Free Media na mkono wa Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Free Media na mkono wa Lowassa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rapkatuni, Nov 24, 2011.

 1. R

  Rapkatuni Member

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika siku za karibuni niliwahi kuandika juu ya wanasiasa ambao wanatumia wanataaluma wa habari katika kujisafisha na kujipigia debe kwa kuwanunua kwa kiasi kichache cha pesa waandishi na wahariri wa vyombo vya habari, ambao kwa njaa yao na ufupi wa fikra wamekuwa tayari kupotosha na kutoa habari za uongo ili wapate fungu kutoka kwa "mabwana wakubwa wao" .

  Miongoni mwa mambo niliyowahi kuyalalamikia na kuwaomba wanahabari kuwa makini nayo na kujirekebisha ni pamoja na kujizuilia kutumika kisiasa kwa kuipotosha jamii..,wengi katika wanaharakati na wachambuzi wa mambo wamekuwa wakiliongelea na kulaani hili la vyombo vya habari kutumika katika kuendeleza chuki na misimamo inayolenga kuligawa taifa katika itikadi tofauti kubwa zikiwemo za udini, ukabila na uchama.

  Hivi leo, moja katika magazeti yaliyo mstari wa mbele katika kupotosha umma wa watanzania (TanzaniaDaima) limeendeleza kuandika habari za upotoshaji kwenye ukurasa wake wa mbele kwa habari isemayo " pesa zamwaga kumng'oa Lowasa"

  Habari hii ukiisoma utaweza kujua ni kwa kiasi gani taaluma ya uandishi ilivyobakwa na waandishi uchwara wenye kukinga mkono kwa ajili ya vijisenti. Mbowe nae ni katika watu wanaojiingiza katika mstari wa mbele kutetea udini na mafisadi kupitia vyombo vyake hivi.

  TUWE MAKINI NA GAZETI HILI NA MFANO WAKE....!
   
 2. d

  dala dala Senior Member

  #2
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Je, wewe wadhani taarifa ya UKWELI ni ipi? Tueleze ukweli unaoujua wewe tofauti na ulioandikwa kwenye Tz Daima.
   
 3. mkada

  mkada JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  rapkatuni nakubaliana na wewe,i think there too much chumvi on lowassa kuliko ukweli,na kwa tabia ya watz ya kusombwa na mitizamo ya wengine wachache bila wao kufikiri critically,lowassa anaonekana a monster kwelikweli,kuna kitu kimoja mi nampenda lowasa,he is a hardworkin guy,mkali kwa wala rushwa na wavivu,sio evasive wa mambo,na hana theories za kufikilika,he so practical kiasi kwamba anaweza kufanya mabadiliko huku akijiamini,na i doubt kwamba walioneza sumu lowassa achukiwe ni watu walio kumbana na mkono wake,the guy sio wa mchezo chezo eti,,,suala la kama amejilimbikizia kipesa,nani hajafanya hivyo??ok labda upinzani wako safi,,CUF wako wapi sasa baada ya kupata madaraka,mwisho wa siku ukute hata chadema wakiingia madarakani watatufanya kama CUF walivyo wafanya wanachama wao,,,,
  hebu watz tubadilike namna ya kufikili,kama ilivyo marekani na nchi zingine,mtu hata kama ni wa chama pinzani,si vibaya ukaaanisha mazuri yake na mabaya yake,sio mabaya yake tu,lowassa mazuri yake yanampita hata pinda mtoto wa mkuliima,nnamini lowassa angekuwa madarakani leo hii bila shaka tz ingekuwa imeshuhudia maamuzi magumu ambayo watz tungekuwa tunajivunia tunapoingia miaka hii 50 ya nchi yetu.
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Nilishaacha kulisoma TanzaniaDaima siku nyingi.
   
 5. vipik2

  vipik2 JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,175
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Mbowe kaingiaje kwenye uandishi? habari yako ni nzuri lakini mwisho umechanganya makande na pilau,
   
 6. s

  sheeupupu New Member

  #6
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nadhani hoja yako ingekua na nguvu kama ungeainisha ni kwa namna gani taarifa hiyo sio sahihi,na uthibitisho walau wa kimazingira wa jinsii mwandishi au mhariri anavyoweza kuwa amenunuliwa na mh Lowasa ili aandike habari hiyo.kama una vielelezo zaid weka jamvini ili kuipa nguvu hoja,vinginevyo usilazimishe hisia zako kuwa ukweli.
   
 7. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #7
  Nov 24, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Bila hata kumwaga shilingi,
  Huyu hafai na anatakiwa kuondolewa kwa haraka sana!
   
 8. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #8
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Aliye msafi na ampige mawe lowassa!!!
   
 9. M

  Mabewa Senior Member

  #9
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 30, 2011
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi mmesahau 6 livyosema kuhusu kubanda?nilikuwa namheshimu kweli lkn ananifanya nifikirie ma2 kununua gazeti lake siku hizi.Anatetea ukaskazini jamani raisi aweza toka popote Tanzania sio lazima huKo..jirekebishe kubanda na habari zako utamuharibia mwenzio biashara au labda awe amekutuma kutekeleza deal.Hivi lowasa mpaka watu watoe hela?mm nampenda lkn hafai kuwa p.hayo ni mawazo yangu
   
 10. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #10
  Nov 24, 2011
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tanzania Daima limekuwa likitumiwa sana na Lowassa kupotosha ukweli wa mambo. Huyu ndiye anayewatuma akina Kibanda wamshambulie adui yake kisiasa, Samwel Sitta. Ukisoma habari ya ukurasa wa kwanza ya Tanzania Daima 'Fedha zamwagwa kumng'oa Lowassa' utagundua jinsi magamba wanavyolitumia hili gazeti linalopaswa kuwa mstari wa mbele kupiga vita corruption.
   
 11. K

  Kintiku JF-Expert Member

  #11
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 607
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Tunaamini katika uhuru wa habari, tunaamini wahariri kutoingiliwa na wamiliki katika kuamua nini kiandikwe/kisemwe kwenye media house zao. Lakini hebu jiulize kitu gani kitatokea kwa wahariri wa vyombo vifuatavyo endapo wataandika habari kama hizi tena kurasa za mbele:

  Nipashe- Yusuph Manji anasingiziwa kashfa ya Kagoda

  RAI- Dr. Mwakyembe ahujumiwa na Mfanyabiashara mashuhuri nchini

  Uhuru: Dr Slaa alalamika CCM kuchakachua matokeo ya Urais 2010

  Al Nuur: Mkutano wa Injili watikisa Bagamoyo Yesu Kristo ahuburiwa kwa kishindo

  Nadhani wote tunakubali kuwa wahariri hao kesho yake watakuwa hawana ajira (refer Sakina Datoo, marehemu Yahaya Buzaragi, Balinagwe Mwambungu, etc.

  Kwa muda mrefu gazeti la Tanzania Daima limekuwa likiandika habari za kuwapamba wale ambao mmiliki wake amekuwa mchana anawaita mafisadi lakini usiku anaenda newsroom na kuwaita mashujaa. Ingekuwa ni mara moja tungesema labda mhariri alifanya bila mmiliki kujua na akamwonya. Lakini kwa vile imekuwa ni kawaida sasa, hatuna shaka kuamini kuwa huo ndio msimamo wa mmiliki wa gazeti.

  Haiwezekani FreeMan gazeti lako liwe linaandika msimamo tofauti na wa chama chako. Sisi unatuchanganya, hatukuelewi ikizingatia huko nyuma kumeshakuwa na matukio mengi ya msimamo wako kutiliwa shaka. Kwa hili naona nitoe hoja.

  NATOA HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA MBOWE...............WANAOUNGA MKONO TUANZE HUO MKAKATI
   
 12. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #12
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Ni habari ipi unayoi-refer katika allegations zako???
   
 13. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #13
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  There is no way ...Itabidi UWENAYO!!!
   
 14. M

  Mwera JF-Expert Member

  #14
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyo mbowe ni mangi ameshakatiwa mshiko na mafisadi unazani ataendelea kuwaandika vibaya wakati keshakatiwa mshiko?aithee mangi umekufaje bila kulipa hela yangu mangii?? Ungenipa hela yangu kwanza ndio ufe aisee!!
   
 15. Dumelang

  Dumelang JF-Expert Member

  #15
  Nov 24, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 2,187
  Likes Received: 1,538
  Trophy Points: 280
  kama uliyoandika ni kweli basi mimi namsifu mbowe naninazidi kuwa na imani naye!! ..kwanini ? kwasababu huo ndio uhuru wa vyombo vya habari, mbowe hatakiwi kuliingilia gazeti kwa chochote kwani media inatakiwa isiwe na bias...ni kweli tanzania daima imekuwa ikibalance sana habari zake tofauti na gazeti la makada....huo ndo uhuru wa kweli kwa vyombo vya habari...jenga imani yako kwa mbowe
   
 16. K

  Kintiku JF-Expert Member

  #16
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 607
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Tujadili suala hili bila kuweka ushabiki wa kisiasa. Tuwe wakweli wa nafsi zetu. Je magazeti mengine yangeandika hivyo tungeyapongeze? Mbona magazeti ya CCM/Serikali yakiwaponda CDM huwa watu wanalalamika sana. Unajua huwezi kutofautisha msimamo wa kisiasa wa mmiliki wa media house na yale anayoyoyatangaza. Mifano ipo dunia nzima kila mtu anajua media house fulani inaunga mkono upande upi. Naomba CDM tusiwe na vipimo viwili.

  Hivi ni kweli jinsi watu wanavyomsema Lowassa humu ndani na kwenye majukwaa ya kisias kuwa ni fisadi halafu unaenda kwenye gazeti la TD unakuta habari tofauti. Je ni kweli mashabiki wa CDM mnapata furaha mkiona hivyo?
   
 17. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #17
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  U r not clear at all. NO STANDIND POINT
   
 18. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #18
  Nov 24, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,059
  Likes Received: 7,276
  Trophy Points: 280
  Wewe kutokua na imani na Mh. Mbowe sio issue sana kwa sababu sio watu wote wenye imani na wewe vilevile!!
   
 19. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #19
  Nov 24, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,874
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  ww kutokuwa na imani mb mbowe is not an issue hata YESU hakubaliki na watu wote ni suala la individual differences kwahyo lisikuumize kchwa. Nalog in...
   
 20. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #20
  Nov 24, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Unategemea nini kutoka kwa DJ?
  OTIS
   
Loading...