Duh, huyo mwanamke naye mkali asubuhi yote hii, au alilala huko jamani, maana kama saa tatu tukio limetokea, it means around saa mbili alikuwa eneo la tukio already hata hiyo guest house huenda hawajaanza usafi maana wateja wengi unakuta wamelala bado.
Sidhani kama baada ya hapo kuna ndoa tena, na kama ipo sijui kama imani itakuja kurejea baina ya hao wanandoa, na hata yule bwana aliyeachwa aende zake kisa eti hana kosa, sijui kama huko aliko anapumua salama.
Unzinzi ni dhambi, lakini unapoufanya kwa mke wa mtu ama mume wa mtu nadhani ni dhambi maradufu, tutafakari zaidi kabla ya kufanya uamuzi ya kishetani.
Huyo dada kwa jinsi alivyokamatwa, na muda huo, hakika kwa mwanaume yeyote anaipenda ndoa yake kipigo kwa huyo dada hakiepukiki, japo nimeona wengine sijui wanasema TGNP, TAMWA nk, as if hizo taasisi zipo kuwatetea wanzizi ama ndizo zimemtuma kuzini tena asb yote hii. Kwenye ndoa tu muda kama kama hakuna sababu za msingi sana huwezi kuta wanandoa wanafanya mapenzi japo kwao ni halali kabisa na hawana kizuizi cha muda sasa wewe na wizi wako unajihimu kana kwamba ndio kazi yako, hapina wakupige tu wewe.