Forget Magufulisation, here is the reality

Forget Magufulisation, here is the reality

Inawezekana. Lakini inahitaji kufanya kazi kweli zaidi ya kucheza na mindsets za watanzania. Inahitaji mabadiliko makubwa sana ya mfumo wa uongozi na uwajibikaji. Hii inamaanisha, inahitaji Magufuli ajitenge kikwelikweli na 'zigo' la CCM. Na namna ya kujitenga inafahamika na ipo ndani ya uwezo wake kama rais. Akiweza kufanya hivyo, hakika ndani ya miaka 5, prosperity index yetu yaweza kuwa bora.

tatizo mifumo ya vyama vetu navyo ni hovyo mfano CCM/CDM mwenyekiti wa chama ndo ana nguvu kuzidi hata chama-mwenyekiti kikwete unategemea nini.maigizo kama kawa
 
Umesoma na kuelewa kweli? Ebu rudia tena kusoma.
Na kama unaelewa 'Magufulisation' ni nini, itakuwa rahisi kuelewa zaidi.

Lakini pia, kumbuka hii ni serikali ya chama kilekile cha utawala (napendelea zaidi uongozi badala ya utawala, lakini kwa kuwa kiuhalisia ni utawala, ngoja nitumie utawala) uliopita. Kilichofanyika ni mabadiliko ya mtu anayeongoza utawala. Ingawa ni kweli kabisa, mtawala huyu akiamua kuweka maslahi ya nchi mbele, anaweza kujitofautisha na utawala uliopita. Na hii naiona ni shida: kutaka kuitenga CCM na Magufuli. 'Zigo' la CCM Magufuli hawezi kuliepuka mpaka pale atakavyotenda kama statesman.

Hivyo basi, hata kama amekaa siku 52 madarakani, haimaanishi masuala ya prosperity hayamhusu. La hasha! Hizo poor rankings zimesababishwa na serikali za chama kilichopo madarakani. Kwa kuwa Magufuli naye anatokana na chama hicho hicho, hawezi kukwepa lawama na majukumu katika hili. Kwa hiyo, nilichofanya ni kumkumbusha uhalisia uliopo mtaani. Ingawa naamini anaweza kuwa anafahamu; siyo vibaya kumkumbusha. Aweke nguvu huko kunakohitajika zaidi. Na nimeweka hilo katika kuwakumbusha fanatics wa Magufulisation kuwa uhalisia mtaani haupo kama vile wanavyotaka kuuaminisha ulimwengu.

Sasa labda nikusaidie tu: hizo rankings zinaonyesha, in fact zinathibitisha tu hali halisi ilivyo on the ground. Hii 'Magufulisation' trend ya kucheza na mindsets za waTZ kupitia media haiendani na hali halisi ilivyo. Na nikasema, majawabu yote yapo mezani kwa Magufuli. Anachopaswa kufanya ni kufikiri na kufanya maamuzi kama kiongozi mwenye kuweka maslahi mapana ya nchi na siyo chama. Hii inamaanisha hata kama ni kwa kubadili status quo iliyotengenezwa na chama, na kumjengea maadui ndani ya chama.
umeeleweka mkuu, lakini mbadiliko ya kweli hayatatokea kama hataanza na wale waliofyeka fedha za taifa hili bado wana enjoy maisha, mfano A.Chenge alifyeka fedha za rada , bado tunacheka naye tu, waliofyeka fedha za EPA wakaambiwa warudishe sijui kama walirudisha maana orodha haikutoka kama ya wale wa makontainer, walifyeka fedha za kukopeshwa Dola mil. 600 ndio kabisa hawajaguswa had SFO inashangaa, walificha fedha ulaya, haya tuseme ZITTO hajampelekea orodha au ilikuwa kanjanja, ifike hatua magufuri afufue kesi za zamani ambazo watu walikwiba fedha na hawakuchukuliwa hatua, fedha hizo zikikusanywa zitatuvusha.
 
Nzi thank you for the background updated information concerning many issues of great value for the well being of our nation.

Mine are few remarks:-

1. What do you think Dr. Magufuli should do for the eight mentioned issues so that he can take our nation to the next level.
Identifying a problem without unveiling proposed solutions is not the character of a Great Thinker.

2. What is the contribution of the party to the eight mentioned issues.

3. What is the culture of Tanzanians? Do you think with this culture of ours we can easily tackle the eight mentioned problems and have our breakthrough?

4. We are the least ranked in education and better in personal freedom, what are your views concerning that.

5. Can you plz show the list of countries surveyed? What is the benchmarks for East African Countries??

Thank you.

Queen Esther
 
Mi nadhani hata kama chadema wangetangazwa kushida uchaguzi uliopita namba zingebaki kuwa hizohizo tu,cha msingi tumpe mda magufuri tuone kama namba zitachange kitu ambacho kwa mtazamo wangu naona kitashindikana kwa approach aloanza Nayo.

Hivi ni kwanini watu huwa mnashindwa kujadili mada bila kuweka u-CCM na u-CHADEMA?
 
tatizo mifumo ya vyama vetu navyo ni hovyo mfano CCM/CDM mwenyekiti wa chama ndo ana nguvu kuzidi hata chama-mwenyekiti kikwete unategemea nini.maigizo kama kawa

umeeleweka mkuu, lakini mbadiliko ya kweli hayatatokea kama hataanza na wale waliofyeka fedha za taifa hili bado wana enjoy maisha, mfano A.Chenge alifyeka fedha za rada , bado tunacheka naye tu, waliofyeka fedha za EPA wakaambiwa warudishe sijui kama walirudisha maana orodha haikutoka kama ya wale wa makontainer, walifyeka fedha za kukopeshwa Dola mil. 600 ndio kabisa hawajaguswa had SFO inashangaa, walificha fedha ulaya, haya tuseme ZITTO hajampelekea orodha au ilikuwa kanjanja, ifike hatua magufuri afufue kesi za zamani ambazo watu walikwiba fedha na hawakuchukuliwa hatua, fedha hizo zikikusanywa zitatuvusha.

Hilo ndilo la kubadili status quo. Lazima rais ajiweke mbali na chama, hata kama hilo litamjengea maadui ndani chama, lakini atakuwa akifanya jambo jema kwa wananchi walio wengi.

Na ndiyo maana mimi siyo mwumini wa kutaka rais awe mwenyekiti pia wa chama, hivi ndivyo kunamfanya afungwe na maslahi ya chama, badala ya taifa. Kwa madaraka na mamlaka aliyonayo kikatiba, rais ni mtu mkubwa mno mbele ya mwenyekiti wa chama. Hivyo hata kama asipokuwa mwenyekiti, kama kweli ataweka maslahi ya taifa mbele, hakuna anayeweza kumbabaisha.

Ila kama mnavyoonyesha wasiwasi, nami pia napata wasiwasi kidogo kama kweli rais ataweza kuacha u-partisanship na kuwa statesman. Hakika nawaambieni, akiweza kufanya hivi, basi ndani ya miaka mitano, prosperity index yetu itakuwa imeboreka sana.
 
Jiulize utatokaje sio Magufuli atakutoaje??? Kumbuka slogan Yake ya hapa kazi tu. Hiyo ndiyo itakayotutoa. Watanzania tufanye kazi tupunguze majungu.

Queen Esther

Labda rudia tena kusoma utaelewa! Sasa hivi Magufuli ndo Mkuu wa nchi ulitaka wamwongelee kikwete tena hapa? Magufuli afikrie anatutoaje huko! Na hii kwenye governance mwakani lazima tuporomoke tu, kwa haya mambo ya Zanzibar na kuzuia mikutano ya wapinzani huku wenyewe ccm wakifanya mikutano ni upumbavu uliopita kiwango cha upumbavu! Mwakani tutakuwa wa 140!
 
mkuu kwani yeye amesema kuwa magufuli ndio kasabibisha,kimsingi haya yote ni kutokana na utawala mbovu wa ccm kwa miaka yote

Magufuli anatumia bajeti ya 2015/2016. Kama ili kuwa mbovu sio rahisi kuifumua yote bali kuna mambo matatu ya kufanya ili atimize yaliyomo katika bajeti ya 2915/2016 1. Kupitia upya bajeti na kufanya "reallocation" bila kuadhiri bajeti kuu kama ilivyopitishwa na bunge Juni 2015. 2. Kuimarisha ukusanyaji wa mapato kutoka kila chanzo halali na kuhakikisha kuwa huduma za kulipa kodi zinazofanana zinatolewa kwenye dirisha moja 3. Kuimarisha dhana ya "value for money" kwa kila aina ya malipo. Kupitia upya aina zote za posho na kujiridhisha zipi zifutwe na zipi zibaki na ikibidi zipunguzwe malipo yake. Vikao vingi vya Bodi hutanguliwa na Vikao vya kamati ambavyo huchukua Karibu wiki moja halafu Bodi nayo huchukua karibu wiki moja. Kama mkuu wa taasisi atakuwa ameandaa vizuri makabrasha ya Bodi vikao vyote vinaweza kufanywa ndani ya wiki. Pia Vikao vyote vitumie kumbi za taasisi husika. Iwe marufuku kufanya vikao vya Bodi kwenye mahoteli.
Baada ya bajeti ya 2015/2016 Magufuli ataandaa bajeti yake ya kwanza 2016/2017 na baada ya hapo apimwe kwenye mzani wa "Prosperity Index".
Pia tunaomba mtoa mada atuonyeshe serikali ya awamu ya nne "Prosperity Indices" zake zilikuwaje kutoka 2004/2005 hadi 2014/2015
 
Queen Esther;14972846 said:
1. What do you think Dr. Magufuli should do for the eight mentioned issues so that he can take our nation to the next level.
Identifying a problem without unveiling proposed solutions is not the character of a Great Thinker.

This would require its own thread for fruitful discussions. But, one thing I can assure you is that, our nation's problems aren't completely new to most of us. They have been well researched and solutions proposed to each of the problem.

Most of the solutions require an overhaul of the existing system [this needs a statesman, and not a partisan]. Other solutions require Tanzania to say NO to stupid IMF and World Bank policies. They have never worked. And I wonder why we are still sticking to failing policies. This also requires a statesman, someone who can stand against the mighty IMF/World Bank.

This is enough for now: an overhaul of the system and saying NO to the IMF/World Bank's economic policies. For more discussions, please open a new thread and tag me.

Queen Esther;14972846 said:
2. What is the contribution of the party to the eight mentioned issues.

By the party, you do mean CCM, don't you? For sake of saving my energy and time, I would say one thing: as long as Tanzania is ruled under the single-party or dominant-party system, CCM would never run away from the misery that most Tanzanians face on their everyday lives.

Queen Esther;14972846 said:
3. What is the culture of Tanzanians? Do you think with this culture of ours we can easily tackle the eight mentioned problems and have our breakthrough?

What do you mean by 'the culture of Tanzanians'? Anyway, whatever, your meaning would be, let me tell one thing: 'culture' can be nurtured. Societies can be cultured to: obey the laws; be disciplined; pay taxes etc. So, there isn't such an excuse as 'the culture of Tanzanians'. As, one may ask, why Tanzanians haven't been 'cultured' in the ways that you wish?

Queen Esther;14972846 said:
4. We are the least ranked in education and better in personal freedom, what are your views concerning that.

According to the report, Tanzania isn't ranked better in any subindex. I wonder, what is your criteria for Tanzania to be ranked better in personal freedom! So, I have no views, as Tanzania is nowhere better in the report.

Queen Esther;14972846 said:
5. Can you plz show the list of countries surveyed? What is the benchmarks for East African Countries??

Here is the link http://www.prosperity.com/#!/ranking where you can find the list of the 142 countries surveyed.

I don't know what you mean by the 'benchmarks for East African countries'!! The prosperity index is a global assessment. It shows prosperity based on income and well-being for the surveyed countries from different parts of the world. So, what would the benchmarks for East African countries help in discussing this? I guess, you want to compare Tanzania with Kenya, Uganda and Rwanda, which is absurd when talking about a global assessment. But, for the sake of making you happy, Rwanda (101th), Kenya (108th) and Uganda (115th) are all above Tanzania.
 
Last edited:
.
Pia tunaomba mtoa mada atuonyeshe serikali ya awamu ya nne "Prosperity Indices" zake zilikuwaje kutoka 2004/2005 hadi 2014/2015
Acha uvivu. Unaweza pia kuleta hizo indices. Siyo lazima nizilete mimi.
 
Haya sasa....hali halisi ndiyo hii...Songea vyoo vinafurika kwenye hospitali. Sasa sijui hilo 'jipu' nalo linahitaji mtumbuaji? Yaani tatizo lipo kwa muda wa siku 4!! Wagonjwa wanajisaidia kwenye ndoo na madishi!
 
Hizi habari huwa hawataki kabisa kuzisikia watu wa upande flani,lakini pamoja nakutozitaka hawana mikakati ya kuziboresha ili wasiziskie au kuziona..Ila wanaweza weza wakazuia vyombo vya habari kuonye matukio kama haya.
 
Nawakumbusha tu kwamba populism haitafanya huduma za afya na za kijamii kwa ujumla ziboreka. Hilo la kutumbua majipu, ndiyo Rais populist analifurahia kwa kuwa anafahamu watanzania wengi watashangilia kelele anazozipiga.

Kuna jamaa mmoja aliwahi kusema: "All new ideas go through a phase of hype and excitement, a phase of disillusionment, and then you start dealing with reality."

Sasa muda si mrefu wataanza kudili na reality pale watakapoona kelele hizo hazisaidii huduma za kijamii kuboreka n.k.
 
Sidhani kama uko realistic mkuu. Yaani survey ya mwaka mzima wa miezi 12 unaihusishaje na utawala uliokaa mwezi 1tu? JK kakaa miezi 10 na Magufuli miezi 2, ukitoa ripoti ya mwaka kwa serikali 1 hii ripoti itamhusu ile ya mwezi 1 ama ile ya miezi 10?

Mjinga kabisa na wewe tuseme hujaelewa somo au?unataka ahusishwe kikwete alieondoka?
 
Sidhani kama uko realistic mkuu. Yaani survey ya mwaka mzima wa miezi 12 unaihusishaje na utawala uliokaa mwezi 1tu? JK kakaa miezi 10 na Magufuli miezi 2, ukitoa ripoti ya mwaka kwa serikali 1 hii ripoti itamhusu ile ya mwezi 1 ama ile ya miezi 10?
Tatizo mmefungwa makufuli kawa Mungu mtu,amesema kuwa anatakiwa angalie hayo.....afanye mabadiliko hivyo ndo hali ilivyo
 
Ni sehemu muhimu hizo za kuangalia ....
 
Huyu jamaa anapenda kutukana wenzake hata pale ambapo hakuna sababu, mods muonyeni huyu jamaa
Mods wenyewe wanafurahia matusi...watu wengi humu lugha yao ni ya matusi tu lakini hawachukuliwi hatua
 
Haya sasa, magari zaidi ya 1,500 na abiria wasubiria masaa zaidi ya 7 maji kupungua katika mto ili wapite. Endeleeni kushangilia hapa kazi tu, huku mkikwama kutokana na maji kujaa barabarani

Sasa ulitaka wapite huku kuna mafuliko,hebu acha mambo ya ajabu we mtoa mada..hata marekani na nchi nyingne kibao huwa zanakumbwa na matatizo kama hayo,au ulitaka magufuli akazuie hayo maji kwa mikono?
 
Chifu, pale ni kuweka daraja tu...na hayo wala siyo mafuriko, ni mfano wa mafuriko...eneo lenyewe dogo na limekuwa sugu miaka nenda rudi mvua zinaponyesha...mwaka jana kama siyo hapo ni eneo jirani kuna polisi alikufa na familia yake...sasa kwa vile unafurahia siasa za kufuata upepo, endelea kufanya hivyo...ila uhalisia wa mambo unazidi kumwumbua mungu mtu wenu...

Ila kukwama kwa magari kwa zaidi ya masaa 7, kumeonyesha jinsi mfumo wetu wa response ni mbovu...yaani masaa 7 wasomi na wahindisi wote wa hapa kazi walikosa mbinu za kufanya safari ziendelee? Fungua macho yako chifu ili uone kwa upana zaidi...

BTW, weka video ya nchi hizo ambapo eneo na kiwango cha maji kama kwenye video niliyoweka, ilikwamisha magari zaidi ya 1500 kwa saa zaidi ya saba..
 
Back
Top Bottom