Freeman Mbowe Shujaa wa Demokrasia

Freeman Mbowe Shujaa wa Demokrasia

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,265
Reaction score
4,452
Natumaini wote mtamaliza mwaka salama pamoja na wengine wetu kuanza kuharibiwa kipindi hiki na watu wasiojulikana.

Tanzania ina mashujaa wengi sana ambao ama wamepoteza maisha au kuumia katika harakati za kuleta mabadiliko katika taifa.
Kuna shujaa mmoja ambaye nafikiri ni busara kabla ya mwaka kuisha tutambue nafasi yake adhimu katika ujenzi wa demokrasia hapa Tanzania

Hapa namzungumzia Mh.Freeman Aikael Mbowe.Mwanamapinduzi halisi muwazi asiyekuwa na chuki wala unafiki.Kijana mwenye mawazo endelevu na anayeonyesha kuwa na fikra mbadala ya kupeleka taifa letu mbele.Ni mtu ambaye pamoja na vitisho vingi,manyanyaso mengi,na fedheha nyingi bado amekuwa ni mtu mwenye msimamo na mtazamo wa kipekee.

Freeman Mbowe ndio mwanasiasa pekee ambaye pamoja na ukweli kwamba alitofautiana kimtazamo na mzee Edward Lowasa lakini imani aliyokuwa nao juu ya uwezo hekima ya Mzee Lowasa ulimfanya akubali kusimama mbele ya Watanzania na kusema pamoja na yote huyu ndie anayefaa kuiongoza Tanzania.

Kwa msimamo ule alituonyesha kuwa yeye sio mtu wa visasi na chuki na kwamba anaamini atika uwezo wa mtu na kwamba anaweza kumpa yeyote fursa.

Freeman Mbowe amewapa fursa vijana wengi ndani ya Chadema.Ni katika uongozi wake uliotukuka tumeona vijana machachari na wenye uwezo wa kujenga hoja wakiibuka katika medani za siasa tena bila kujikomba bali ni kwa kuonyesha uwezo wao thabiti.

Freeman Mbowe amekifadhili chama chake kwa kujitoa kwa pekee na kuhatarisha usalama wake na wa familia yake na mali zake lakini bado hakukata tamaa kutokana na imani yake kwamba tanzania bora itajengwa na wenye moyo

Freeman Mbowe anawasilisha mawazo na fikra za wana mageuzi,vijana wa kisasa wenye imani kuwa Tunaweza kuwa taifa la kipekee katika bara la Afrika

Kwa kusema haya napenda nimtakie mwaka mpya mwema ndugu Mbowe na kumwambia kuwa asife moyo wakati wa ushindi u karibu na Mungu yuko upande wake

Aluta Continua

Wasalaam

PBK
 
Tukiachana na madhaifu ambayo kila mwanadamu anayo ila Freeman Mbowe ni mmoja ya viongozi muhim sana wa upinzani katika historia ya vyama vingi vyama vingine huwa vikipata migogoro ya uongozi au hujuma za chama tawala vinakufa ila CHADEMA imevuka milima na mabonde mengi ikiwemo migogoro ya uongozi na propaganda za kila aina ila imefika kuwa chama kikuu cha upinzani na tishio kwa ccm kwa hayo tu Long live Freeman Mbowe
 
Namkubali mbowe sana, hata jpm anamkubali ndo maana yuko tayari kwa dau lolote kwa atakaechomoka mikononi mwa haikaeli
 
Mchaga alime kwenye Greenhouse ili afadhili watu kupanua vidole pasipo faida yoyote? Mmerogwa?

Vijana pekee wanaopewa nafasi kubwa na Mbowe ni wale matutusa ikitokea mwelevu akapewa kwa zali la benefit of doubt basi atatengenezewa zali afukuzwe/apotezwe atakapoanza kuhoji.

Mbowe Ni chongo kwenye kundi la vipofu.
 
Mbowe ni jabali na anaweza akasema lolote na watu wakamsikiza
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mchaga alime kwenye Greenhouse ili afadhili watu kupanua vidole pasipo faida yoyote? Mmerogwa?

Vijana pekee wanaopewa nafasi kubwa na Mbowe ni wale matutusa ikitokea mwelevu akapewa kwa zali la benefit of doubt basi atatengenezewa zali afukuzwe/apotezwe atakapoanza kuhoji.

Mbowe Ni chongo kwenye kundi la vipofu.
Kitumvua cha...mam
... Ako wewe jamaa bana
 
Tukiachana na madhaifu ambayo kila mwanadamu anayo ila Freeman Mbowe ni mmoja ya viongozi muhim sana wa upinzani katika historia ya vyama vingi vyama vingine huwa vikipata migogoro ya uongozi au hujuma za chama tawala vinakufa ila CHADEMA imevuka milima na mabonde mengi ikiwemo migogoro ya uongozi na propaganda za kila aina ila imefika kuwa chama kikuu cha upinzani na tishio kwa ccm kwa hayo tu Long live Freeman Mbowe

Ninauhakika Chadema itakuwa na nguvu kubwa huko mbele ya safari
 
upload_2017-12-31_17-3-37.png
 
Tukiachana na madhaifu ambayo kila mwanadamu anayo ila Freeman Mbowe ni mmoja ya viongozi muhim sana wa upinzani katika historia ya vyama vingi vyama vingine huwa vikipata migogoro ya uongozi au hujuma za chama tawala vinakufa ila CHADEMA imevuka milima na mabonde mengi ikiwemo migogoro ya uongozi na propaganda za kila aina ila imefika kuwa chama kikuu cha upinzani na tishio kwa ccm kwa hayo tu Long live Freeman Mbowe
mbona umemsahau Dr Slaa ?
 
Freeman Mbowe amewapa fursa vijana wengi ndani ya Chadema
Ni kweli. Wengine wamekuwa Lulu wa upande wa pili na wamepta shavu huko, Shonza, Mwampamba, Kitila, Msando. Wapo wengi pia akina Zitto, Mwigamba, Kafulila, Mkosamali nadhani ni zao lake mbowe. Marehemu Mawazo angekuwa fit sana katika siasa hapa Tz. Binafsi alikuwa ananivutia sana Mawazo hata kama sio mwana CDM.
 
mbona umemsahau Dr Slaa ?
Yeah Dr slaa pia ni mpambanaji sana ingawa ndio hivyo mwisho alikuja kusaliti mabadiliko ila Kamanda Mbowe aliendelea kuwa mwaminifu kwa chama na kikavuka uchaguzi salama bila mpasuko ambao ulitabiriwa kwa zitto na slaa kuhama chadema !!!! Na hta tishio baada ya lipumba kujitoa CUF na NCCR kumeguka kuelekea uchaguzi 2015!!! Ila chadema pekee hta baada ya kuondoka slaa ndio imeendelea kuwa imara maana CUF inakufa tayari huku bara

Kwa hilo mbowe namkubali sana
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom