Kaulizie Dagaa uone!Sasa jaribu kupika wali na nyama loooooooo! Twafa.
Akufukuzaye mjini hakwambii toka! Kwa bei hizi mjini kutatushindi narudi 'Malinyi' kupanda mpunga na kuasha kibatari.
tuache kulalamika, wenzetu huko japan wanaishi magorofani lakini kwa mboga za kutumia wanajitosheleza wenyewe. Wao wanapenda vitu fresh, so wamepanda mboga kwenye makopo, au kule juu kabisa wametengeneza concrete slabs ambazo zimewekwa udongo, sasa wa dar es salaama msiotaka kushika uchafu, hayo ndio matokeo yake.
Mchele, dagaa, nyama, sukari, maharage ,unga navyo kila mtu afanye namna ya kujipatia bila kununua?
Binafsi napenda sana wazo la kujiwezesha na ndivyo tulivyokua tunafanya kule kwetu Moshi, mtu ananunua mafuta tu na chumvi tu wakati mwingine. Ila Dar, sehemu ambayo wengi wanaishi kwenye nyumba za kupanga ambazo hazina hata sehemu ya kuotesha maua kujiwezesha huko hakuwezekani.ofcourse siyo kila kitu utaweza kujitosheleza, lakini kwa vile ambavyo una uwezo wa kuzalisha mwenyewe kwanini usifanye mwenyewe ukapunguza japo kidogo bajeti yako?
tuache kulalamika, wenzetu huko japan wanaishi magorofani lakini kwa mboga za kutumia wanajitosheleza wenyewe. Wao wanapenda vitu fresh, so wamepanda mboga kwenye makopo, au kule juu kabisa wametengeneza concrete slabs ambazo zimewekwa udongo, sasa wa dar es salaama msiotaka kushika uchafu, hayo ndio matokeo yake.
sasa wote tukikimbilia kijijini, mjini atabanana nani mpenzi?
Halafu huko kijijini mi sijazoea jembe meen?