FT: Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup | Simba SC Vs Azam FC | 1- 0 Uwanja wa Maji Maji

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Michuano ya Nusu Fainali ya Kombe Shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC), kukamilika kwa mchezo kupigwa leo Juni 26 2021, ambapo Mnyama Mkali Simba SC anatingishana na Wana lamba lamba Azam FC kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea.

Msimu uliopita katika michuano hii timu hizi zilikutana katika hatua ya robo fainali, ambapo Simba SC waliweza kuibua na ushindi wa mabao mawili kwa bila.

Je Simba SC kuendeleza ubabe kwa Azam FC ama Azam FC kulipa kisasi na kutinga fainali? Dakika 90 za jasho na damu kuamua.

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 9:30 Alasiri. Usikose Ukasimuliwa

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana


============

Naaaam mpira umeanza Uwanja wa Maji Maji.

ASFC.. Simba SC 0-0 Azam FC


05' Mchezo umeanza kwa Kasi huku umiliki ukiwa upande wa Simba wakiwa wamepata Free Kick amabayo haikuzaa bao.

10' Hakuna timu imeona lango la mwenzake, huku Timu zikitafuta mbinu ya kuweza kupenya gome ya mpinzani wake.

15' Daniel Amoah anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa kumchezea faulo Miquissone na Taddeo Lwanga anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa kumchezea faulo Nado

ASFC..Simba SC 0-0 Azam FC

20' Mchezo umepoa kwa sasa huku rafu za hapa na pale kwa pande zote mbili, lakini refa anadhibiti kuhakikisha mchezo unakuwa nzuri.

30' Jaribio nzuri kwa Azam FC kuelekea lango la Simba nusura wapate bao kama si umahiri wa golikipa Manula kupangua na kuwa Kona.

40' Mshako wa kufatuta bao kwa pande zote mbili unaendelea, hapa lazima mtu asonge mbele.

45+2' Kuelekea kuwa mapumziko Uwanja wa Maji Maji.

Naaaam mpira ni mapumziko ambapo hakuna timu imeweza kusalimia lango la mwenzake katika dakika hizi 45

ASFC, HT; Simba SC 0-0 Azam FC

Kipindi cha pili kimeanza huku Simba wakifanya mabadiliko..Ametoka Mzamir na ameingia Kagere.

48' Almanusura Onyango awazawadie bao Azam FC, Abubakar anakosa nafasi ya kufunga.

60' mashambulizi yakiendelea kuelekea upande wa Azam FC kusaka bao, huku Simba wakifanya mabadiliko Ametoka Bwalya na ameingia Morrison.

65' Anakwendaa Chama nafasi kwa Simbaaaaaa njeee.. ASFC Simba SC 0-0 Azam FC.

Mabadiliko upande wa Azam FC, Ametoka Lyanga na ameingia Ismail.

75' Azam FC wanafanya shambulizi bomba, lakini Chirwa anashindwa kutumia nafasi, shuti lake linatoka nje

80' Chamaaa woooool, Namna gani tena Simba wanakosa utulivu eneo la kufunga ilikuwa nafasi ya dhahabu kufunga.

Free Kick kuelekea Azam FC, anaanzisha Morrison kwake Miquissone Goooooooooaaal Goooooooaaal

Luis Miquissone anaipatia Simba SC bao la kwanza | Simba SC 1-0 Azam FC

90+3' Kuelekea kumalizika kwa mchezo ASFC

Naaaam mpira umekwishaaa ambapo Simba SC wanaibuka na ushindi wa bao moja kwa bila na kutinga fainali dhidi ya Azam FC.

ASFC, FT Simba SC 1-0 Azam FC.

..... Ghazwat
 
Simba SC kama kawaida huwa wanapitishwa njia ngumu sana kwenye haya mashindano, lazima wakutane na vigingi vya kweli wavisogeze pembeni ili watinge fainali, natumai na leo hilo halitakuwa tatizo, kazi iliyopo ni kuthibitisha tu Simba ndio babalao Tz.
 
Michuano ya Nusu Fainali ya Kombe Shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC), kukamilika kwa mchezo kupigwa leo Juni 26 2021, ambapo Mnyama Mkali Simba SC anatingishana na Wana lamba lamba Azam FC kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea.

Msimu uliopita katika michuano hii timu hizi zilikutana katika hatua ya robo fainali, ambapo Simba SC waliweza kuibua na ushindi wa mabao 2-0.

Je Simba SC kuendeleza ubabe kwa Azam FC ama Azam FC kulipa kisasi na kutinga fainali? Dakika 90 za jasho na damu kuamua.

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 9:30 Alasiri. Usikose Ukasimuliwa

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
Simba ataendeleza dozi 3-0 , zikipungua basi 2-1
 
giphy.gif
 
Matokeo ya jana yalinifurahisha sana kuona digidigi akielekea kwenye empire ya mnyama bila kuwindwa

Idadi ya goli kwenye mechi hii ni kuanzia 2 na ushee huku miqusion, chama waki ng'aa zaidi
 
Matokeo ya jana yalinifurahisha sana kuona digidigi akielekea kwenye empire ya mnyama bila kuwindwa

Idadi ya goli kwenye mechi hii ni kuanzia 2 na ushee huku miqusion, chama waki ng'aa zaidi
Simba leo anafungwa
 
Simba ataendeleza dozi 3-0 , zikipungua basi 2-1
Mkuu we kaa kilingeni kabisa leo hawa watoto wasije kutuadhiri. Maana uto wameshinda nashangaa hawashangilii ila wakisikia tumedundwa ndo wataanza kushangilia ushindi wao wa jana.
 
Back
Top Bottom