FT: Ligi Kuu Bara | Simba SC 3-0 Geita Gold | Uwanja wa Benjamin Mkapa | Agosti 17, 2022

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kupigwa leo Agosti 17, 2022, ambapo Mnyama Mkali Mwituni Simba SC, anakiwasha na Geita Gold kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.

Mchezo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90, kwa kila timu kuhitaji ushindi na hasa ukizingatia ndo mchezo wa kwanza kwa timu zote mbili baada ya kufunguliwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023.

Kocha Zaron Maki wa Simba SC amesema kuwa wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo wa kesho (leo) hakutakuwa mchezo rahisi, ni mechi ngumu dhidi ya timu ngumu, licha ya kupata muda mdogo wa kufanya maandalizi dhidi ya Geita, lakini anaamini atafanya vizuri.

Naye Kocha Msaidizi wa Geita Gold Mathias Wandiba amesema kuwa kwa upande wao wamejiandaa vizuri kwasababu wamepata muda wa kutosha kwa kujua wanacheza mechi ngumu dhidi Simba, kwahivyo wapo tayari kwa ajili ya kupata ushindi.

Nani kuibuka na ushindi wa mabao ya kutosha kwenye mtanange huu wa kwanza kwa timu zote mbili Ligi Kuu Tanzania Bara?

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 12: 15 Usiku.. Usikose Ukapata Simulizi

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana


=============

00' Naaam mpira umeanza Uwanja wa Mkapa | Simba SC 0-0 Geita Gold

05' Mashambulizi kwa sasa yameelejezwa zaidi upande wa Geita, lakini hakuna bao.

08' Sakho anakwendaaa kwa kasi na kupiga shuti ambalo limembabatiza beki na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao.

12' Pembeni kule Mpole anapiga shutii lakini mpira unatoka nje na kuwa goal kick.

16' Mpira ni wa kasi huku kila timu ikitafuta nafasi ya kufunga..Banda anashindwa kutumia nafasi.

21' Ni Free Kick kuelekea Simba SC, inapigwa kulee lakini mpira unaokolewa, wanamiliki Simba sasa

Mpole kwenye nafasi, lakini refa anasema ni Offside

25' Henock anafanya Kazi nzuri kuokoa hatari langoni kwake, anapiga chenga na kupiga mbele kuleee.

Geita wanapata Free Kick.. Inapigwa lakini golikipa Manula anaokoa na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao.

Banda anapiga shutii lakini linatoka sentimita chache lango la Geita na kuwa goal kick

Lyanga yupo chini baada ya kupata rabsha, ameinuka mpira unaendelea

Ametoka Mkude na ameingia Okrah upande wa Simba SC.


37' Ni Free Kick kuelekea Geita Gold.. Anakwenda kupiga super sub Okrah

Okrah Goooooooooooooaaal gooal

Kagoma anaonyeshwa KADI ya Njano kwa kumchezea madhambi Kanoute, mpira ni Free Kick kuelekea Geita

45+2' Kuelekea kuwa mapumziko

George Wawa anapiga shutii lakini refa anasema Kabla hajapiga Sakho alimchezea madhambi ni Kadi ya Njano kwa Sakho.

Naaam mpira ni mapumziko ambapo Simba SC wapo mbele kwa bao moja kwa bila dhidi ya Geita Gold

HT: Simba SC 1-0 Geita Gold

Mpira umeanza kipindi cha pili, huku Masai wa Geita akionyeshwa Kadi ya Njano kwa kumchezea madhambi Okrah

Ametoka Jezi namba 10 na ameingia Jezi namba 30 upande wa Geita

Manula anaokoa hatari langoni kwake na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao, Kanoute anapigwa ndefu lakini wanaokoa Geita.

Mpole anakwenda anapiga shutii lakini Mohamed Ouattara anakataa maridadi kabisa

52' Phiri anakwenda mbele, lakini Beki anakataa na kuondoa hatari ile.

Geita wanapambana vizuri sana kutafuta mpenyezo kwa mabeki wa Simba, lakini Mpole na Edimund bado hawajakaa sawa.

61' Phiri Goooooooooooooaaal gooal

Moses Phiri anahesabu bao la pili akipokea pasi murua kutoka kwa Chama

Mpole anaonyeshwa KADI ya Njano kwa mchezo mbaya, huku Geita wakipata Kona ambayo haikuzaa bao

Shamte na Seleman wameingia kuchukua nafasi za Wawa na Edimund upande wa Geita Gold

Simba wanapanga mashabulizi sasa

70' Ametoka Banda na Phiri na wameingia Dejan na Mzamiru upande wa Simba.

Chikola anapiga shutii lakini golikipa Manula anaokoa hatari

Anakwenda. Okraaaaah penalty kuelekea Geita Gold baada ya Okrah kufanyia madhambi

81' Chama Goooooooooooooaaal gooal

Ametoka Mpole na ameingia Chombo Kawa Geita

Ameingia Kibu na Okwa na wametoka Chama na Sakho kwa Simba

Wanakwenda sasa Simba kulee kwake inapigwa Krosi inamfikia Dejan Georgijevic anapiga, anakosa nafasi nzuri ya kufunga

90+3' Kuelekea kumalizika kwa mchezo, Geita wanapata Kona inapigwa kulee lakini mpira unatoka nje.

Okrah anapiga Krosi lakini kichwa cha Kibu kinasgindwa kulenga lango

Kwake Chikola anakwenda mbele kutafuta kusawazisha lakini mpira unaokolewa na mabeki wa Simba

Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao matatu kwa bila dhidi ya Geita Gold.

FT: Simba SC 3-0 Geita Gold

.... Ghazwat...
 
Kocha Zaron Maki ningependa kuona leo anamuanzisha Dejan Georgijevic
20220817_144030.jpg
 
Back
Top Bottom