Freeman Mbowe Mgeni Rasmi wa Siku ya Wanawake BAWACHA Dodoma

Freeman Mbowe Mgeni Rasmi wa Siku ya Wanawake BAWACHA Dodoma

UWT walipo humu wanatakiwa kuiga hili jambo
Mwanaume kuhutubia wanawake siku ya wanawake hilo haliwezekani kuna shida

Mfano ulaya sasa hivi wameruhudu ndoa za jinsia moja.Sasa kuna umoja wa wake za mawaziri wakuu wa nchi za ulaya.Wanaume walioolewa na wanaume wenzao Ulaya wanahesabika wanawake.Hivyo huhudhuria mikutano yote ya wanawake wake wa mawaziri wakuu kama wanawake

Nauliza tena Mbowe ni mwanamke kuhudhuria huo mkutano wa wanawake? Pengine kuna siri watanzania hatuijui kumhusu vizuri .Picha hiyo ikienda Ulaya wenyewe wanamwelewa vizuri kuwa ilikuwa sawa yeye kuhudhuria tena kama mgeni rasmi
 
Mwanaume kuhutubia wanawake siku ya wanawake hilo haliwezekani kuna shida

Mfano ulaya sasa hivi wameruhudu ndoa za jinsia moja.Sasa kuna umoja wa wake za mawaziri wakuu wa nchi za ulaya.Wanaume walioolewa na wanaume wenzao Ulaya wanahesabika wanawake.Hivyo huhudhuria mikutano yote ya wanawake wake wa mawaziri wakuu kama wanawake

Nauliza tena Mbowe ni mwanamke kuhudhuria huo mkutano wa wanawake? Pengine kuna siri watanzania hatuijui kumhusu vizuri .Picha hiyo ikienda Ulaya wenyewe wanamwelewa vizuri kuwa ilikuwa sawa yeye kuhudhuria tena kama mgeni rasmi
Tuanze na wewe, bashee yupo naye kwenye maazimisho yenu?
 
Anaenda kichagua wa kumtembezea rungu hapo baada ya J Mukya kuchuja
 
Relax mkuu,mbona unaweweseka sana, mara CDM ni mfu, mara sio tishio ,mara chama cha kikanda, sasa wasiwasi wote huo wa nini ?,mnakosa usingizi na ndio kwanza CDM plane inajiandaa kuruka,pilot atakapo weka full throttle ready for take off, Lumumba street mtasambaratika,why Singida kuna umasikini wa ajabu, alisikika mpangaji mkuu wa magogoni aliuliza hili swali!!
Kwa hizi porojo sasa naa wewe unaona umejibu swali langu?
 
Mkutano ilitakiwa uhutubiwe na mgeni Rasmi mwanamke kutoka ndani ya Bawacha au taasisi yoyote ile au mwanamke yeyote yule mwenye ushawishi katika jamii, ili atoe muelekeo sahihi na ujumbe kwa wanawake wenzake wa CHADEMA katika masuala mbalimbali yanayogusa wanawake.ikiwepo kuwapa hamasa ya wao kushiriki katika chaguzi zijazo kwa kugombea na kuwaunga mkono wanawake wenzao waliogombea,kujadili masuala ya uchumi na ujasiriamali na namna ya kuinuana, kujadili masuala ya malezi kwa watoto,kujadili masuala ya nafasi ya mwanamke katika mabadiliko ya namna yoyote ile katika jamii na umuhimu wa mwanamke na nguvu ya ushawishi aliyo nayo.

Haya yangezungumzwa na mgeni rasmi ambaye ni mwanamke na siyo Mbowe. kumpa ugeni rasmi mbowe ni kuwadharau Bawacha kuonekana hakuna mtu mwenye uwezo wa kuongoza shughuli hiyo na mwenye kutoa ujumbe wa kugusa wanawake na kuwaleta pamoja ndani ya CHADEMA.ni kuwadogesha na kuonekana jumuiya haipo imara na haiwezi kusimama yenyewe na ikajizungumzia mambo yake yenyewe.

Pia ni kuonyesha kuwa CHADEMA bado haijawa taasisi imara kwa kuwa kila kitu ili kionekane kitakwenda sawa na kukamilika basi ni lazima kuongozwa na kusimamiwa na mbowe mwenyewe.sasa mbowe mpaka lini? Jumuiya zitakuwa na nguvu yake lini? Mnawaandaa vipi viongozi wa kesho kama mnashindwa kuwaamini viongozi wake kuweza kuongoza na kusimamia shughuli yake? Mtawajengea kujiamini katika matukio yapi sasa? Mimi nafikiri matukio makubwa kama haya ndio mngewapa hao wanawake wenu wa Bwacha fursa ya kuendesha na kusimamia matukio hayo makubwa wenyewe,ili kuwaongezea kujiamini,kupata uzoefu,kujijenga na kuijenga jumuiya pamoja na kuvuta hisia za watu nje ya jumuiya kuliko kumtegemea mbowe kwa kila kitu hata ambavyo kwa wenye akili unaona kuwa hapa hakustahili kuwa yeye.

Shida ya CHADEMA ni ile hali ya kutokujiamini na kujipendekeza kuliko pita kiasi.kila mtu anamuagalia Mbowe.hali hii inakidhoofisha Chama na kutokukikuza wala kukiimarisha maana mawazo yanakuwa ni yale yale kutoka kwa mtu yule yule wa miaka yote.kwanl hiyo kunakuwa hakuna radhi mpya kwa masikio ya wasikilizaji.
Screenshot_2024-03-08-19-54-03-1.png
 
Inashabgaza saba mwanaume kuwa mgeni rasmi siku ya wanawake kulikoni? Kwani Mbowe ni mwanamke? Au yale mambo ya ulaya yameshaingia Tanzania. Kupitia Chadema?
Usilie , Mambo bado
 
CHADEMA nayo imehamia DODOMA au mimi ndiye sielewi? Nimezoea kusikia shughuli za CCM kufanyika Dodoma kwa sababu walihamishia makao makuu kule, hivi vyama vingine sikufahamu navyo vimehamia au bado.
 
Back
Top Bottom