Fuatilia uteuzi wa mawaziri wapya wa Uingereza

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
theresa-may-680x334.jpg



Mawaziri wa Brexit walioteuliwa mpaka sasa wako sita na Waziri Mkuu mpya wa Uingereza katika uongozi mpya baada ya kujitoa EU (Brexit).
  • Chancellor of the Exchequer (finance chief): Philip Hammond
  • Foreign Secretary: Boris Johnson
  • Home Secretary: Amber Rudd
  • Defense Secretary: Michael Fallon
  • Minister for Brexit: David Davis
  • Secretary of State for International Trade : Liam Fox
Kwa Watu hawa muhimu katika Baraza hili jipya mpaka sasa kuna usawa kati ya wale waliokua wakipigania Uingereza kuondoka kwenye Umoja huo (Johnson, Davis and Fox). na wale ambao walipigania kubakia katika Umoja huo (Hammond, Rudd and Fallon).

Leo wanatarajiwa kutangazwa Viongozi wengine watakaokuwa kwenye Baraza hilo litakalo ongozwa na Theresa May, na watachaguliwa kati ya wale wale waliotaka kubaki na waliotaka kutoka Kwenye Umoja wa huo na wanawake watakua wangapi katika ngazi kubwa kwenye Uongozi huu wa Waziri Mkuu wa pili Mwanamke Uingereza.
 
Wanawake wengine wawili wameteuliwa kushika idara za sheria na elimu.

Elizabeth au "Liz" Truss - Sheria
Justine Greening- Elimu

Mama Theresa May anafanya mabadiliko ya wizara na idara mbalimbali kwa kupangua na kuunda idara mpya ikiwemo hiyo ya biashara ya kimataifa itakayosimamiwa na Dr Liam Fox.
 
Bwana Gavin Williamson ameteuliwa kuwa mnadhimu wa bunge au Chief Whip.

Kazi yake ni kuhakikisha wabunge wanahudhuria vikao na wanapiga kura bungeni kupitisha maamuzi mbalimbali.
 
Mpaka sasa mawaziri waliofukuzwa kazi ni kama wafuatao:

George Osborne ambae alikuwa chancellor
Michael Gove ambae alikuwa waziri wa Sheria
Nicky Morgan
John Wittingdale
Oliver Letwin
 
Watapangiwa kazi nyingine. Wasiwe na wasiwasi.

Hawa jamaa ni baadhi ya wale Brexit ambao wangemsumbua mama May kwa misimamo yao mikali.

Kwa vile ni wabunge watakuwa back benchers kwani hawawezi kushika nafasi yoyote kwenye serikali ya mama Theresa May.

Yaani hawa jamaa ambao wanaitwa "miamba" walifukuzwa kazi jana jioni baada ya mama kuapishwa.
 
  • Ikifika zamu ya wakurugezi na ma ded wa wilaya mnshtue na mm nicheki!!
Mimi nasubiria uteuzi wa ma-DAS! Kuna baadhi watafukuzwa wakati wakiapa kwa kuingia kwenye listi kwa bahati mbaya. Vipi jamani Mama ameeleza mikakati yake ya kupambana na watumishi hewa? Madawati vipi? Ametumbua wangapi hadi muda huu?
 
CnUppmvWIAAGMOS.jpg


Waziri mpya wa mambo ya ndani Amber Rudd aliingia wizarani hapo jana usiku na leo mchana alikuwa eneo la Westminster akizungumza na maofisa wa polisi.

Kushoto kwake ni kamishna wa polisi Sir Bernard Hogan Howe na Constable wake PC Bowen na kulia kwake polisi jamii au PCSO Ribeiro.
 
CnUw0EDXgAA3tKF.jpg

Waziri mpya wa mambo ya nje bwana Boris Johnson nae hajachelewa na leo mchana amekutana na wafanyakazi wote wa wizara hiyo.
 
Waziri anaehusika na fedha jina lake linafanana na waziri anaehusika na mambo ya fedha wa Tanzania!
 
Waziri anaehusika na fedha jina lake linafanana na waziri anaehusika na mambo ya fedha wa Tanzania!

Anaifahamu vizuri Afrika kwani amewahi kuishi Malawi akiwa mshauri wa serikali kwenye miaka ya tisini.

Ni mjasirimali mkubwa sana na yeye ni Remainer na anapinga sana uhamiaji wa watu wa kutoka Ulaya Mashariki.

Pia ni rafiki wa karibu wa mama Theresa May na hakusita kabisa kumpa cheo hicho.
 
Waziri wa kazi na mafao bwana Stephen Crabb amejiuzulu.

Ametoa sababu kwamba anajiuzulu kutaka kuwa karibu na familia yake.
 
Mama Andrea Leadsom amepewa wizara ya Mazingira. Huyu mama alitaka kuwania nafasi ya uwaziri mkuu lakini baaae akaamua kumwachia Theresa May.

Mama Priti Patel amepewa wizara ya maendeleo ya kimataifa- hivyo kuna uwezekano akatembelea nchi mbalimbali hadi Tanzania.

Mama huyu alizaliwa jijini London na wazazi wake walihamia Uingereza baada ya utawala wa Idi Amin kuingia madarakani.

Bwana Sajid Javid ambae alikuwa anashughulikia biashara amehamishiwa wizara ya maendeleo ya jamii na serikali za mitaa.

Bwana Damian Green ambae aliwahi kuwa naibu katika wizara ya mambo ya ndani akishughulikia uhamiaji, amehamishiwa wizara ya kazi na mafao.

Bwana Damian Green amesoma chuo kimoja na mama Theresa May chuo kikuu cha Oxford.

Bwana Chris Graying anakuwa waziri wa usafiri.

Bwana James Brokenshire anakuwa waziri wa nchi anaeshughulikia Ireland ya Kaskazini.

Bwana Graig Clark anakuwa waziri wa Biashara.

Bwana Alun Cairns anakuwa waziri wa nchi anaeshughulkia Wales.

Na dada Karen Bradley anakuwa waziri wa utamaduni , habari na michezo.

Karen Bradley na James Brokenshaw wamefanya kazi chini ya mama Theresa May alipokuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi.

Mama Barons Evans anakuwa kiongozi wa bunge la mabwanyenye.

Na mwisho bwana Patrick Macloughlin anakuwa mwenyekiti mpya wa chama cha Conservative.
 
Back
Top Bottom