Uchaguzi 2020 Freeman Mbowe usiwanyime wengine Ubunge kisa wewe hujashinda

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,388
2,000
Kuna taarifa zinasambaa kuwa CHADEMA hakitachagua wabunge wa viti maalumu kwenye uchaguzi huu huku wakijua kabisa kuwa ipo kisheria.

Kutochaguliwa wabunge waliokuwa wabunge miaka 10 kutoka CHADEMA katika uchaguzi huu akiwepo Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe isiwe ndio kigezo cha kuwaminya wengine wasiingie Bungeni.

Mbona mlipochaguliwa hakuna aliyelalamika kuwa Lowassa ameibiwa hivyo mkasusa kwenda Bungeni mwaka 2015.

Waachieni na wengine wakafanye kazi za ubunge pia mbona Trump kafungasha mizigo huko White House wewe Mbowe ni Nani?
 

PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
13,355
2,000
CDM waache ubinafsi na ubaguzi kwa wanawake walioshinda viti maalumu, mbona wao walishinda dhidi ya tume hii hii na wakaenda bungeni?
Jiteue wewe uende.

Watu wamechomwa moto, wamebakwa, wameuliwa, wamepigwa mabomu, wamepigwa risasi na wengine wako magerezani mpaka sasa kwa maelfu halafu unataka wakashirikiane na hao wauaji?

Kama unaona ni sahihi jiteue wewe uende.

Si mlitaka bunge la chama kimoja hii kulilia Chadema ya nini sasa?

Msituchoshe.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
37,502
2,000
Wa Nkasi amesema atakwenda Bungeni kuapishwa ili awatumikie wananchi waliomchagua Sasa hapo Mbowe hataki ....dada nenda Bungeni kawawakilishe waliokuchagua

Huyo wa Nkasi aende, maana inaonekana amejali zaidi ushindi wake kuliko hujuma za wazi zilizofanywa. Cdm kwenda kushiriki hilo bunge ni kubariki umwagaji damu uliofanywa na vyombo vya dola, wizi na ukiukwaji wa haki za wananchi. Cdm isijikite kwenye faida za muda mfupi, bali ijali mustakabali wa demokrasia ya nchi hii. Bunge lenyewe halina jipya bali ni rubber stamp ya serikali.
 

cariha

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
14,138
2,000
Jiteue wewe uende.
Watu wamechomwa moto, wamebakwa, wameuliwa, wamepigwa mabomu, wamepigwa risasi na wengine wako magerezani mpaka sasa kwa maelfu halafu unataka wakashirikiane na hao wauaji ?

Kama unaona ni sahihi jiteue wewe uende.

Si mlitaka bunge la chama kimoja hii kulilia chadema ya nini sasa ?

Msituchoshe.
Kwani kipindi kina mnyika wanaenda bungeni watu hawakufa mfano Yale maandamano ya Arusha. Kwangu mimi acheni ubinafsi, hafu Mimi siko chama chochote ni raia wa kawaida nisiye na mihemkoa.
 

PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
13,355
2,000
Kwani kipindi kina mnyika wanaenda bungeni watu hawakufa mfano Yale maandamano ya Arusha. Kwangu mimi acheni ubinafsi, hafu Mimi siko chama chochote ni raia wa kawaida nisiye na mihemkoa.
Kwani yale mauaji yalifanyika kwenye uchaguzi?
 

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,388
2,000
Kwani kipindi kina mnyika wanaenda bungeni watu hawakufa mfano Yale maandamano ya Arusha. Kwangu mimi acheni ubinafsi, hafu Mimi siko chama chochote ni raia wa kawaida nisiye na mihemkoa
Nakumbuka Sana uchaguzi wa marudio wa madiwani pale uwanja wa Soweto lilipolipuka bomu na kuuwa watu kadhaa na hata yale maandamano kule Arusha pia watu walikufa na wao wakina Mbowe na Lema walikwenda kula kiapo Cha ubunge Dodoma Sasa kwanini wanataka Kenani asiende Dodoma kuapa Bungeni, wamuache dada wa watu naye akafanye kazi aliyotumwa na wananchi wake.
 

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,388
2,000
Unyama, ukatili, ushenzi na uhayawani wa wazi uchaguzi huu, nitawadharau sana cdm iwapo watabariki upuuzi huo kwa kwenda bungeni. Wakati wa Lowasa hakukuwa na ushenzi wa wazi hivi.
Lazima watakwenda bungeni
 

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,388
2,000
Huyo wa Nkasi aende, maana inaonekana amejali zaidi ushindi wake kuliko hujuma za wazi zilizofanywa. Cdm kwenda kushiriki hilo bunge ni kubariki umwagaji damu uliofanywa na vyombo vya dola, wizi na ukiukwaji wa haki za wananchi. Cdm isijikite kwenye faida za muda mfupi, bali ijali mustakabali wa demokrasia ya nchi hii. Bunge lenyewe halina jipya bali ni rubber stamp ya serikali.
Hakuna wizi wa kura Chadema hamkwenda kupiga kura mlibaki mqjumbani na ndiyo 14 million Ssasa mnalalamika nini.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
37,502
2,000
Hakuna wizi wa kura Chadema hamkwenda kupiga kura mlibaki mqjumbani na ndiyo 14 million Sasa mnalalamika nini

Hivi unadhani hatukuona kilichofanyika kwenye uchaguzi huu? Je, wale wabunge 28 na madiwani kibao wa CCM kupatikana kabla ya uchaguzi, nayo ilikuwa ni matakwa ya wananchi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom