Freeman Mbowe awasili kituo kikuu cha Mabasi Ubungo na kulakiwa kwa shangwe kubwa

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amrwasili muda huu hapa Ubungo Bus Terminal kuzungumza na madereva waliogoma na amelakiwa kwa shangwe kubwa sana.

Hakika ni shangwe kubwa hapa na madereva wanapaaza sauti kumtaka Mbowe awasaidie..

Taarifa zaidi zitafuata hivi Punde nikiwa na Kamanda Standalone kwenye msafara wa Mwenyekiti..

[h=2]CHADEMA kuasisi mgomo wa madereva ni kwa manufaa ya nani?[/h]
Kwa mda mrefu chadema wamekuwa na mipango mingi ya kuhakikisha kuwa serikali ya Rais kikwete inashindwa kutawala na hatimaye ianguke japo lengo lao bado halijafanikiwa kwa kiwango wanachotaka wao. hii ni kutokana na uimara wa Rais kikwete pamoja na viongozi wanaomsaidia katika kutekeleza majukumu yake.


kwa kurejea kidogo tu chadema wameweza kuasisi mandamano mengi haramu ambayo yalikuwa na lengo la kuvuruga nchi na kufanya isitawalike,kama haitoshi chadema pia walishirikiana na baadhi ya watu wakiwemo waroho wa madaraka katika tasisi za afya na kuaandaa mgomo wa madaktari ambao uliishia kwa baadhi ya madaktari wetu kupoteza kazi na kupotea kwa maisha kwa baadhi ya watu wetu.


Lakini pia chadema wamejaribu kuandaa mipango mingi ya kushinikiza watumishi kwenye kada nyingi wagome pasipo sabubu za msingi japo hawajapata mwitikio mzuri kutoka kwenye jamii.


Kwa sasa chadema wanahangaika na kuwashawishi madereva wagome kwa malengo yaleyale ya kusababisha serikali ichukiwe na watanzania ili wao wapate agenda ya kusema majukwaani,nimeweza kushuhudia kwa macho na masikio yangu baadhi ya viongozi wa chadema wakiongozwa na John Mnyika pamoja na Tundu Lisu wakiwa kwenye vikao na viongozi wa madereva wakiwataka wawashawishi madereva wenzao wagome kutoa huduma ya usafiri kwa lengo la kuikomoa serikali ya jk.


Jambo kubwa la msingi hapa ni kwamba serikali kazi yao ni kutengeneza barabara pamoja na miundo mbinu yote ambayo itawasaidia wasafirishaki kusafirisha abiria katika hali ambayo ni njema zaidi.


Mimi nijuavyo serikali hawahusiki na jukumu la usafirishaji jukumu hili liko mikononi mwa sekta binfasi. Hii ni baada ya serikali kujiondoa kwenye mambo ya kibishara na kuaachia sekta binafsi sasa iweje mnyika,Lisu na wafuasi wao wawashawishi madereva kudai madai yao serikalini wakati wakijua wao mwajiri wao siyo serikali?


Madereva lazima watambue kuwa mambo yao yanapaswa kupelekwa kwa waajiri wao wakajadili na kukubaliana namna nzuri ya utendaji kazi lakini siyo kulazima serikali ifanye kazi ya waajili wao.


Jambo kubwa linalo nisumbua ni kweli Lisu na mnyika hawajui kuwa madereva mwajiri wao siyo serikali? Je ni kweli mnyika na Lisu hawajui kuwa mikataba ya kazi ya madereva lazima ifanyike baina ya mwajiri wao na madereva husika?


katika hatua nyingine ambayo inafanya niwaze ni pale mnyika na Lisu wanapokuwa mstari wa mbele kutengeneza mgomo bila kujali watu wanateseka kiasi gani halafu wanajiita ni wapigania haki za watu.Nashindwa kuwajua hawa makamanda wao wanachotaka nini kwa watanzania manake kila wanachofanya lazima wapange mgomo bila kujua watanzania wanateseka kiasi gani.


Hili nalisema kwa ukweli kabisa nimeshuhudia vikao vya hawa waheshimiwa vikifanyika usiku kupanga hii mipango miovu isiyokuwa na tija kwa watanzania.


 
Fikiria kwa mapana utagundua mbowe alishatambua kuwa dili lao litaback fire ndio maana kaenda pale. Hoja za madereva kwa serikali ilikuwa swala la Tochi za barabarani na serikali ikaziondoa ikaja hoja ya shule pia serikali ikaiondoa. Hoja zilibaki ni mikataba ya ajira sasa hiyo mikataba wanataka serikali itatue nini? Kwani ni waajiriwa wa serikali?

Ishu ya mikataba walitakiwa wamalizane wao na waajiri wao na kikubwa ilitakiwa chama chao ndio kisimamie na ikishindikana basi wakawashtaki hao waajiri wao katika vyombo husika. Yaani leo ndio mmethibitisha kweli CHADEMA MAZEZETA na ndio maana Maoperation kibao mnafanya hampati matokeo mazuri. Always remember strategy bila tactics hamtafika popote MAPIMBI NYIE.

Naona chama chenu cha wasaliti mnatafuta pa kutokea.
 
Nchi haina Uongozi? au ndo iko kwenye autopilot kama alivyosema Mbowe? ... Hope CHADEMA watafanikiwa kutatua mgogoro huu maana inaonekana kuwa CCM wanataka kukabidhi nchi ikiwa haitawaliki tena ...

Mkuu wa nchi yupo marekani huku dollar ikiwa inaimaliza shilingi, na madereva wa public transport wakiwa kwenye mgomo.

Ninahisi CHADEMA wanahusika na kuporomoka kwa value ya shilingi dhidi ya dollar.
 
Achana nao CHADEMA wana siasa za kitoto sana. Wanajitekenya kisha wanacheka wenyewe. Tangu mwanzo wenye akili walishajua kuwa huo mgomo uko politically motivated na chadema ndio wanaohusika.

Mbinu zimewaishia, wanatesa wananchi kwa maslahi yao PUMBAFUU SANA HAWA JAMAA. Walianza na madaktari wameua watu serikali ikaingilia kati umeisha wamekuja na usafiri na serikali imewachunia naona wameamua wakajifanye wamesuluhisha.

Wapuuzi zaidi ni hawa madereva.
 
Taarifa inayotangazwa sasa hivi katika vyombo vya habari mgomo wa madereva umekwisha baada ya serikali kukubali madai ya madereva na kusaini madai yao kiongozi mmoja wa serikali ndie alie saini( hawakumtaja jina)
 
Achana nao CHADEMA wana siasa za kitoto sana. Wanajitekenya kisha wanacheka wenyewe. Tangu mwanzo wenye akili walishajua kuwa huo mgomo uko politically motivated na chadema ndio wanaohusika.

Mbinu zimewaishia, wanatesa wananchi kwa maslahi yao PUMBAFUU SANA HAWA JAMAA. Walianza na madaktari wameua watu serikali ikaingilia kati umeisha wamekuja na usafiri na serikali imewachunia naona wameamua wakajifanye wamesuluhisha.

aiseeee chadema ina nguvu...kumbe ni chadema??hahaha mbowe ameweza kufanya madereva wote tanzania kugoma..basi wana nguvu sanaa kuliko tunavyofikiri
 
mtaongea mengi humu ila kwangu mimi mwananchi wa kawaida niliyeteseka na mgomo huu najua mambo mawili tu.Kwamba nimeona huduma ya usafiri ikisimama na kunifanya niteseke.Kwamba nimeona mzee mmoja anavaaga miwani ya jua na combat ameenda Ubungo, ameshangiliwa sana, hajaongea sana, lakini mawe yakaacha kurushwa, viongozi wa

serikali wakaenda na kusikilizwa, usafiri umerudi tena, tumaini limerejea.This guy with sunglasses, nimezoea kumuona magazetini na kwenye tv...this guy..who is he? I wanna know him more, I wanna know why he is wearing combats, I wanna know why in his presence things are just keep going like this.
 
kwahiyo ameshawapa mikataba ya kazi hao madereva?
soma hapa patakusaidia

Mbowe kawaambia sentensi moja tu... "Serikali iliyopo haina uwezo wa kutatua matatizo sio ya nyie tu madereva, bali na makundi mengine ya kijamii ikiwemo wakulima, wafugaji, walimu, madaktari, wauguzi, askari nk... hivyo njia pekee ni nyie kuendelea na kazi na kuvumilia miezi michache iliyobaki kisha itaingia serikali makini itatue matatizo yenu"..
 
Ni kweli ulichosema CHADEMA wanatumia siasa chafu bila kujali wanamuumiza nani.Madai ya madereva wanaoungwa mkono na CHADEMA yanaumiza wamiliki wa magari nchi nzima.Hivyo kama kuna mmiliki wa mabasi yuko CHADEMA na anachangia pesa CHADEMA namwonea huruma.

Pia mgomo uliochochewa na CHADEMA umeumiza wapiga kura na kuwaathiri vibaya mno.Hivyo kila mpiga kura aliyeumizwa na huu mgomo uliochochewa na CHADEMA mwezi wa kumi akiipigia kura CHADEMA au akiichangia CHADEMA HELA mimi nitamwona ni mwehu.Waathirika wote AMBAO NI wamiliki wa magari na wapiga kura ACHANENI NA chadema inayowaumiza.

Hapa tu wanaumiza wananchi bila kujali hawajapata dola.Wakikamata dola watakuwa balaa hawa.Wanasema ogopa mtu anayekumulika na tochi mchana ikifika usiku atakuchoma.Katika vyama vilivyoua na kutesa watu wengi ni CHADEMA.Chadema ilichochea mgomo wa madaktari watu kibao wakafa kwa kukosa matibabu sasa walioteseka hawana idadi kwa huu mgomo waliochochea.Wananchi kaeni mbali na CHADEMA tafuteni kujiunga na vyama vingine sio chama uaji na tesaji kama CHADEMA.
Alafu pia hawa chadema wamesababisha nvua ipungue sana msimu huu!, yahani wamesababisha mafuriko kule arusha na dumila,
 
Tatizo Pinda hakusoma muda,na pili aliogopa anaenda kuwaambia nini?Hapo hakuna siasa,Mbowe ametumia MUDA tu na amepata CREDIT,walikuwa wanamuhitaji Pinda,akaleta Mizengwe kisa kadanganywa na Seven,shauri yenu siyo kila kitu siasa,tunatakiwa kuwa watu wakutumia akili za kuzaliwa.

Tusichague Politicians without Performance,tunatakiwa kuwa na Politicians with Performance,wakiangalia RESULTS based activity..................pole MwanaCCM Mtanzania mwenzangu ambaye hujagundua wanasiasa wanavyofanya kazi.............

Ndugu kosa moja la kipa linaleta GOLI.....................Tunatakiwa kuwa TAIFA :grouphug: na si MAADUI

Pinda alishajua nini kiko nyuma ya pazia. Jiulize leo tangu asubuhi wamegoma nani kashindwa kwenda kazini? Ukimya wa serikali umewashtua waliochochea huo mgomo na mwisho wa siku wangekuja umbuka. Hao jamaa walilianzisha na wenzao Serikali wakaja na Plan B.

Ukiangalia kwa makini walichotegemea hao wapinzani ni serikali itoe matamko ambayo wao watayachukulia kama njia ya kuanzisha vurugu. Pia walisahau kuwa huo mgomo ungezidi hata siku tano hao madereva wote waningekuwa na kazi coz hakuna tajiri asiyetaka faida huku benki zikiwapumulia shingoni.

Wamepotea sana. Leo nimeamini kweli tuna serikali imara na isiyotetereka hata kidogo. Salute kwa Kikwete Rais wa Tanzania na cabinet nzima Big up sana wametuonyesha kweli hatukufanya makosa kuwachagua na pia tutawachagua tena October 2015
 
Taarifa inayotangazwa sasa hivi katika vyombo vya habari mgomo wa madereva umekwisha baada ya serikali kukubali madai ya madereva na kusaini madai yao kiongozi mmoja wa serikali ndie alie saini( hawakumtaja jina)

Unataka wasemeje? Ni yule aliyefukuzwa na mawe asubuhi?
 
Mbowe kafanya kazi ya serikali anayoitumikia, wananchi tunapiga makofi. Siasa na governance ya nchi inahitaji akili ya ndani saaana kuielewa!

Kapakua chakula alicho kipika mwenyewe.
 
Mgomo wa siku mbili umemalizwa kwa dakika tano tena na mtu asiyemtawala ni PM kivuli tu.... je ukimpa nchi....


Tuwape UKAWA nchi tuone
 
aiseeee chadema ina nguvu...kumbe ni chadema??hahaha mbowe ameweza kufanya madereva wote tanzania kugoma..basi wana nguvu sanaa kuliko tunavyofikiri

Kimya kingi kina mshindo mkuu. Angesubiria kidogo aone kilichokuwa kinaenda kutokea. Nahisi walifikiri kuwa TISS Wanajiandaa tayari wameshajipanga wafanye ile kitu inaitwa Funika Kombe Mwanaharamu Apite. Na ingefanikiwa hiyo nahisi usingesikia tena mgomo wa madereva kama ambavyo haitatokea uje kusikia mgomo wa Madaktari kwa miaka ya hivi karibuni
 
Pinda alishajua nini kiko nyuma ya pazia. Jiulize leo tangu asubuhi wamegoma nani kashindwa kwenda kazini? Ukimya wa serikali umewashtua waliochochea huo mgomo na mwisho wa siku wangekuja umbuka. Hao jamaa walilianzisha na wenzao Serikali wakaja na Plan B.

Ukiangalia kwa makini walichotegemea hao wapinzani ni serikali itoe matamko ambayo wao watayachukulia kama njia ya kuanzisha vurugu. Pia walisahau kuwa huo mgomo ungezidi hata siku tano hao madereva wote waningekuwa na kazi coz hakuna tajiri asiyetaka faida huku benki zikiwapumulia shingoni.

Wamepotea sana. Leo nimeamini kweli tuna serikali imara na isiyotetereka hata kidogo. Salute kwa Kikwete Rais wa Tanzania na cabinet nzima Big up sana wametuonyesha kweli hatukufanya makosa kuwachagua na pia tutawachagua tena October 2015

Ama kweli wajinga hawaishi ulimwenguni.akili mgandovkama uliyonayo haiwez kutambua athari za mgomo huu nchini.pole mzee.
 
Back
Top Bottom