwa namna moja au nyingine unamuondoa hofu kubwa sana juu ya mawazo kwamba hujisiki vizuri

MWISHO KABISA NAMALIZIA NDOA NI BAADA YA HARUSI


MY OTHER POSTS

Funzo: Mapenzi imara yatakayodumu muda mrefu
Jifunze kupendwa ndani ya dakika chache
Jifunze mbinu za kujitegemea kiuchumi na kuwa tajiri
Jinsi ya kupata marafiki na kuwafanya wafanye unachotaka
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
6,691
2,000
DARASA TOSHA KWA MAPENZI MUBASHARA.SIKU HIZI MADARASA YA MAPENZI NI MENGI SANA LAKINI MAPENZI YANZIDI KUEGEMEA KWENYE PESA
 

Marlex Jr El

JF-Expert Member
Nov 6, 2015
1,766
2,000
Mwanamke upenda kwa kusikiliza na Nwanaume upenda kwa kuona...
Hii ina maana mwanamke masikio yake ndo nyenzo yake muhimu ya kupenda kwa mwanaume ni macho.
Ewe mwanaume tenga muda wako angalau kila siku saa moja au nusu saa ya kufanya mazungumzo na mke wako au mchumba na hata mpenzi wako kwa kufanya hivyo hata tatizo la wewe kuchunwa pesa sahau.
Ewe mwanamke jaribu kupendeza siku zote zaidi na zaidi tofauti na siku ambayo mume wako, mchumba hama mpenzi wako mlipo kutana kwa mara ya kwanza maana kupenda kwa mwanaume ni katika kutizama (kuona) kufanya hivi kutaondoa mwanaume wako kutafuta mpango wa kando.
Zingatia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom