Kwa miaka mingi nimekuwa nikihangaika na mafundi wa Solar systems bila mafanikio .Mpaka sasa nimefikia hatua ya kuamini kwamba hapa nchini hatuna mafundi wabobezi wa Solar Systems kabisa. Yaani wote ni majanga matupu....Nime install solar system mara nyingi lakini zote huwa ni hopeless....Sasa mwaka 2015 nikanunua very expensive na genuine three complete sets za Solar systems toka Japan ...nimeinstall set moja lakini mpaka ninavyozungumza nimeshabadili mafundi zaidi ya watano....system bado haijatulia..yaani nashindwa kuitumia to the fullest.......wakati zipo Solar Panels na power systems za kufa mtu na ni original.... Yaani huyu fundi wa sasa hivi kila mwezi lazima atie timu sababu inakuwa imekorofisha...sasa sijui anafanya makusudi au uwezo wake umefika mwisho.......nimeleta set tatu nataka nizifunge sehemu tofauti lakini mafundi wana nichanganya kabisa.......yaani mpaka sasa naamini hatuna mafundi wabobezi katika taaluma hii..au waliopo ni wahuni wahuni......Kama kuna mtu anaweza kunipa mawazo au ushauri naomba tusaidiane.
Nawasilisha.
Nawasilisha.