Fumanizi la mwalimu, wachomana visu, utumbo nje

Fumanizi la mwalimu, wachomana visu, utumbo nje

ruanganyi

Senior Member
Joined
Aug 19, 2014
Posts
115
Reaction score
34
MUMEACHOMWAVISU.JPG
Mume wa mtu, Raphael Bernard (33) aliyechomana visu na mwalimu baada ya fumanizi.


Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, msala huo ulijiri juzikati nyumbani kwa ticha huyo, Kichangani ambapo mwalimu huyo alidaiwa kufumwa na mume wa mtu, Raphael Bernard (33) ambaye ni dereva wa bodaboda.

KATIKA hali ya kutisha, fumanizi lililoambatana na bonge moja la mtiti linadaiwa kujiri nyumbani kwa mwalimu ‘ticha' wa Shule ya Msingi ya Mafisa ‘A', iliyopo Manispaa ya Morogoro mjini hapa aliyefahamika kwa jina la Rosemary Mkoba kisha watu wakachomana visu.

Habari zilidai kwamba mwenye mume amekuwa akimfuatilia mumewe kwa muda mrefu, akagundua huwa anakwenda kujichimbia kwa ticha huyo huku akiacha familia ikilala njaa.

Ilisemekana kuwa, siku ya tukio, mwenye mume, akiwa na ‘jeshi' lake, alimfuatilia mumewe hadi akamuona akiingia nyumbani kwa hawara wake huyo.

Ikazidi kudaiwa kwamba baada ya kuhakikisha jamaa amelala kwa ticha huyo, mwanamke huyo na ‘skwadi' yake waliondoka, asubuhi iliyofuata mishale ya saa 1:04 wakatia timu na kulianzisha timbwili huku mke huyo akidaiwa kumtishia ticha kuwa akipata ujauzito atazaa kwa mdomo.

P1240513.JPG
Bw. Raphael Bernard akiuguza majeraha hospitalini. Habari zinadai kuwa, baada ya mke huyo na timu yake kuondoka, ticha huyo alimuwakia Raphael kwamba kumbe ana mke, kwa nini hakuwahi kumwambia? Ugomvi mwingine ukazuka hapo.
 
kama sielewi elewi vile...mara mwenye mume mara mwenye mume akamfata mume wake ambaye ni mme wake ni boda boda...aaaaagh!
 
kifupi acha kucheat mihemko si ishu.
 
Yaan hii thread hata haieleweki kabisa........

Hii kiufupi ni kwamba:
huyo jamaa aliye na jeraha hapo juu alimfuma mkewe na jamaa flan ndipo akamdunga kisu mke wake na baada ya kudhan mkewe atakuwa ameshakufa nayeye kaamua kujichoma kisu tumbon ili ajiue lakn wakamuwahi wasamalia na kumpeleka polisi.

Mpaka hapo yupo chini ya ulinzi wa polisi na anapingu kabisa
anashikiliwa kwa kosa la kutaka kuua.
 
kama sielewi elewi vile...mara mwenye mume mara mwenye mume akamfata mume wake ambaye ni mme wake ni boda boda...aaaaagh!

kama mimi yaani sijaelewa .naona wanaolezewa kufumaniwa wote ni jinsia moja yaani me..
 
Hueleweki mkuu, mume na mume na mume tena na ticha ndo nn?
 
Kukurupuka si kuzuri.Una habari motomoto lakini uwasilishwaji wake ni "sifuri" kabisa mkuu.
 
Madhara ya kuwinda ndege shule ya msingi na kuendelea katika secondary ya kayumba madhara yake makubwa.
 
mwenye mume, mume, mwenye mume, ticha, bodaboda, saa moja asubuhi, na timu yake, ticha, aaghh! ili mradi makolokocho tu
 
Story haileweki labda somo ni kwamba michepuko siyo dili
 
View attachment 198148
[FONT=Times
New Roman]Mume wa mtu, Raphael Bernard (33)
aliyechomana visu na mwalimu baada ya
fumanizi.
[/FONT]



Kwa mujibu wa mashuhuda wa
tukio hilo, msala huo ulijiri juzikati nyumbani kwa ticha huyo,
Kichangani ambapo mwalimu huyo alidaiwa kufumwa na mume wa mtu, Raphael
Bernard (33) ambaye ni dereva wa bodaboda.

KATIKA hali ya kutisha, fumanizi lililoambatana na bonge moja la mtiti
linadaiwa kujiri nyumbani kwa mwalimu ‘ticha’ wa Shule ya Msingi ya
Mafisa ‘A’, iliyopo Manispaa ya Morogoro mjini hapa aliyefahamika kwa
jina la Rosemary Mkoba kisha watu wakachomana visu.

Habari zilidai kwamba mwenye mume amekuwa akimfuatilia mumewe kwa muda
mrefu, akagundua huwa anakwenda kujichimbia kwa ticha huyo huku akiacha
familia ikilala njaa.

Ilisemekana kuwa, siku ya tukio, mwenye mume, akiwa na ‘jeshi’ lake,
alimfuatilia mumewe hadi akamuona akiingia nyumbani kwa hawara wake
huyo.

Ikazidi kudaiwa kwamba baada ya
kuhakikisha jamaa amelala kwa ticha huyo, mwanamke huyo na ‘skwadi’
yake waliondoka, asubuhi iliyofuata mishale ya saa 1:04 wakatia timu na
kulianzisha timbwili huku mke huyo akidaiwa kumtishia ticha kuwa akipata
ujauzito atazaa kwa mdomo.

View attachment 198147
Bw.
Raphael Bernard akiuguza majeraha hospitalini. Habari zinadai kuwa,
baada ya mke huyo na timu yake kuondoka, ticha huyo alimuwakia Raphael
kwamba kumbe ana mke, kwa nini hakuwahi kumwambia? Ugomvi mwingine
ukazuka hapo.


michepuko vumbi iyoooo! lo!
 
Yaan hii thread hata haieleweki kabisa........

Hii kiufupi ni kwamba:
huyo jamaa aliye na jeraha hapo juu alimfuma mkewe na jamaa flan ndipo akamdunga kisu mke wake na baada ya kudhan mkewe atakuwa ameshakufa nayeye kaamua kujichoma kisu tumbon ili ajiue lakn wakamuwahi wasamalia na kumpeleka polisi.

Mpaka hapo yupo chini ya ulinzi wa polisi na anapingu kabisa
anashikiliwa kwa kosa la kutaka kuua.

Jitahidi uelewe, ndipo tulipofikishwa watanzania na liccm lenu, mara Div - 5, mara BRN, Mara mkukuta, Mara Mkurabita, mara
........haya ndiyo matokeyo yake. wala tusimpe lawama mleta uzi tuilaumu ccm kwa mfumo mbuvu wa elimu mimi nimemwelewa.
 
to be a good player you must have skills...
sasa bwana hakua na skillz..
 
Waluguru na uandishi wao, mkude njooo, hii habari haisomeki bwanaaa ondoka hapo mataaa uvuke njooo jamiiforum huku
 
Back
Top Bottom