Funzo kwa wewe mwanachuo (copied somewhere)

kamati yamaamuzi magumuu

JF-Expert Member
Nov 14, 2019
227
262
EWE MWANACHUO, TAMBUA MAZITO HAYA 2019 INAPOKUAGA, NJOO KIVINGINE 2020. TAFAKURI KALI BALA JUMAPILI YA LEO.

Unaposhangilia boom, usomi ama sherehe za graduu ndani ya joho hadi unajaa nyodo na mishauo hata ukadharau wengine usiyasahau kabisa haya:

Na Power Lufunga, the foresighted living philosopher;

EWE kijana msomi uliyeko chuoni, Unayehitimu sauti kutoka nyikani sikia, ubongo fungua maarifa kuyasharabu, vinginevyo elimu yako si ukombozi Tena Bali Ni mzigo wa kukutia fedheha na uoga wa maisha na kukuchelewesha maisha tu.

Kwamba primary school ulikaa miaka 7 kumbe hapakuwa kwenu licha ya kuzoeana na marafiki, waalimu na jamii za hapo, hatumae siku ilifika ukaondoka, Seko hata Advance hapakuwa kwenu, ulipita tu na pengine marafiki wote uliowahi kuwa nao hata chumba au geto Moja Leo hauna hata namba zao za simu.

Hayo yanakukumbusha hata hapa chuoni siyo kwenu na haujatoboa maisha bado, siku yaja nayo haiko mbali unaondoka hapa na kwenda kuganga huku ukitarajiwa na ndg, jamaa, wazazi na Taifa kuwa msaada wao, yajue haya

Mbwembe lukuki, majivuno na hamasa kubwa unaripoti nayo ukiwa first year Tena kwa matumaini na imani kubwa kuwa ndoto zimetimia na hata kuanza kudharau na kupuuza marafiki na wengi uluowahi kuwa nao.

Taratibu akili inakusogea uwapo mwaka wa pili baada ya kuona mbereko za chuo, masomo na uhalisia wa maisha ya taaluma yako huko field, hatimaye mwaka wa 3 unakomaa kiakili na aidha kujutia uliyoyaishi miaka yote hapo chuoni.

Elimu Ni maarifa, maarifa Ni ajira, ajira Ni maisha!

Mambo haya tunayajenga shuleni. Cha ajabu wengi huitazama elimu Kama ajira zaidi ya maarifa na hivyo kuishi kwa kuamini akimaliza shule tu ataajiriwa jambo ambalo kwa wengi si halisi na wengi wamejutia maisha baada ya Chuo kuisha.

Uliyepo first year huenda tusielewane vizuri ila kesho utamtafuta wa kukusaidia elimu hii na hatatokea, tafakari mazito haya

Unaposhangilia kula boom, jumuiya kubwa chuoni, maisha ya gharama na kulala kwenye maghorofa ya Chuo au geto Kali hapo mjini, tambua Ni kipindi Cha miaka 3 tu na baadaye huenda utajikuta hauna namna nyingine ispokuwa kurudi kwa Bibi yako, mjomba au kwa mama kijijini na kwa Hali ya kisiasa na kiajira pengine ndo basi pamoja na taaluma zako, mbwembwe na Uslayqueen/ uslayking wote kubaki historia isiyojirudia.

Na hapo ndipo msemo "majuto Ni mjukuu" huaminika.

Kijana msomi, jifunze kutazama kesho, jione "muda Kama huu mwakani, miaka miwili ijayo utakuwa wapi. Ndiyo una ndoto na malengo lakini haitimii kirahisi Leo Wala kesho na maisha lazima yaendelee, ubongo fungua, mulika kesho, jione sehemu maisha yakiendelea.

MAHUSIANO NA MAISHA.

Kama kuna Mambo kijana msomi waleo anaogopa na kuyatumia vibaya Ni mahusiano na maisha.

Vijana wengi wa like wawapo chuoni, mahusiano ni uchumi, Ni kudeti, Ni pesa na starehe!!, Na wakiume wengi Ni ustar, kula starehe na kuacha!!. Hakuna wanachoogopa Kama uchumba, ndoa na kujitegemea.

Hii imefanya, licha ya wengine kupata vijihela vya hapa na pale aidha kwa udhamini, kuishi maisha ya anasa bila hata kuona namna ya kujibana na kujiwekeza, wengi wamepata kuwa na mahusiano na watu wengi bila malengo yoyote Ili kukidhi mahitaji ya ujana na mwisho wamerudi kwao kutulia wakisubiri upepo wa kisulisuli wapate wenza waanze maisha baada ya kukiri Hali ya mtaani na nyodo za kipindi Cha chuoni kuwakwisha.

Nami nawaambia, Ni vema sasa tukijua maisha ya Chuo yanapita na pengine Ni mwisho kwa wengi kusoma na wachache watabahatika kusoma shahada zingine Bali Ni chuo vilevile, kumbe chuoni Ni hatua ta mwisho wa kusoma na baadaye Ni maisha na kujitegemea.

Je unajiandaaje? Kuburuza mabegi kurudi kwa shangazi kutulia bila mbele Wala nyuma itasikitisha!

Ni vema sasa tukijiepusha na anasa, maisha makali yakishikaji, tukaheshimu suala la mahusiano pia kwani huenda pia hapa Ni sehemu sahihi kumpata mtu sahihi wa kupanga future naye pamoja na maisha baada ya Chuo kuyakabili na si kuburuza mabegi kwenda kutulia kwa mjomba kungoja ajira ambayo hujui lini itatoka.

Ni vema sasa tukijibana kwa kidogo tupatacho, tukajua kesho pia tutahitaji kuishi na hivyo tukajiwekezea hata kwa kufungua biashara ndogondogo na tukijua tuendako baada ya Chuo Ni gizani tutaweza kujipanga mapema.

Pia tusome kwa bidii, tuepuke kufeli mitihani, ili maisha yetu chuoni yasiingiwe dosari, tuishi vema na watu kwani hawahawa tulionao Leo baada ya Chuo tutaanza kuwaona katika nafasi za juu serikalini, bungeni na wizarani, wasanii wakubwa, wafanyabiashara wakubwa, watumishi nk.

Kumbe kuishi vema na Hawa tunaojyana nao Leo Ni hazina kubwa Sana kwetu Leo na hata kwa watoto wetu.

Na hii ndiyo iitwayo kesho inajengwa Leo, na hivyo kwa matendo yako, maadili yako, kauli zako kwa wengine, machaguo yako na maamzi yako ya Leo unaijena ama kuibomoa kesho yako hiyo

Nami nawaambia, utakayoshindwa kuyafanya Leo ungali chuoni yatakuwa magumu Sana baada ya kumaliza Chuo maana utakuwa huna Tena uhakika hata wa Laki Moja kwa miezi minne, boom kwaheri, utakuwa na changamoto za kuwaza ajira ambayo huenda ikajificha zaidi, huenda utakuwa kwenu kijijini ambako hakuna hata mtandao wa simu wa kujua fursa zilizopo, hautakuwa na Hawa marafiki mnaopeana nao vichwa Leo na kuyapuuza mambo ya msingi ya maisha.

Kwa hakika vyuma vitakaza Sana. Kumbe Ni vema sasa ukiyajua na kuyafanyia kazi haya ungali fursa unayo.

Je wewe unaogopa Sana mambo gani? Yapi unayaendesha je? Unadhani kesho itakuwaje? TAFAKURI jenzi na ndivyo Mwana wa Lufunga natua pen.

POWER LUFUNGA@THE VERY CRITICALLY ARGUING FORESIGHT LIVING PHILOSOPHER

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli mtupu kwa kweli nahisi walegwa wanabidi wazingatie hili kwakuwa Huu ukweli ni zaidi ya ukweli

Ambaye akifanikiwa kufuata Huu ujumbe atafika mahali pazuri sana baadae na utakuja kuwa kumbukumbu
 
Back
Top Bottom