Forex: Biashara Haramu kwa Muislamu

Hiz Dini africa zimetupoteza na zinatupoteza sana, unajua hawa jamaa wanajua kucheza vyema na akil zetu
Mtu alipotoka uko anakuambia heslb nayo n haramu, Daah na
Uislam ukikuingia inafika pahala unakua kama unaweweseka iv ata kama mama yako n mkrstu bas utamuona kafir,

Nilikutana na mtoto anakuambia napenda sana madrasa kuliko shule yan anataka kuacha shule na baaz ya waislam niliokua nao wakashadadia kabisa
Leo mwngn anakuja ooh forex haramu, stil salio likikata anachukua mkopo tigo 450/= anarudsha 500/=
Ukifikia stage hii huwa nakuona fal.a tu kwa dini tulizoletewa hakuna ata nabii mmoja mweus huu n ujinga daraja la kwanza....

Kulikua na mzozo ukristu sio dini kwa sababu haijawai kuandikwa kwenye kitabu kuwa ukristu n dini kama ilivyo uislam n dini ya kwel na ya haki
Aya mtuletee maandio FOREX NI HARAMU


na aliesema hatak dini zisizo na maendeleo tuko pamoja. 21century mpunguze upimbi ata kidogo
 
....Mtu alipotoka uko anakuambia heslb nayo n haramu...


Nani aliyesema heslb ni haramu kijana??

...Daah na
Uislam ukikuingia inafika pahala unakua kama unaweweseka iv ata kama mama yako n mkrstu bas utamuona kafir
...

...
Kulikua na mzozo ukristu sio dini kwa sababu haijawai kuandikwa kwenye kitabu kuwa ukristu n dini kama ilivyo uislam n dini ya kwel na ya haki...


Umeelewa hii mada lakini?? Hii mada haihusiani na Ukristo.. Tatizo la wabongo ni "taarifa vichwa vya magazeti", ni wavivu mno wa kusoma, kama huyu, kaona kichwa cha habari "fasta" kakurupuka kuingia na kucomment!!

....
Nilikutana na mtoto anakuambia napenda sana madrasa kuliko shule yan anataka kuacha shule na baaz ya waislam niliokua nao wakashadadia kabisa....


Wewe kama "umesoma", huna tofauti na huyo mtoto aliyeacha shule... Umeandika maelezo tele, pumba tupu.

..
Aya mtuletee maandio FOREX NI HARAMU
...


Tulia kijana, soma taratibu mada, maandiko yanayoharamisha biashara hii utayapata humo na kama muelewa bila shaka utaelewa. Pia, wewe unaonekana sio Muislamu, hivyo hii mada haikuhusu.. Umeelewa??

Uache "Kuwashwa washwa"
 
Halafu iyo tabia ya kulala na kuamkia kuvitia vitu uharam aisee mtafikia pabaya... Ulizuka mzozo kikombe cha babu loliondo n haram kuna waislam wengne walikataa kabisaa mbona imeswii
Leo hii fisi maji wawil watatu mnataka kulisha wenzenu ujinga, nakemea sana hii tabia, achen mara moja
Sijui akil zenu zpo wap, kuna mashek wanatia mikeka daily lakn apo apo kuna wengne wanakuambia haram
 
Halafu iyo tabia ya kulala na kuamkia kuvitia vitu uharam aisee mtafikia pabaya... Ulizuka mzozo kikombe cha babu loliondo n haram kuna waislam wengne walikataa kabisaa mbona imeswii
Leo hii fisi maji wawil watatu mnataka kulisha wenzenu ujinga, nakemea sana hii tabia, achen mara moja
Sijui akil zenu zpo wap, kuna mashek wanatia mikeka daily lakn apo apo kuna wengne wanakuambia haram


Sikia wewe "Kichwa Maji",

Ni Hiviiiiiii;

Forex Trading ni Biashara Haramu Kwa Muislamu,

Wacha iendelee kukuuma mpaka uvimbe "Makalio", There is nothing you can do about it.

PUMBAVU
 
Hawa waislamu wanaoishi dunia ya tatu ni wapuuzi sana(baadhi lakini akiwemo mleta mada) wana complications za ajabu kiasi kwamba hata ambao wamewaletea sheria za hiyo dini yao huwa wanawashangaa na kuwaona ni kama visiki tu wasivyojua dunia inaenda wapi. Kwa tasfiri fupi tu huyu jamaa ana twambia technology inapingana na dini yake!.

Anaongelea riba na speculation kama vitu haramu kwa muislamu yeyote kujihusisha navyo, anasahau kwamba hata serikali yake yenyewe tu inafanya speculation kwenye upangaji wa bajeti, anasahau kwamba hata wao wenyewe kuandama kwa mwezi huwa wana speculate.

Anatwambia forex ni haramu wakati cha kustahajabisha huko Dubai kwenye waislamu wenyewe ndio wamejaa ma forex traders kibao tu, yaani hawa waislamu wa bongo pasua kichwa wanasemaga eti hata mpira ni haramu wakati mataifa yaliyoshika dini ya kiislamu hapa afrika kama Egypt,Algeria,Tunisia ndio yanayofanya vizuri kimpira. Hawa macomplicator kama huyu mleta mada ni wakupuuza kabisa
Mkuu mbn jazba badala ya kuibua au kujibu hoja!
Habr ya ukristo c dini inakujaje hapa, lkn we unaonaje!? Ukristo Ina maana mpk Leo we hujui km no jina LA MTU na siyo dini! Nioneshe wapi kwenye biblia ukristo umeelezwa kama dini!?
Uislamu ni Dini sababu imeelezwa kwenye Qur an 3:19.
Argue don't shout!
 
Una shilingi ngapi kwenye account yako ya benki na mpesa na tigo pesa una shilingi ngapi huko pia?!

Maana sio unakuja kuanzisha uzi wa kubwabwaja hapa ili hali haupo vema kiuchumi. Maana kama story za pesa si chochote tutaziacha duniani na tutakwenda mbinguni, hizo porojo hazilipi bili ya maji na ada ya watoto. So wadau hawawezi kukuelewa chochote unless uwape plan B ya kutengeneza pesa.
 
Sawa ndugu zangu waislam... Vp mikopo ya vyuo vikuu maana wanadai usipoanza kulipa baada ya mwaka mmoja tuuu unavyo maliza chuo kuna kariba pale kanapenyezwa... Na ukichelewa zaidi wana double.. Je! Mikopo nayo ya vyuo vikuu ndugu zangu waislam tuiache?
Aisee bora muiache mtatupunguzia idadi ya wahitaji kwakweli. Na kitimoto pia ili kishuke bei
 
Una shilingi ngapi kwenye account yako ya benki na mpesa na tigo pesa una shilingi ngapi huko pia?!

Maana sio unakuja kuanzisha uzi wa kubwabwaja hapa ili hali haupo vema kiuchumi...

Huna akili...
 
Hapa utabaki wewe tu. Siwezi kuacha forex sababu ya upuuzi huu uliouleta hapa. Yaani dini yetu tunaroho mbaya sana, suala lolote lenye mafanikio ni haramu ndo tunaishia kwenye migogoro kama wenzetu Middle East
 
Assalam Alaykum,

Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyoeleza, uzi huu utajikita kujaribu kutoa mwanga kwa wasiofahamu juu ya uharamu wa biashara ya forex kwa mtazamo wa sheria ya kiislamu.

Kwa siku za hivi karibuni, kumekuwa na uhamasishaji mkubwa sana juu ya biashara hii ya forex kupitia mitandao ya kijamii hapa nchini Tanzania. Waislamu wengi wa Tanzania, kwa kutofahamu dini yao ama kwa kughafilika tu, wamejikuta wakiingia kichwa kichwa kwenye biashara hii pasipo kuelewa kama ni halali ama haramu kwa mtazamo wa sheria ya dini yao.

Binafsi niliifahamu biashara hii ya forex ( na nyinginezo kadhaa) na kufungua Forex Trading Demo Account kati ya mwaka 2010 na 2011 wakati nipo chuo kikuu nje ya nchi (sitoitaja nchi), kipindi nasoma undergraduate. Kiukweli ni biashara inayolipa sana japo ni wachache sana wanaofikia daraja (level) ya kuwa washindi (in a long-term basis), wengi hupoteza pesa kwa sababu ni biashara inayohitaji elimu na uzoefu wa muda mrefu na uvumilivu wa hali ya juu na bahati pia.

Namshukuru Mwenyezi Mungu aliniongoza na nikafahamu kuwa biashara hii hainifai mimi kama muislamu na nikaweza kuachana nayo (japo iliniuma kimtindo, maana ni biashara inayolipa). Mimi nilichoangalia ni radhi za Mwenyezi Mungu kwangu hivyo nikaacha kujishughulisha na kuingiza kipato cha haramu kupitia hii biashara. Binafsi, Akhera kwangu ni muhimu kuliko Dunia.

Niliipoona biashara hii ya Forex imepamba moto nchini, nilijisikia vibaya kuona vijana wenzangu wa kiislamu wakiingia kichwa kichwa. Najua wengi ni kutojua dini tu, maana hata mimi nilikuwa vivyo hivyo mwanzoni. Hivyo niliona dhima kubwa ya kuwafikishia onyo juu ya kujihusisha na biashara hii. Nimeutua mzigo na mbele ya haki kwa Mwenyezi Mungu nitakapoulizwa nitajibu kwamba nilijitahidi kuwaeleza waislamu juu ya uharamu wa hii biashara.

Muhimu
Kuuza na kununua currencies tofauti (kama tanavyofanya kupitia Bureau de Change) si haramu kwa sheria ya kiislamu, kinacholeta uharamu kwenye biashara ya Forex ni System inayoendesha biashara yenyewe (yaani STP na ECN brokerage Systems).

Masheikh wengi wa Tanzania bahati mbaya hawana elimu ya Dunia, na hata hiyo elimu ya dini wengi wapo juu juu tu. Hivyo kamwe usijisumbue kwenda kuwauliza kuhusu Forex. Wengi hata hawajui Forex ni kitu gani kama ambavyo watanzania wengi walikuwa hawajui forex ni kitu gani.

Nakuletea Sheikh Hacene Chebbani kutoka Algeria ambaye anaishi Canada tokea mwaka 1997. Sheikh Hacene ana Masters in Islamic finance (UK, 2012) pia ana BA in Islamic Sharia kutoka Islamic University of Madinah (1993).

Nakuomba fuatilia lecture aliyoitoa Sheikh Hacene kwa wanafunzi kupitia Youtube kuhusu uharamu wa biashara ya Forex kwa mtazamo wa sheria ya kiislamu.




Sheikh anazungumzia masuala mbalimbali ya hii biashara, tafadhali ewe muislamu usiache kuitazama lecture hiyo ili upate elimu juu ya masuala hayo.

Kwa wale watakaoshindwa kuitazama, angalau ondoka na Summary ifuatayo ambayo nimeiwasilisha kwa mtindo wa maswali na majibu (Q&A) kama ifuatavyo:

Swali: Je biashara hii ina Riba??
Jawabu: Ndiyo, Kuna riba kwenye biashara ya Forex

Swali: Je, Islamic forex Trading Accounts (Swap Free Accounts) zipo na brokers wanatoa hii huduma??
Jawabu: Ndiyo zipo. Forex brokers karibia wote duniani wanatoa huduma ya account maalum kwa ajili ya waislamu tu (Islamic Forex Trading Accounts).

Swali: Je, Islamic Trading Accounts zinahalalisha biashara ya forex kwa mtazamo wa Sheria ya kiislamu?
Jawabu: Hapana, Islamic Trading Accounts bado hazihalalishi biashara hii ya Forex kwa waislamu.

Pia Sheikh Hacene amezungumzia masuala mengine kama Margin, Leverage na nidhamu ya ukopeshaji/ukopeshwaji wa mtaji.

Nimetua dhima hii na kilichobaki ni juu yako wewe muislamu, chagua kutii ama kukaidi, Dunia ama Akhera. Hilo ni juu yako.

Namshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu

Ahsante.


Pia soma fatwa hii hapa chini kutoka jopo la wanazuoni wa kiislamu:


Jazzakallahu khayr mleta mada
 
Hapa utabaki wewe tu. Siwezi kuacha forex sababu ya upuuzi huu uliouleta hapa. Yaani dini yetu tunaroho mbaya sana, suala lolote lenye mafanikio ni haramu ndo tunaishia kwenye migogoro kama wenzetu Middle East

Mwenyewe nilifatilia hilo swala kwa kadri ya uwezo wangu. Ukweli ni kwamba inabidi ukubali fact za dini bila kuingiza hisia zako. Mimi huwa nasoma sana hadith (Sahih Bukhari) na jambo la kwanza kabisa mwanzoni wakati najua kuhusu forex, nilisema niende kuangalia nini hadith za Mtume zinasema kuhusu hilo swala. Ukisoma Book of Sales and Trade kwenye Bukhari Vol. 3: 9, 81-83, swala la foreign currency exchange limeongelewa vizur sana:

"Narrated Abu Al-Minhal:

I used to practice money exchange, and I asked Zaid bin 'Arqam about it, and he narrated what

the Prophet said in the following: Abu Al-Minhal said, "I asked Al-Bara' bin 'Azib and Zaid bin Ar-qam about practicing money exchange. They replied, 'We were traders in the time of Allah's Apostle and I asked Allah's Apostle about money exchange. He replied, 'If it is from hand to hand, there is no harm in it; otherwise it is not permissible."

"Narrated Abu Salih Az-Zaiyat:

I heard Abu Said Al-Khudri saying, "The selling of a Dinar for a Dinar, and a Dirham for a Dirham (is permissible)." I said to him, "Ibn 'Abbas does not say the same." Abu Said replied, "I asked Ibn 'Ab-bas whether he had heard it from the Prophet s or seen it in the Holy Book. Ibn 'Abbas replied, "I do not claim that, and you know Allah's Apostle better than I, but Usama informed me that the Prophet had said, 'There is no Riba (in money exchange) except when it is not done from hand to hand (i.e. when there is delay in payment).' "
"

Kama utaweza, you can trade forex kupitia physical cash. Sikumbuki vizuri ni uzi gani lakini nakumbuka vizuri sana kuna mtu aliongelea kupata faida kwenye kuchange Rand ya SA kupitia hizi bureau de change. Forex trading tunayofanya sisi sio mkono kwa mkono kama wale wanaochange hela mipakani au kwenye bureau de change. Hivyo ni haram.

Tatizo letu hatusomi na hatufatilii mambo kiundani, na tukija kuambiwa ukwel mnaleta hisia zenu. Anyways, now you know.

Note:
"Bukhari Vol. 3: 9, 81-83" - Hii ilikua kwenye physical copy, vile vitabu saba vya Sahih Al-Bukhar.
Unaweza soma hadith zifuatazo:
Volume 3, Book 34, Number 276 : Hapa
Volume 3, Book 34, Number 386: Hapa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom