Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 61,211
- 99,963
Umejibu vyema sana sana tuna tatizo la kujibu bila kusoma na kuelewa, hata hivyo hongera kwa kuchukua muda kumueleza kwa upole. unarejesha heshima ya JF
Umesoma na kuelewa kweli? Ebu rudia tena kusoma.
Na kama unaelewa 'Magufulisation' ni nini, itakuwa rahisi kuelewa zaidi.
Lakini pia, kumbuka hii ni serikali ya chama kilekile cha utawala (napendelea zaidi uongozi badala ya utawala, lakini kwa kuwa kiuhalisia ni utawala, ngoja nitumie utawala) uliopita. Kilichofanyika ni mabadiliko ya mtu anayeongoza utawala. Ingawa ni kweli kabisa, mtawala huyu akiamua kuweka maslahi ya nchi mbele, anaweza kujitofautisha na utawala uliopita. Na hii naiona ni shida: kutaka kuitenga CCM na Magufuli. 'Zigo' la CCM Magufuli hawezi kuliepuka mpaka pale atakavyotenda kama statesman.
Hivyo basi, hata kama amekaa siku 52 madarakani, haimaanishi masuala ya prosperity hayamhusu. La hasha! Hizo poor rankings zimesababishwa na serikali za chama kilichopo madarakani. Kwa kuwa Magufuli naye anatokana na chama hicho hicho, hawezi kukwepa lawama na majukumu katika hili. Kwa hiyo, nilichofanya ni kumkumbusha uhalisia uliopo mtaani. Ingawa naamini anaweza kuwa anafahamu; siyo vibaya kumkumbusha. Aweke nguvu huko kunakohitajika zaidi. Na nimeweka hilo katika kuwakumbusha fanatics wa Magufulisation kuwa uhalisia mtaani haupo kama vile wanavyotaka kuuaminisha ulimwengu.
Sasa labda nikusaidie tu: hizo rankings zinaonyesha, in fact zinathibitisha tu hali halisi ilivyo on the ground. Hii 'Magufulisation' trend ya kucheza na mindsets za waTZ kupitia media haiendani na hali halisi ilivyo. Na nikasema, majawabu yote yapo mezani kwa Magufuli. Anachopaswa kufanya ni kufikiri na kufanya maamuzi kama kiongozi mwenye kuweka maslahi mapana ya nchi na siyo chama. Hii inamaanisha hata kama ni kwa kubadili status quo iliyotengenezwa na chama, na kumjengea maadui ndani ya chama.