FT: Ligi Kuu Bara | Geita Gold FC 1-1 Simba SC | Uwanja wa CCM Kirumba | Leo Mei 22, 2022

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Vuguvugu na patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kupigwa leo Mei 22, 2022 ambapo Wajimbaji wa dhahabu Geita Gold FC wanakiwasha dhidi ya Mnyama Mkali Mwituni Simba SC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Ni mchezo wa ushindani mkubwa kwa timu zote mbili, ambapo Geita Gold FC wanapingania kumaliza kwenye nafasi nne za juu kwenye ligi, huku Simba SC wakitaka kupunguza gepu la alama dhidi ya Yanga SC ambao wapo kileleni, hivyo hakuna timu inatamani kudondosha alama tatu.

Kocha msaidizi wa Geita Gold FC Mathias Wandimba amesema kuwa, wachezaji wake wapo vizuri kwa ajili ya kukikabili Kikosi cha Simba SC katika mchezo huo na kuongeza kuwa, vijana hao wa Msimbazi hawampi wasiwasi kwa kuwa Kikosi chake kuna vijana walio bora, wenye vipaji.

Naye Kocha wa Simba SC Pablo Franco amesema kuwa wataingia katika mchezo huo kwa tahadhari kubwa, kwa kuwa wanaenda kukutana na timu nzuri huku akiongeza kuwa, anafikiri ni timu bora zaidi msimu huu ameiona ikicheza vizuri kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza Simba SC waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa..Je leo nani kuibuka na ushindi?

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10:00 Jioni.. Usikose Ukaulizia

Kulitaka Mwana..Kulipewa Mwana

00' Mpira umeanza kwa kasi uwanja wa Kirumba

05' Simba wameanza kwa shuti kali la Sakho ambalo limeokolewa na golikipa na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao.

Geita Gold nao wamejibu Shambulizi ambalo halikuwa na madhara yoyote

10' Geita Gold wamepata Kona tatu na Simba wamepata Kona mbili, mpira ni nzuri kwa timu zote.

Mpole anafanya Jaribio kali sana lango la Simba SC.

Wapo katikati ya Uwanja Simba wakijaribu kutafuta mpenyezo kwa mabeki wa Geita Gold

19' Mpole Goooooooooooooaaal gooal

George Mpole anaipatia Geita Gold bao la kwanza | Geita Gold FC 1-0 Simba SC

Chikola anagongesha mtambaa wa panya, ilikuwa hatari lango la Simba SC.

26' Kapombe amekwenda kwenye benchi na ameingia Jimmyson upande wa simba.

28' Kibu Goooooooooooooaaal gooal

Kibu Denis anasawazishia Simba SC bao kwa kichwa | Geita Gold FC 1-1 Simba SC.

Chikola anaonyeshwa KADI ya Njano

Onyango anakosa nafasi nzuri ya kufunga, nafasi kama hizi Mshambuliaji hakosi, beki ni beki tu

38' Mpira umekuwa nzito, bado mabao ni moja kwa moja, Kanoute anarukaaaa kichwa lakini mpira unatoka nje.

43' Edimund yupo chini baada ya kukumbana na Lwanga, mashambulizi ni kwa zamu sasa.

45+2' Zimeongezwa dakika 2 kukamilisha kuwa mapumziko, Kabumbu limepoa kwa sasa, hakuna kashi kashi.

Mpira ni mapumziko ambapo Geita Gold bao moja na Simba SC bao moja

Geita Gold FC 1-1 Simba SC

Kipindi cha pili kimeanza, kwa kasi kama kipindi cha kwanza..!

Kibu yupo chini akipatiwa matibabu baada ya kupata rabsha.

Anakwenda Sakho, lakini Yondani anakataa maridadi kabisa.. huku Beno akionyeshwa Kadi ya Njano upande wa Simba

61' Mabadiliko kwa upande wa Simba SC, Ametoka Bocco, Gadiel na Lwanga na nafasi zao zimechukuliwa na Kagere, Hussein na Nyoni.

64' Kagoma anaonyeshwa KADI ya Njano kwa kumchezea madhambi Kanoute

65' Mpole anapiga shutii lakini golikipa Beno anadaka bila wasiwasi

Lyanga anaonyeshana umwamba na Kanoute, lakini refa anawatuliza

Kagereeee shutii la mbali sana lakini linatoka nje na kuwa goal kick.

70' Chikola anatoka na anaingia Kadikilo upande wa Geita Gold FC

Geita wanamiliki mpira kwa sasa, lakini mashambulizi yao hayajazaa matunda.

Bwalya anapitisha mpira mrefu kumtafuta Kagere, lakini golikipa anawahi.

75' Kanoute anakwenda kwenye benchi na ameingia Peter Banda upande wa Simba SC,

Edimund anaonyeshwa KADI ya Njano kwa kumchezea madhambi Sakho, inapigwa Counter mbele kuleee..Ni Offside Mpole

80' Kibu anapiga shutii, linambabatiza beki wa Geita, kwake Sakhooo anakosaaaaaa.

Yondani yupo chini baada kupata rabsha, akikumbana na Kagere

85' Ametoka Edimund na ameingia Masota upande wa Geita Gold, Mpole anapiga shutii lakini golikipa Beno anadaka.

88' Sakho anajaribu kufungua ukuta lakini Duchu anacheza mpira na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao

90+3' kuelekea kumalizika kwa mchezo

Kameta Duchu anarukaaaa kule, wanauwahi Simba SC, wanapiga mbele lakini hakuna mtu

Nyoni anaonyeshwa KADI ya Njano

Free Kick inapigwa kuelekea Simba, Mpole anapiga shutii lakini golikipa Beno anadaka.

Unapigwa mbele kuleee Kagere, kwake Sakhooo

Naaam mpira umekwishaaaaaa timu zinagawana alama ambapo Geita Gold FC moja na Simba moja.

FT: Geita Gold FC 1-1 Simba SC

...... Ghazwat...
 
Ugumu wa huu mchezo ni
1. Saikolojia ya mechi ya jumamosi ijayo ambayo simba atacheza na mabingwa Yanga.

2. Vita ya magoli ya George Mpole na Mayele Fiston Toupsant Kalala mutu Ya Kongo

3. Simba wamuachie Mpole ashinde wampe nafasi ya kumpita Mayele halafu Yanga atangaze ubingwa mapema mechi ijayo.

4. Yanga aachelewe kutangaza ubingwa na Mayele awe mfungaji bora.


Kongo siyo kongowe.......
 
Oya Nyie Vigagula Nakodisha Msimamo Unaonesha Mnaongoza Ligi...Maana Hiyo Pumzi Ya Moto Naona Kama Mmejipulizia Wenyewe Msimu Huu
IMG_20220521_143934.jpg
 
Tuna jambo letu tarehe 28 . Hatuna haja na Geita. Tutamwachia mpole afanye yake ili mwandamane kwenda Ikulu kwa mama.
 
Back
Top Bottom