From a Mwananchi perspective............ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

From a Mwananchi perspective............

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by M'Jr, Jun 19, 2012.

 1. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Bunge la Bajeti limeanza wiki moja sasa ambalo ndilo session muhimu kuliko zote katika maendeleo ya taifa letu, kwani ndipo tunapoamua mustakabali wa nchi yetu kwa mwaka mzima unaokuja. Lakini kwa jicho langu kama mwananchi tangu kikao hiki kimeanza ninaona comedy na upuuzi usio na kichwa wala miguu ambao for God's sake nauchukia kuliko maelezo.

  Vijembe na mambo ya kijinga vimejaa, taarabu na mipasho huku watu wakitishiana ngumi limekuwa jambo la kawaida katika kipindi hiki zaidi ya vingine nadhani. Hivi kazi gani tumewatuma wabunge wetu wakafanye? Je hivi ndivyo tumewatuma wakatuwakilishe?

  Nimejiuliza pia kama hiki kinachitwa kiti kinafaa kuwepo pale, nadhani kumekuwa na maamuzi ya kutatanisha na hata yanayoweza kulilinganisha bunge na darasa la chekechea hasa pale linapokuwa chini ya yule mwenyekiti anaitwa Mabumba kama sikosei. Hivi ni kweli hata kuchagua viongozi tu hatuwezi? Yule jamaa hafai hata kuwa mtendaji wa mtaa maana hana sifa yoyote ya kuwa kiongozi wa ngazi yoyote ile.

  what do we have now? Bunge au genge la la wapuuzi kama mashabiki wa Yanga na Simba? Hivi sisi kama wananchi hatuna namna ya kuwafanya hawa wabunge wakajua kwamba sisi kama wananchi ndio tuna mamlaka juu yao?
   
Loading...