Fundisho la asili la nguvu za Mwanamke

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,578
3,485
NGUVU YA MWANAMKE
Siandiki ili kuwasifia Wanawake au kwa maslahi mengine yoyote yale isipokuwa kujifunza. Natamani kueleweka wazi kuwa maandiko yangu yote likiwemo hili ni kwa ajili ya kujifunza tu na siyo nje ya hapo.Siandiki ili kuifanya jinsia yoyote ile kujiona bora yenye thamani kuliko nyingine kwa sababu ninaamini katika ukamilifu na upekee wa kila kitu.

Kwa nini leo natamani tujifunze juu ya nguvu ya Mwanamke?..Msukumo mkubwa wa andiko hili ni uzoefu kutoka kwa Mama yangu na Mke wangu. Niliyoyaona na kujifunza kwao yanatosha kupata jambo la kujifunza.

Mwanamke ni mtu ambaye kwa asili ana uwezo mkubwa sana wa kuwa na subira.Uzoefu huu wa subira kwa Mwanamke unaweza kujidhihirisha kwenye mchakato mzima wa uzazi kuanzia kutungwa kwa mimba hadi kujifungua. Mchakato huo wote unamjenga Mwanamke kuimarika katika kusubiri au kungoja mchakato.

Katika kungoja "subira" mtu hukutana na changamoto nyingi sana mathalani mfano nilioutoa hapo juu wa mchakato mzima wa utungaji mimba unadhihirisha namna asili inavyomuandaa Mwanamke kuwa imara katika kungoja. Simaanishi kuwa nguvu hii ni kila Mwanamke anakuwa nayo ila nataka kuonesha namna asili inavyomuandaa Mwanamke kuwa na subira.

Wakati wa kungoja " kuwa na subira" unaweza kuwa ndiyo wakati mgumu zaidi na wenye changamoto nyingi sana lakini wakati huo ndiyo wakati muhimu zaidi wa mchakato utakaosaidia kupata matokeo. Kuna maumivu mengi katika kungojea mchakato maumivu ambayo hujenga uimara au misuli ya subira.

"Subira yavuta heri" ni moja ya methali inayoshadidia umuhimu wa kusubiri au kungojea na kwa maana ya andiko hili ni nguvu ya kuungojea mchakato na changamoto zake hadi kufikia lengo.

"Kuvuta heri" siyo jambo jepesi ila ni jambo linalohitaji kuwa imara " nguvu" na kuwa imara au kuwa na nguvu siyo jambo linalotokea kwa ghafla na kwa kulipuka tu ila ni jambo linalohitaji kulipa gharama.

Katika maisha ya kawaida tukiachana mfano nilioutoa karibu kila jambo Duniani linamchakato wake " process" mchakato ambao aghalabu hauhitaji kuwa imara katika kungojea/ kusubiri au kuwa na subira.

Ninafikiri tukiangalia matokeo ya kila kitu katika maisha yetu katika muono wa mchakato tunaweza tukagundua thamani ya kuwa na nguvu za kusubiri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom