dada umenigusa kweli,,, na ndo maana napenda kuwa na mtt wa kike,,, wasichana huwa wanakumbuka wazazi kuliko mtu mme... lipo wazi kabisa....mie mpaka dada zangu walianza kuniwekea vikao.... namshukuru Mungu waliweza kuniweka sawa....nlijisahau kabisa...mpaka wakasema wifi yao kanilimbwata.... kumbe ni akili tuuu....hongereni wanawake wote katika hili......ni kweli kabisa nyumbani muhimu sana, nimeona watu wanaishi mjini vizuri ukiona kwa wazazi wao ni balaa hapaingiliki. wanaume wajifunze kwa hili watoto wa kike wanajitahidi sana.
hahahahahahaa.... umeona kuna anaebishaaa?? kimyaaaaa,,, tumeimeza silencer....Hili tatizo liko kwa wanaume sana kusahau kwao,,,, hope watabadilika!.
Nimeikuta sehemu hii.
Vijana hebu jifunzeni, mzazi alokuzaa anastahili kuishi mahala pazuri kama wewe una uwezo! Acheni ujinga wa kununua altezza, kutanua kwenye majumba ya starehe wiki nzima, kula kwenye restaurant za maana, kuhonga mademu simu, kununua viwalo vya bei mbaya wakati mzazi wako anaishi kwenye nyumba ya kiwango duni! Ndo maana kila leo mara altezza imeingia mtaroni, mara simu imeibiwa, mara demu ulomgaramikia kaku-dump, mara umetuma pesa kibao kwenye wrong number and the like mishaps...,ni laana ya kuacha mzazi na maisha duni huku we ukitanua mjini. Fungukeni macho vijana esp wa kiume!
The truth shall set u free.
Pole sana kama uko humu kushindana.. Sioni kama hii imelenga upande moja, hii imelenga kote kwani wanaume tu ndio wa kuwakumbuka wazazi? Wazazi hukumbukwa na kila mtoto regardless jinsia, usiweke kichwani kia mwanaume ndio kila kitu nyumbani utakua weak sana ndio maana madingi wengine wanavuta mizigo pembeni, sababu wnawake wanataka wakae ka mizigo tu, tena anataka na house girl juu... Mi nikioa siwezi kuacha mke akae tu bila mishe, kama hana kazi ntamfungulia biashara aweze kujitegemea baadhi ya vitu sio nikifa na familia nayo imekufa...Zamu yenu wakaka/wanaume imefika, ngoja na nyie tuwape vidonge vyenu na mjitahidi kweli kuvimeza kama sie tulivyovulimilia kuvimeza. Na ndio imeanza hivyo!
siku itokee msiba au jambo lolote linalolazimu watu wakusanyke kwao ndio utawajua wakat wanahangaika kujenga hadi kajumba kasiku 5 ili mradi kufuta aibu....
ukweli tunapaswa kutengeneza pa kufikia kwanza, mimi ni mojawapo nilivyoanza kazi nilimjengea mama na baba nyumba na nashukuru sasa wamehama kutoka tembe kwenda bati, kutoka ngozi hadi godoro, kutoka kuvujiwa hadi kutokuvujiwa, wamefurahije, wamenibarikije, usiombe Baraka Mwanzo mwisho, naendelea kumwomba Mungu awaongezee siku za kuishi nioe wawaone wajuku zao, Wazazi wanabaraka sana asikudanganye mtu, kwa wale ambao
hawana wazazi nawashauri Mjenge makaburi yao! UA BLESSED
Wachaga hoyeeee
Kuna ka ukweli hapa.
Thanks God nimefanikiwa kumjengea Mama mzazi nyumba nzuri sana. Soon nitaanza kujenga ya kwangu. Na kwenye pato langu la kila mwezi Mama anapata 4%.