Full mkanganyiko:huku mh. Jk kule mh. Shein! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Full mkanganyiko:huku mh. Jk kule mh. Shein!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MTENDAHAKI, Jul 21, 2012.

 1. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Kuna vitu lazima tuviseme ili kulitendea haki taifa letu!Kwa sasa nchi yetu in wakati mgumu MNO kiuongozi!Hili lilijidhihirisha juzi baada ya meli ya kuzama na watu wengi kupoteza maisha!Maana baada ya tukio Rais wa Zanzibar Mh. Shein alitangaza siku tatu za maombolezo, na bendera zikaanza mara kupepea nusu mlingoti kule Zanzibar (Bendera zote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Zanzibar) wakati bara mambo yalikuwa bado!Naomba mnisahihishe kama nitakosea lakini mie nasema ni kichekesho pale ilipolazimu na bara napo kutangazwa siku tatu za maombolezo,hivi asingetangaza ingekuwaje kikatiba kwa bendera ya jamhuri ya muungano wa tz!Lakini suala la pili ambalo ninaliona ni mathalani ikatokea janga bara tena shinyanga huko labda,na Rais JK akatangaza maombolezo bendera za Zanzibar itakuwaje, nazo lazima Mh Rais wa Zanzibar DR. Shein atangaze maombolezo?Mie nadhani tukubaliane kimsingi kuwa ikitangazwa na Rais wa Zanzibar kuwa kuna maombolezo na bendera zishushwe nusu mlingoti kusiwe na haja ya mtu mwingine kutangaza bara na kinyume chake ni sahihi!Nadhani kama kweli sie ni ndugu hatuwezi kuwa na janga la upande mmoja huu ni mkanganyiko mkubwa!
  Naomba kuwasilisha
   
 2. b

  busar JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Unit in diversity ndugu. Only negativity
   
 3. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,898
  Likes Received: 2,319
  Trophy Points: 280
  Hebu tujuze ka suala la misiba kama hii ni suala la muumgano na katiba inasemaje.
  Hata hivyo please note the bad blood betn the two sides, currently Wazenj hawapendi waTang sioni jinsi waTang watawachangamkia, hilo ni dhahiri.
   
 4. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #4
  Jul 21, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  kizunguzungu .. kila kitu kizunguzungu.. nadhani haya maswali ni magumu sana na hoja yako watawala hawaipendi sana..sipigilii msumari but ni muendelezo wa hoja chokozi hapo juu kwamba kama Bendera ya JMT imefanywa kato kule Zanzibar je hii ina maanisha nini kwa mamlaka ya ya Rais wa JMT. Je Rais wa SMZ ana sovereign ya Rais wa SMZ inaishia wapi kwenye bahari na Tukija kwenye mzizi wa Tukio, je waliokumbwa na maafa ni Wazanzibari peke yao, (jibu ni kwamba boti lilikuwa na wazanzibari, wabara na watu wa mataifa mengine) sasa kama ni wazanzibari wanaoomboleza hoja ya wa-bara kuwa kimya ina nguvu kiasi gani?

  kwenye Insue ndani ya mipaka ya Zanzaibar, ambazo haziko direct affiliated na JMT, Rais wa SMZ ana power ya kutoa tamko, sasa how kwa insue kama ajali hii..

  ni hoja tu uzalendo bado upo.. Kwanini tuwe wagumu wa kuamini tatizo tulilonalo. KABLA YA KATIBA LAZIMA KWANZA TUUJADILI MUUNGANO..
   
 5. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  WaTanganyika si waZanzibar ila wanZazibar ni waTanganyika.
   
 6. B

  Bob G JF Bronze Member

  #6
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mkanganyiko ktk muungano uko ktk maeneo mengi, Itakuaje zanzibar cuf na ccm wakaunda serikali, na Bara ikashinda CDM?
   
 7. Imam Yussuf Shamsi

  Imam Yussuf Shamsi Member

  #7
  Jul 22, 2012
  Joined: Jun 8, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kimsingi hapa tusitegemee kupatikana katiba mpya, kabla ya suala la muungano kujadilhwa na kuwekwa sawa. Wazanzibari wanajipanga kutangana mgogoro wa kikatiba kuhusu muungano, tusubiri tuone kama Dct Shain ataambiwa ajiuzuli, kama ilivotokea kwa Aboud Jumbe.
   
 8. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Hapa naona kuna too much assuptions؛‎ hivi katiba ya JMT huwa haizungumzii muungano?. But, habe tujiulizee wakati wa majanga yaliyotokea bara- MV bukoba, mabomu etc, smz ili behave vipi?.
   
Loading...