Barongo E
Member
- Apr 10, 2014
- 26
- 7
Kumekuwa na taarifa inayozagaa katika mitandao y kijamii hususani Jamii Forums na Tanuru La Fikra juu ya tuhuma kwamba Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa amekuwa akizunguka nchi za Saudi Arabia kuomba misaada ya pesa na magari kwa ajili ya kujiandaa na mbio za kusaka urais ifikapo 2015.
Msingi wa tuhuma hizi ni habari iliyoandikwa na gazeti la Rai mali ya New Habari Cooperation ambayo ni kampuni ya ubia kati ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa awamu ya nne aliyejiuzulu kwa kashfa ya wizi katika sakata la kampuni ya uzalishaji umeme ya Richmond, Mh. Edward Ngoyai Lowassa na aliyekuwa Mbunge wa Igunga na Mweka Hazina wa Ccm ndugu Rostam Abdulrasool Aziz ambaye alijiuzulu kwasababu ya shinikizo la chama tawala kutokana na kashfa za ufisadi zilizokuwa na zinazoendelea kumtafuna hadi sasa ndani na nje ya nchi.
Kwa masikitiko makubwa tumeamua kujibu propaganda hizi kwasababu hazina ukweli wowote ndio maana tumediriki hata kuziita ni propaganda. Sote tunafahamu kuwa Mh. Bernard Kamillius Membe ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi amekuwa ni kiongozi pekee ndani ya Ccm ambaye hadi sasa anaonekana kuw tishio kwa wasaka urais ambao kwa asilimia mia moja mmoja wao ndio mbia katika umiliki wa gazeti la Rai, kwa nguvu na kauli moja tunaomba jamii itambue kuwa hizi sio habari za ukweli bali ni hatua ya mafisadi kumchafua ili aonekane hafai katika jamii ya Tanzania.
Tuhuma hizi zimejaa lugha ya picha isiyo na ushahidi wa kuridhisha,lugha hii ya picha tunayoimaanisha hapa ni ile ambayo imeegemea katika ushahidi wa kusikia ambao hata mahakamani haukubaliki. Tuna mashaka na waandishi wa kampuni hii ya New Habari Cooperation, maana sio mara yao ya kwanza kuandika habari isiyo na ushahidi na hatimaye wanaishia kufikishwa mahakamani na kulipa fidia ya mamilioni ya pesa. Kama mtakumbuka hata mwaka 2011 gazeti la Mtanzania ambalo pia ni mali yao liliwahi kumchafua Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania na Diwani wa Kata ya Hananasif manispaa ya Kinondoni kuwa amefisadi 500m ya ujenzi wa shule ya Hananasif ila mwisho wa siku ile habari haikuwa ya kweli na mhusika akaamua kuwafungulia mashitaka mahakama kuu na sasa wanahaha kumaliza sakata hili nje ya mahakama.
Pia, jamii ikae ikifahamu kuwa Mh.Membe hajawahi na hatowahi kuomba msaada wa aina yoyote ile nje ya nchi ili kusaidia kampeni zake za kusaka urais kwasababu hakuna mahali amewahi kutamka kuwa anataka urais na ndio maana bado anasisitiza kuwa hajaoteshwa. Hao wanaotamka kuwa anazunguka kusaka hela na magari ya kampeni watueleze ni lini na wapi na muda gani wana ushahidi wa Mh. Membe akiwatamkia kuwa anasaka urais wa nchi hii. Siasa za maji taka hizi ambazo hazina tena nguvu.
Gazeti la Rai na mtoa habari katika Jamii Forums wanasema kuwa Mh. Membe amepewa onyo na Kamati ya Maadili kuwa asishiriki uchaguzi wa aina yoyote ndani ya Ccm kwa miezi 12 ila hawataji kama kweli Kamati ya Maadili iliwapa barua za onyo na hawataji waliotajwa kuhusika na rushwa katika kampeni ambazo sio stahili kwa muda huu.Ukweli upo hivi; Kamati ya Maadili haijatoa barua kumtia Mh. Membe hatiani ndio maana hajakata rufaa mahali na kukaa kwake kimya ni kuheshimu maamuzi ya CCM kwani kwa Mcha Mungu kama yeye anaamini kuwa ipo siku ukweli utajulikana. Ila pia ukweli ambao haujawekwa hadharani na sasa sisi tumeona tuuweke hadharani ni kwamba waliokutwa na hatia katika Kamati ya Maadili ni watu wanne tu nao ni Mh. Edward Ngoyai Lowassa, Mh.William Mganga Ngeleja, Mh. January Yusuph Makamba na Mh.Stephen Masatu Wassira. Hawa wamepatikana na hatia kwa kugawa pesa taslimu na simu za mikononi kwa baadhi ya wajumbe na wanachama wa Ccm.
Wito wetu kwa New Habari Cooperation ni kwamba wasitake kutajirisha watu kihalali kwa kutoa habari za kuchafua watu zisizo na ushahidi mbele ya macho ya sheria kwasababu madhara yake ni makubwa sana katika safari yao ya kibiashara na hata kisiasa pia kwa huyo wanayemtumikia kwasababu hawamsaidii bali wanazidi kumharibia.Waache kujadili watu na sasa wajadili issues.Jamii ya Tanzania haiko tayari kusikiliza uzushi, inahitaji kusikia masuala yahusuyo maslahi