Inawezekana ndugu hermanthegreat,
kuwa na wifi yako inawezekana kabisa tena bure ila internet ndio sio bure , cha kufanya kuwa na wireless router alafu connect router na computer yako kwa kutumia ethernet cable.
- Fungua browser yoyote kama chrome alafu ingiza default IP address ya router ambayo utaikuta imeandikwa kwenye stika kama iyo router ni mpya na kama sio mpya au hujui tumia 192.168.1.1 au 192.168.0.1 au 192.168.2.1 alafu bonyeza enter .
-Itafunguka interface ya kuweka username na password , sasa apo tumia za kwenye stika iliyopo kwenye router au kama hauna pale kwenye username jaza (admin) na password jaza pia (admin) bila mabano, alafu ingia, kama ikigoma itabidi u reset iyo router alafu uingie tena itakubali, kikubwa ujue ku reset.
-Itakuja interface ya ndani ya router na utaona setting nyingi tu, mpaka apo utakuwa umeingia ndani ya router , sasa fanya configaration kama kutengeneza jina la wi-fi yako na password, kwenye password chagua WPA2 maana ni salama zaidi alafu save.
-Mpaka apo unaweza kujaribu hata kwenye simu ukaiona.
Ishu ya speed sio wewe bali ni ISP(Internet Service Provider) anaekupa internet ndo anaamua akupe speed gani sio wewe.