FT: Mbeya Kwanza FC 0-1 Geita Gold FC | NBC Premier League | George Mpole kwenye Kilele cha Ufungaji

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara NBC Premier League imeendelea tena leo Mei 17, 2020 ambapo Mbeya kwanza FC walikuwa wakiwakaribisha Geita Gold FC kwenye Dimba la Maji Maji mkoani Songea.

Mchezo ulikuwa wa mkali na wa kusisimua ambapo hadi dakika 90 zinakamilika, Mbeya kwanza FC wamekubali kipigo cha bao moja kwa bila dhidi ya Wageni Geita Gold FC.

Bao la George Mpole kunako dakika ya 12' | Gooal linamfanya mpaka sasa kufikisha mabao 13 na Assist 3 akimzidi Fiston Mayele mwenye mabao 12, hivyo kuwa kwenye Kilele cha ufungaji wa Ligi Kuu hivyo kuwa kwenye nafasi nzuri ya mbio za kuwania kiatu cha ufungaji bora msimu huu wa 2021/22.
 
Hata msimu uliopita Mugalu na Kagere na Bocco kwenye kuwania kiatu cha ufungaji bora tulipenda achukue Bocco ijapo wote walikuwa Simba SC

George Mpole endelea kukiwasha
 
Wala sishangazwi na hii record pengine ilitakiwa iwe extreme zaidi ya hapa ila kutokana na usimba na uyanga ndio umechangia kupunguza digits za idadi ya magoli yake
 
Wala sishangazwi na hii record pengine ilitakiwa iwe extreme zaidi ya hapa ila kutokana na usimba na uyanga ndio umechangia kupunguza digits za idadi ya magoli yake
Kongole kwake...Mwanzo mwa msimu aliachwa na Mayele na Lusajo kwa mabao 4 lakini amepambana sana mpaka amewafikia na sasa Kinara.

Sipati picha kama angekuwa Simba au Yanga.
 
Kongole kwake...Mwanzo mwa msimu aliachwa na Mayele na Lusajo kwa mabao 4 lakini amepambana sana mpaka amewafikia na sasa Kinara.

Sipati picha kama angekuwa Simba au Yanga.
Simba wafanye mpango msimu ujao aje msimbazi
 
Mkuu bocco ana kazi gani Simba sasa hivi? Tunataka timu ya kuchukua caf cl au cc. Wachezaji waliokwisha choka waachwe sasa. Tunashukuru kwa mchango wao then tunasonga mbele.
Bocco hawezi kuuchwa kirahisi kama unavyodhani, na kama hatacheza msimu unaofuata basi anapewa majukumu mengine ndani ya timu.

Ila akina Kope Mugalu, Meddie Kagere, Pascal Wawa, Bernard Morrison, Taddeo Lwanga, hawana muda ndani ya Simba SC.. Utakuja Kuniambia Mkuu Championship
 
Akibaki kwa majukumu mengine hakuna tatizo ila kubaki kama striker wa Simba ni utani mkubwa.

Hao hapo pia waachwe na kuongezea mzamiru, nyoni, gadiel na onyango.
 
Akibaki kwa majukumu mengine hakuna tatizo ila kubaki kama striker wa Simba ni utani mkubwa.

Hao hapo pia waachwe na kuongezea mzamiru, nyoni, gadiel na onyango.
Onyango huenda asiache katika wachezaji wa Kimataifa..!
 
Hata msimu uliopita Mugalu na Kagere na Bocco kwenye kuwania kiatu cha ufungaji bora tulipenda achukue Bocco ijapo wote walikuwa Simba SC

George Mpole endelea kukiwasha
Maajabu haya! Badala ya kuwapigia chapuo wachezaji wako wa simba kuchukua kiatu cha ufungaji bora! unampigia chapuo George Mpole wa Geita Gold aendelee kukiwasha! 🤔

Bila shaka umeshatambua fika msimu huu mna washambuliaji butu.
 
Pendekezo kwa Simba SC msimu unaofuata..!

Mugalu/ Phiri

Kagere/ Adebayor

Morrison/ gabadinho & Ki

Lwanga/ Zemanga & Dieng

Wawa/ Idumba

Hapa lazima wapinzani wetu wateme Ndoano...!
Itakuwa mimi sio mfuatiliaji sana maana sijawahi kuwaona hao wote, nasikia tu hapa jf phiri na huyo adebayo. Hope watakuwa wazuri.
 
Back
Top Bottom