Funga kazi!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Funga kazi!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jpinduzi, Dec 31, 2011.

 1. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #1
  Dec 31, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hii ni siku maalumu kwako. Tumia siku hizi kumshukuru Mungu na kumwomba Mungu kuhusu 2012. Mweleze Yeye mikakati yako yote uliyoipanga na umwombe akufanikishe katika hiyo. Omba kama Mungu atakavyokuongoza. Katika mkesha wa mwaka mpya nia muhimu ukitumia wakati huo kumweleza Mungu mambo hayo yote,(pamoja na familia yako kama unayo), imba nyimbo za sifa,na DUA za kumwomba Mungu.
  Mwisho napenda kusema;
  Mwaka mpya ni neema kubwa kutoka kwa MUNGU na wakati huo huo neema hii inaweza ikabadilika na ikawa ni adhabu na mitihani mikubwa kwa mwanadamu. La msingi ni kufuata mambo yanayompendeza Mungu. Kufanya hivyo, ndio mwaka wako utakuwa ni mwaka wa neema nyingi. Kinyume na hayo, mwaka wako utakuwa ni adhabu na mitihani na misukosuko mbali mbali ya kilimwengu..
  Tumuombe Mungu Atusamehe madhambi yetu yaliopita na Atuwezeshe kuwa na afya njema katika mwaka huu mpya, na Atuteremshie baraka na neema katika mwaka huu mpya.
   
Loading...