Kama habari za kustaafu za bwana Mbowe ni za kweli basi zitakuwa habari njema kwa wale wote wanaoitakia mema CHADEMA.CHADEMA pale ilipo inahitaji mabadiliko makubwa sana, mabadiliko kuanzia kwenye image ya nje ya chama.CHADEMA inahitaji Mwenyekiti mpya ambaye akiingia tu jambo la kwanza ni kuhakikisha chama kinajenga makao makuu yake mapya,tena ya kisasa na ya kupigiwa mfano ambayo ita_accommodate offices za jumuiya mbalimbali za chama kama vile BAVICHA,BAWACHA,BARAZA LA WAZEE,nk.Ikiwezekana pia office ya media house ya chama iwemo humo humo kwa mfano TV na radio. Mwenyekiti mpya anapaswa kufanya mabadiliko makubwa ya kimfumo,hasa kuweka sawa baadhi ya vipengele vilivyomo kwenye katiba,vingi vina mapungufu mengi sana vinavyopelekea baadhi ya viongozi ku_abuse katiba kwa maslahi yao.Ifike wakati katiba izipe meno mamlaka za kimaamuzi kama baraza kuu la chama,kamati kuu ya chama na mkutano mkuu wa chama kuwadhibiti viongozi wabadhilifu na wanaotumia madaraka yao vibaya.Lazima CHADEMA ianze kujenga misingi imara itakayosaidia kuwapata viongozi safi na wenye uwezo mkubwa, tena watakaopatikana ktk mazingira ya haki na ya kidemokrasia.CHADEMA haiwezi kwenda mbele kwa kumng'ang'ania mtu mmoja tu,hiyo tu peke yake inaonyesha jinsi chama kilivyo dhaifu mno kama taasisi.Chama kinahitaji mawazo mapya,fikra mpya,mwonekano mpya,muundo na mfumo mpya ili kisonge mbele.