From General To specific

From General To specific

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
525
Reaction score
2,951
Niliwahi alikwa ITV,katika kipindi cha MEZA HURU ,kuzungumzia Madawa ya kulevya TANZANIA.

siku 3 baada ya kufanya uchunguzi na namna swala hili lilivyokuwa linashamiri hasa maeneo ya Mwananyamala,tandika ,temeke
Nilijisikia faraja baada ya serikali kuingilia kati nakujua sasa suala hili linaenda kutokomezwa.

Ukisoma sheria ya kudhibiti Madawa ya kulevya No.5 ya mwaka 2015,utasikitika na kesi zinazoendelea leo dhidi ya madawa ya kulevya.

Utaamini tuu ,mapambano Yale yalikuwa from GENERAL TO SPECIFIC.

-kifungu cha 11 na 12,kinasema atakaye husika na ulimaji wa bangi ,au ulimaji wa madawa ya kulevya kifungo ni miaka 30,Leo hii tungefurahi kuendelea sikia kesi za waliokamatwa wakilima bhangi katikati ya shamba la mahindi huko hukumu yake imeishia wapi,hakuna hatusikii tunasikia ya Tajiri mmoja tuu.

-ukisoma kifungu cha 15,kinasema watakaoshikwa wakisafirisha na kuingiza madawa ya kulevya ,heroin,bhangi kifungo ni kifungo cha maisha,Leo hii ningejisikia faraja kujua hukumu au mienendo ya kesi ya waliokamatwa na madawa uwanja wa ndege,katika mabasi wakisafirisha kesi zao zinaendeleaji kimya ila twasikia kesi ya Tajiri mmoja tuu.

-kifungu cha 18,kinachosema yeyote anaye tumia,kuvuta(sniff),kujidunga hukumu yake ni miaka 3 au faini ya shilingi mil.1.hakuna waliokamatwa wala kesi zao hazisikiki ,inamaanisha hakuna wanaotumia ,tungesikia hukumu na kesi zao ila tunasikia kesi ya Tajiri mmoja tuu.

Kifungu cha 63,kinatoa nguvu ya mamlaka kuwa na vituo maalumu kwa walioathirika na madawa ya kulevya (sober house).

Hapa sielewi ,kifungu cha 18 kinasema mtumiaji hukumu ni miaka 3 au mil.1 ,kifungu cha 63 kinasema kuwepo kwa vituo maalum kwa kuhifadhi watumiaji na waliothirika na madawa ,aliyeathirika hakutumia?,je yeye hahusiki na kesi ya matumizi?

Wapo waliokamatwa " ready handed" wakiwa wanatumia hawa hatuwasikii ,wapo waliokamatwa kwa kupimwa mkojo not "ready handed" hawa ndio tunawasikia.

Waliokamatwa wanasafirisha na kuingiza mbona hatuwasikii.

FROM GENERAL TO SPECIFIC.

Abdul Nondo.
0659366125

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom