Majiji yetu yamelala mno ingetakiwa ukiingia Dar/Mwanza/Arusha/Mbeya/Moshi unaconnect free wifi?
Vyuoni ni upofu wa TCRA na TCU. Ingekuwa ni lazima na wapewe special rates unlimited.
Kwanini basi la mwarabu liwe na wifi vyuo vikuu ishindikane?
We hujui hata tuko wapi.TCRA na TCU wanaingiaje hapa ?
Mitandao ya simu (Tigo,Airtel,Vodacom &Halotel) wana vifurushi maalum kwa wanavyuo
kuna cable zilichimbiwa chini wenyewe wanaita mkongo wa taifa hizi unaweza ukazivuta hadi mahali unapotaka kuna vitu wanakufungia kisha unaweza kuruhusu free wife eneo hilo
UDSM kuna free wifi hii imewekwa kuwasaidia wanafunzi ku-download material yao lakini wengine wanaitumia ku-download movie/music.Nimesikia TTCL wamesign contract na DART kuweka wifi kwenye vituo vyote vya DART
Tanzania hii hii?
Bossman, unajua kuwa JNIA kuwa Wi-Fi ya bure?
Na naijua migawaha mingi Dar ambayo ina hiyo huduma.
Boogie Woogie wanayo, Samaki Samaki wanayo, Rhapsody's wanayo....na wengineo wengi tu.
Hizo sehemu nafahamu zipo....
but nilikuwa hasa nafikiria maeneo ya watu weengi zaidi....
mfano labda eneo lote la ferry na posta....
au vituo vyote vya UDART....
Kuna fibre zilipitishwa chini ya ardhi maeneo ya Mbezi Beach zaidi ya miezi miwili iliyopita, sina hakika kama kuna Watu wameunganishwa! Ingewezekana sana kutumia huo mfumo nafuu kwa ajili ya Wifi hasa kwenye eneo lote la beach.
kampuni gani walipitisha?