Mbona hakusema ana nyumba pale Wazo Hill nyuma tu ya kiwanda cha sementi?Vilevile, ukiwa mtoto wa mwanasiasa mara nyingi kuna dhana katika jamii yetu kwamba umeishi a privileged life na kwamba umeharibika au umedekezwa na kwamba huwezi kujisimamia mwenyewe. Hii si kweli. Maisha yetu sisi miaka yote yamekuwa ya kawaida sana. Nakumbuka Mzee wangu kwa mara ya kwanza amemiliki nyumba yake si muda mrefu uliopita, na ilikuwa ni nyumba ya makuti pale kijijini Kiomoni, Tanga. Wakati wa mvua, nyumba hii ilikuwa inavuja. Tunahamisha vitanda na furniture. Na wakati tunakaa Kiomoni tulikuwa tunasoma Masiwani, Tanga Mjini ambapo ni Kilomita 12, na tulikuwa tunaenda kwa mguu, ukibahatisha ni baiskeli, na lunch ilikuwa ni mihogo ya kuchoma na maji, mama alikuwa anatupa shilingi hamsini kila asubuhi. Lakini leo kila mtu anadhani maisha yako yote umekula mkate na siagi na umepelekwa shule kwa gari.
Kama haya ni kweli basi ndio maana Makamba anashindwa kukiongoza chama ,kwani hata maisha yake ameshindwa kuyaongoza atawezaje kuongoza chama kizima?
Kama amekuwa mkuu wa Mkoa, amefanya kazi jeshini akashindwa hata kujenga nyumba atawezaje kujenga CCM?
Mshahara wake alikuwa anafanyia kazi gani?
Nini kilikuwa kitu cha msingi kwake?
Ina maana nyumba kwake sio priority?