Freeman Mbowe: Hatukupeleka mabondia bungeni

Msengapavi

JF-Expert Member
Oct 23, 2008
8,507
2,000
Juliana ni mchepuko wake ndiyo maana kaamua kuwakomoa wabunge wa chadema cha kufanya ni wabunge wa chadema wamsake mke wa Spika na binti zake wachepuke nao ili apate kujifunza aache Udikteta wake.
Sentensi umeianza vizuri na kumaliza vibaya. Siku zote ubaya unashindwa kwa wema ingawaje kwa hali iliyoko bungeni unatamani mabaya yawapate maccm. Anyway, tuwaombee maisha marefu wayaone mafanikio ya upinzani na uangamivu wa udhalimu wao.
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
10,939
2,000
Mwanaume mtu mzima kushadadia ''umbea na mipasho'' ya wanawake si dalili njema. Juliana Shonza na wale akina mama huenda walikuwa wanapashana kama ilivyo kawaida yao lakini kitendo cha Speaker kulivalia njuga suala la wamama ni umama.
 

NnyaMbwate

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
1,679
2,000
Wakati mwingine kama mtu ungekuwa na uwezo, unatamani uroge baadhi ya watu flani flani hivi. Najaribu kuwaza kimoyomoyo!!!
 

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
5,178
2,000
Kuna kampeni zinafanywa zenye high level of impartiallity kuonyesha wananchi kuwa wapinzani ni wahuni na matahayira. Ni kampeni ambazo zinataka kuwaaminisha watu kuwa CCM na wabunge wao ni waadilifu na Malaika ndio maana husikii wakipewa adhabu
 

Maserati

JF-Expert Member
Jun 15, 2014
11,604
2,000
Ccm wase. Nge kama wase. Nge wengine tu. Mbona yeye ndugai akipiga mtu mpaka akapoteza fahamu au yeye yupo juu ya sheria???
Kmanyoko
 

Maserati

JF-Expert Member
Jun 15, 2014
11,604
2,000
Wakati mwingine kama mtu ungekuwa na uwezo, unatamani uroge baadhi ya watu flani flani hivi. Najaribu kuwaza kimoyomoyo!!!
Mi nawaza zaidi yako mpaka naogopa kuandika humu aisee.
Bang bang bang.... Booooom!!!
 

mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,544
2,000
Kweli sasa wabunge wa chama flan mmeamua kututukana sote watz. Hivi tuliwatuma kwenda tafutana na kugombana huko bungeni au kuyajadili maisha mema ya watz??
Ugomvi wako weye Juliana na hao wapinzani una uhusiano gani na taifa hili?? Hebu jamani tujitahidi kuwaza kabla. Hebu tuelezewe, ni nini taifa litapata hata kwa kuwafunga hao wabunge wote 8 bila faini miaka 4??
I wishi I kuldu be a Spika. Ningelifuta nafwasi zoote za upinzani hadharani nikaombe kwa Lubuva kuwa hatuna wabunge hao na majimbo yapo wazi kabisa tuchague upyaaaaa. Huenda wananchi mnaowaamini hivyo wakawachagua hao mnaowataka. Hata kwa goli la mkono amani iwepo tu.
Tumefika mahali pa kuchafuana hadi kukamata wenyeviti wa Kanseli. Tumefika mahali pa kubomoa majumba ya watu, tumefika mahali pa kung'oa mimea iliyokuwa karibu na kuiva bila huruma. Mnataka nini basi viongozi wetu???
Ndo maana hata hao vichaa wa Kibiti wanaua watu wasio na hatia yeyote bila hata kusema wanataka nini tuwape?? Naomba tufike mahali watz tuseme; Sasa baasi, hatuwi wajinga zaidi. Tumuone kila mtu ni ndugu kama zamani. Mwl huko uliko mbona wanasemaga kuwa mizimu hurudi kuwachapa watu. Wa kwako mwl umefungiwa wapi?? Mbona kanisa lako ulilolipenda wanataka kukutangaza Mtakatifu Julias??? Yewoooooomi.
Natanguliza samahani kwa yeyote niliye mkwaza kwa mawazo yangu potofu.
 

mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,544
2,000
Ccm wase. Nge kama wase. Nge wengine tu. Mbona yeye ndugai akipiga mtu mpaka akapoteza fahamu au yeye yupo juu ya sheria???
Kmanyoko

We ni mwanamke au?? Jamani, maadili yetu yamekwenda wapi?? Mzaha mzaha utamtukana mumeo hivi hivi, mkipigwa mkimbilie polisi ka Juliana
 

Mgibeon

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
10,208
2,000
Kuna shida moja kwenye sheria, hii kesi itaisha kwa hawa wabunge wa CDM kushinda, kinachofanyika ni kupotezeana muda na focus kwenye mambo ya msingi, sasa ili kuwafanya CCM wasitumie hii mbinu chafu ya kupelekana mahakamani hata kwa makosa ya kuunguza mboga na kuzidisha chumvi kwenye chakula, KESI ZOOOOOOTE WAPINZANI WANAZOSHINDA IDAIWE FIDIA KUBWA SAAAANA, hili litafanya tuheshimiane..

Ningekua mods ningemfuta kabisa huyu binti humu JF.
 

Maserati

JF-Expert Member
Jun 15, 2014
11,604
2,000
We ni mwanamke au?? Jamani, maadili yetu yamekwenda wapi?? Mzaha mzaha utamtukana mumeo hivi hivi, mkipigwa mkimbilie polisi ka Juliana
Una sajili jinsia??
Maadili my Ass.
Umejuaje kama namtukana mume wangu? Kama inakuuma njoo akuoe mke wa pili umfute machungu.
Endelea ku wish uwe spika uufute upinzani but fanya hayo ukiwa umeibadilisha isiwe nchi ya demokrasia .
Shubamit
 

MTENDAHAKI

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
4,014
2,000
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mh. Freeman Mbowe amelaani kitendo cha wabunge 8 wa upinzani kukamatwa na jeshi la polisi kwa madai yakutaka kumpiga mbunge wa CCM Juliana Shonza, na kusema hawajapeleka mabondia bungeni.

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mh. Freeman Mbowe
Freeman Mbowe amesema hayo leo mjini Dodoma baada ya kutoka mahakamani na kudai kuwa wao wanaamini kuwa mahakama itatenda haki kwa wabunge hao.

"Kama ambavyo mnajua kwa masaa zaidi ya 48 wabunge wa CHADEMA wameshinda polisi, jana siku nzima wameshinda polisi na leo wameshinda polisi mpaka mchana huu, kwa maana hiyo wawakilishi hawa wa wananchi wameshindwa kuwajibika kwa ajili ya wananchi kwa makosa ambayo kimsingi kabisa hayakutakiwa kupewa uzito huu yanaopewa, inasemakana kuwa wabunge hawa walimfanyia fujo Mbunge wa viti maalum (CCM) Juliana Shonza jambo hili linafedhehesha sana, sisi tuna wabunge ambao wanajiheshimu na kuheshimu sheria za nchi, hatukupeleka wapiganaji bungeni bali tumepeleka viongozi wa kutunga sheria" alisisitiza Freeman Mbowe

Mbali na hilo Mbowe anasema kitendo cha Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai kulivalia njuga suala hilo ni jambo ambalo yeye limemsikitisha.

"Kitendo cha kuwapeleka polisi na kuwashtaki wabunge wetu na Spika wa Bunge kushadadia jambo hili limenisikitisha sana, Spika kusema ametoa ruhusa wahukumiwe kwa kesi za jinai ni mwendelezo wa kutaka kutunyamazisha, ila hatutayumba na tunaamini kuwa jopo la majaji litatenda haki katika jambo hili, maana hakuna mbunge yoyote wa CHADEMA wala UKAWA ambaye amemshambulia mbunge yoyote yule bungeni" alisisitiza Mbowe.

Katika watuhumiwa wote nane, mtuhumiwa mmoja ambaye ni Mbunge wa jimbo la Ubungo, Mbunge Saed Kubenea leo alipandishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa moja la shambulio la kawaida hivyo amedhaminiwa na shauri hilo upelelezi wake bado haujakamilika hivyo kesi itatajwa tena tarehe 26, Julai 2017 Dodoma.

Chanzo: EATV
"kutaka kutunyamazisha" Hiki ndio kichaka cha kufanyia fujo, swaga zilezile
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom