Aliyekuwa Rasi wa pili wa Zambia, Frederick Jacob Titus Chiluba (68), amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo nchini Zambia. Chiluba, ambaye aliiongoza Zambia kuanzia mwaka 1991 - 2002, hadi jana mchana inadaiwa alionekana mwenye afya njema, lakini ilipofika saa 6 usiku aliugua ghafla na kuaga duania. Hadi sasa hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu sababu za kifo chake. Katika siku za karibuni, Chiluba alikuwa akikabiliwa na kesi ya ubadhirifu wa mali ya umma wakati akiwa rais wa nchi hiyo.
pema wapi, aende ajibu mashitaka. Amekwenda kwenye mahakama ya haki, akahukumiwe . Wangapi wamekufa kwa ajili yake wacha afe apate hukumu ya kweli kwa muumba wake. Asifunguliwe mlango mpaka aliowaua/watesa duniani wamkute mlangoni