Funzo kutoka kwa Jenerali Constatine Chiwenga

Funzo kutoka kwa Jenerali Constatine Chiwenga

comrade igwe

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2015
Posts
7,295
Reaction score
3,952
chiwenga-2.jpg


Jenerali mzalendo, mahiri na mfano wa kuigwa barani Afrika, uzalendo wake hasa katika kuilinda katiba ya Zimbabwe, ni Jenerali kutoka kabila la Washona huyu sio mwingine bali ni Jenerali Constantine Guveya Chiwenga mwenye kutumia akili sana katika maamuzi sahihi na wakati sahihi, Jenerali Constantine Guveya Chiwenga baada ya kuhisi katiba inavurugwa na Rais Mugabe katika mustakabali wa kuongoza nchi alifanya maamuzi yaliowastua watu wengi sana duniani hususani viongozi wa Afrika katika kuheshimu na kuilinda katiba ,mafunzo yanayopaswa kusomwa sana ni utulivu, uvumilivu na hekima vilevile akili ya hali ya juu sana katika kuwasoma viongozi na familia zao hasa katika kuilinda katiba, katika suala kubadili uongozi wa nchi ili asionekane kama amefanya mapinduzi ya kijeshi kwa kuwa anajua fika yanapingwa duniani kote,wala sio kupindua nchi kama wakuu wengine wa majeshi hususani nchi za Afrika magharibi.
 
Natabiri Maumimivu Yakizidi Doto Atafanya Kama Alivyofanya Kurwa Zimbabwe
 
Sijawahi kuona jambo kama hili katika maisha yangu...
Mungu amjalie maisha marefu na baraka tele... kumtoa mtu mwenye tamaa kama yule babu sio kazi ndogo, kaepusha umwagaji wa maelfu ya raia wa Zimbabwe... anastahili tuzo ya heshima ya amani ya nobel.

Tunahitaji watu wenye hekima kama hawa, God bless him na taifa lote la Zimbabwe kuelekea uongozi bora unaojali demokrasia.
 
Tungekua na jenerari kama huyu ungekuta lile jamaa lenye kipara halipo nchini...
 
Mimi nimependa jinsi alivyofanikisha power transition kwa amani bila hata kudhuru sisimizi zaidi ya mapolisi kutandikwa kama watoto wadogo. Jamaa iko akili mingi sana yule; hiyo coordination na majenerali wenzie; nani afanye nini, wapi, na kwa muda gani bila "adui" kustuka sio akili ya kawaida. Paaap, wananchi wakaona mavifaru yametanda mitaa ya Harare huku wakihubiriwa "habari njema" ya amani; amani; amani!

Tulieni tunapambana na wahuni (sio wapinzani) wachache wanaokusababishieni maisha ya taabu. Mara ghafla, wakapata support ya ajabu ya wananchi (yaani the people's power) bila kujali rangi zao, dini zao, kabila wala umri wao; duh! dikteta aka-confirm siku zake zimekwisha naye mbwa asiye na meno AU akibweka lakini kila mmoja akamdharau; rubbish!
 
Huyu General anafanya historia ya kipekee ambayo nchi zote duniani ninatakiwa kuiga. Atakumbukwa Zimbabwe kama shujaa. Wale ambao kazi yao ni kuua raia kwa excessive power and force kwa jambo dogo tu wajifunze kwa huyu generally. Kwa nini watu tuishi kwa hofu ya Mtutu ya bunduki? Kwa nini tunaoona marehemu kila kona wakiwa wamekufa kwa mateso? Nimeumia mno kama mzalendo mpendw amani. Tunapofanya maovu jwa binadamu tujaribu kufunga macho na kumuangalia Mungu aliyetufia msalabani ili kukataa damu nyingine isimwagike tena. Sad Africa.
 
Back
Top Bottom