Fruit Salad Special Thread: Jifunze jinsi ya kutengeneza fruit salad za aina mbali mbali

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
Jinsi ya kutengeneza fruit salad ya nanasi, machungwa na maembe

DSCN4543.JPG

Mahitaji

  • 4 vikombe vya mananasi yaliyomenywa na kukatwa vipande vidogo vidogo
  • 2 machungwa yaliyomenywa na kukatwa vipande vidogo vidogo
  • 2 maembe yaliyomenywa na kukatwa vipande vidogo vidogo
  • 2 ndizi zilizomenywa na kukatwa vipande vidogo vidogo
  • Vijiko 2 vya maji ya limao au ndimu
  • Vijiko 2 vya sukari

Jinsi ya kutengeneza

  1. Chukua matunda yote yaliyomenywa na kukatwa katwa na uyachanganye katika bakuli.
  2. Weka maji ya limao au ndimu na sukari kisha endelea kuchanganya.
  3. Baada kuchanganya vizuri, ifunike na uiweke kwenye friji kwa muda wa saa moja.
  4. Baada ya hapo fruit salad yako itakuwa tayari kwa kuliwa.
 
Mkuu hii salad nzuri ila mimi hapo kwenye tui la nazi hapo mhh, ila ntajaribu nione test yake!
 
Mkuu hii salad nzuri ila mimi hapo kwenye tui la nazi hapo mhh, ila ntajaribu nione test yake!

Hata mimi nilidhani ataishia pale kwa limao/ndimu na kuweka kwenye friji kwa lisaa limoja.
Hilo tui la nazi sijui itakuwaje!
 
Kitu Matango yakutosha,Nyanya ziwe Nusu ya kiasi cha Matango,Pilipili ikatiwemo,Nyunyiza na Chumvi inayokuotosha!Lazima ujilambe midomo tu...
 
Mkuu Young Master kuna wataalamu wa lishe wanasem tusichanganye matunda machachu na yasio machachu. Weeewe unalizungumziaje hili?
 
Last edited by a moderator:
Jinsi ya kutengeneza fruit salad ya nanasi, machungwa na maembe

DSCN4543.JPG

Mahitaji

  • 4 vikombe vya mananasi yaliyomenywa na kukatwa vipande vidogo vidogo
  • 2 machungwa yaliyomenywa na kukatwa vipande vidogo vidogo
  • 2 maembe yaliyomenywa na kukatwa vipande vidogo vidogo
  • 2 ndizi zilizomenywa na kukatwa vipande vidogo vidogo
  • Vijiko 2 vya maji ya limao au ndimu
  • Vijiko 2 vya sukari

Jinsi ya kutengeneza

  1. Chukua matunda yote yaliyomenywa na kukatwa katwa na uyachanganye katika bakuli.
  2. Weka maji ya limao au ndimu na sukari kisha endelea kuchanganya.
  3. Baada kuchanganya vizuri, ifunike na uiweke kwenye friji kwa muda wa saa moja.
  4. Baada ya hapo fruit salad yako itakuwa tayari kwa kuliwa.

Mkuu ukiongeza na ice cream ya vanilla juu yake, woooh yummy yummy!
 
Back
Top Bottom