Funguka Mbunge Wako Yukoje?


Nimecheka hadi kuchanganyikiwa..... Mbavu za mbwa?
 
Mimi pamoja na kuwa ni mkazi wa Mbagala, ukweni kwangu ni Madesa-Jimbo la Chalinze. Nina shamba na nyumba huko. Mbunge wetu huko ni SAID BWANAMDOGO. Kama mwezi hivi uliopita nilishamlalamikia humu jamvini, manake jimbo letu hilo ni kama lipo wazi. Manake huduma za afya ni kama hakuna kabisaaa, zipo duni mno, hadi watu ni kama wameshahalalisha huduma za 'kienyeji' style; Mto wami unapita katika vijiji vingi, lakini hakuna mkakati wowote wa kuanzisha kilimo cha umwagiliaji; Kilimo kwa karibu 100% kinategemea jembe la mkono, hata teknolojia za jembe la kukokotwa na ng'ombe hakuna, matrekta ni ya kuhesabu nk; Shule nyingi ni hoi kabisa! hakuna maabara, madarasa, mabweni, vitabu na waalimu wa kutosha; michezo hakuna kitu kabisa; NA hakuna jitihada za wazi za kusambaza umeme vijijini. Zaidi bungeni hasikiki kabisa, iwe katika hoja binafsi, maswali ya msingi wala maswali ya nyongeza! Zaidi hajaweza hata kujitokeza na kukukutana na wadau wa jimbo ili kubadilishana mawazo tufanyeje ili kuendeleza jimbo letu. Kwa sasa wanakijiji wamezamia kabisa katika unywaji pombe za kienyeji! sijui ni stress au vipi? Kumbuka hili ndio jimbo ambalo tumetoa rais wa sasa wa JMT.
 
Ukisikia Gogo lilolala, Zoba lililozubaa, Domo zito kama zege, Zigo lisilo na tija, basi ndio Mbunge wangu.

Tatizo ni kuwa wapo watu (wazee) huko jimboni kwetu walipoona ati kafanya kazi kama Daktari wa Nyerere kwa muda mrefu wakadanganyana kwamba atafaa kuwa Mbunge!

Alipoingia tu na kuuona utamu wa Ubunge akaung'ang'ania vipindi 3 na kipindi kimoja JK akampa u-Waziri wa Afya! Mwaka 2010 alipita kwa mizengwe kura za maoni na hata hivyo kwenye kazxi ya uWaziri alikuwa dhaifu mno JK akamtoa...kilaza asiye na busara...!

Jimboni kwake wakazi wengi wanategemea kilimo, yeye alichofanya ni kuwaongezea machungu kwa kuunga mkono vi-ushirika vya kinyonyaji! Majanga....lakini ndugu zangu nao wanavuna walichopanda
 
Wote mna afadhali Mimi cjui Km mbunge yu hai au mungu kashamchukua, maana toka alivyopata ubunge kimazabe cjamuona jimbon kwetu, kuna jamaa yng mmoja aliniambia cku moja amemkuta nyantare anakula monde, jimbo letu sasa hv ndoo ya maji tunanunua tsh500, karibun jimbon kwetu segerea, kiwanja cha soko mbunge kafanya makaz Yale ya kudumu duuuuh!!!
 
Wa kwangu mimi ni Mwenyekiti wa Simba......... Amekwamisha hata uwanja wa Simba kujengwa kasema, "Serikali yenyewe ilijenga uwanja wa Taifa kwa miaka 50" Duh! Alshabab muongo kweli...........................
 
Mimi wa kwangu sikumpigia kura ila vilaza walimpa kura akapita sasa yeye kazi yake ni kuunga mkono hoja mia kwa mia.... Afu hachangii bungeni toka achaguliwe niliwahi kumuona mara moja akiuliza swali la nyongeza tena akitetemeka....Kila waziri akijibu hoja hata kabla ya kuanza kuongea yeye anapiga makofi kwenye meza....wapinzani wakiwa wanaongea yeye ananongonezana na jirani yake.....Mara nyingine hulala bungeni!!!
 
Mi wa kwangu mpaka naona aibu kumtaja,ni yule mla rushwa wa maccm mwenye kesi na Takukuru ya kuhongwa milioni moja.BADUELI LA BAHI.naomba M4C inisaidie,karibuni na mimi nachukua rikizo kwenda kuelimisha ndugu zangu.
 

Haa....!!!!! haahaaa!!!!.. !! Nahisi wewe wa Isimani.
 
yaani cjui kwnn nilikuwa cjaufungua huu uzi!, nimecheka mpaka basi!
..mi wangu jembeeeee,haogopi mtu, Msigwa, kiukweli mji ss unakua, barabara ya ir-dom,dom -arsh-mosh...inaendelea kujengwa kwa kiwango cha lami....japo kwa ss naishi town tena kwa jembeeeee Mnyika, yaani mule muleeeeee
 

...aisee,so interesting!
Pole sana mkuu!
 
Hahaaa mkuu kumbe tuko jimbo moja.Nimeipenda hiyo yaani badala yakusambaza maji yeye kutwa kucha anasambaza namba za viongozi ili watukanwe utadhani hao ndio waliotuomba dhamana 2010.

Kwa akili yako ndogo unazani kazi ya Mbunge ni kusambaza maji????? kwani yeye ni DAWASCO?????? Kama unataka mume sema binti!!!!!:A S kiss:
 
pole mkuu BARAFU...lukuvi ni janga...
Ss onana na ofisi ya cdm,M4C ipite huko, najua chiku abwao+Msigwa wapo huko ir town wanawakilisha!
..ismani naijua sana watu wameamka sana nwdays
 
Mimi wa kwetu simjui jina kwani anatumia jina la rais wa marekani wa awamu ya 44.Anapenda kutembea na kafimbo kama ka Nyerere,na huwapa baadhi ya wananchi wake bia,soda na wali nyama mara kadhaa.Inasemekana eti anamiliki ukumbi mkubwa wa starehe hapa Dar ndo maana anapenda sana kutoa offer za bia awapo jimboni kwake.Pia amefanikisha kuweka mawe kama tofali kwenye barabara ya jimboni kwake ili kuzuia utelezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…