FT: Yanga S.C 0-0 Rivers United | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa Stadium | 30.04.2023. Yanga yatinga Nusu Fainali

mwarabu feki

JF-Expert Member
Feb 16, 2023
682
1,461
Ni siku ya kipekee siku ya kihistoria katika soka la nchi yetu ambapo tunaweza kushuhudia timu kutoka Tanzania kwa mara ya kwanza ikitinga hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Timu hiyo si nyingine Bali ni Mabingwa wa nchi na vikombe vyote nchini na ambao ndio wawakilishi pekee wa Tanzania na Afrika Mashariki na kati katika michuano ya kimataifa Young Africans almaarufu Yanga.

Leo jioni wanashuka dimbani Estadio de Benjamini Mkapa kumenyana na Rivers United katika hatua ya robo fainali kombe la shirikisho barani Afrika.

Ikumbukwe mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa kule Nigeria, Yanga walipata ushindi wa mabao 2-0, Hivyo wataingia Uwanjani wakiwa na kiu ya kuendeleza ubabe wao mbele ya mapopo na kutinga nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Pia Yanga watakuwa na kiu ya kulipa kisasi cha kufungwa na hawa Rivers nje ndani hivyo watakuwa na kila sababu ya kupata ushindi kwenye ardhi ya nyumbani,

Mchezo huu utapigwa mishale ya saa 1.00 usiku na utarushwa na Azam Sports kupitia channel ya ZBC2

20230430_190439.jpg

Timu zote zimeingia uwanjani kupasha misuli. Uwanja wa Mkapa umetamalaki Wananchi wamejitokeza Kwa wingi kuja kushuhudia historia ikiandikwa katika soka la nchi hii.

Mda wowote kuanzia sasa kipyenga kitapulizwa kuashiria kuanza kwa mpambano huu.

00" Mpira umeanza Rivers ndio wanaanzia mashambulizi kuelekea lango la Yanga

02" Faulo kuelekea lango la Yanga ila unaokolewa..

04" Wananchi wameanza kutandaza soka ice cream

05" Khalid Aucho ameumia na anapatiwa matibabu

11" Clement Mzize anapoteza nafasi ya wazi ya kuweka mpira kambani, alibaki yeye na golikipa tu ila mpira wake ukaenda nje

22" Clement mzizee anapaisha, nafasi nzuri anapoteza ya kuiandikia Yanga goli la uongozi

24" Taa za uwanjani zimezima na Mpira imesimama Kwa muda kusubilia mafundi warekebishe. Ni Giza tupu hapa uwanjani

25" Mpira unaendelea baada ya Taa kuwaka tena..

35" Bado matokeo ni 0-0 japo Yanga wanaliandama sana lango la Rivers United

45+2" Zimeongezwa Dak 2 kufidia muda uliopotea.
Mpira ni mapumziko. Yanga 0-0 Rivers United.

Kipindi cha pili kimeanza

50" Yanga wanashambulia lango la Rivers United kama nyuki

57" Mayeleee anakosa nafasi ya kufunga goli

60" Kichwa cha fiston kinaenda nje

70" Yanga wanaongeza presha ya kutafuta goli

90" Zinaongezwa dakika 3

Full Time
 
Back
Top Bottom