Mheshimiwa, mbona solution zipo wazi ila wote tumevaa miwani ya mbao (japo spika wako hapendi hii kauli, au sijui alisahau kama ni nahau!)kuziona hizo solutions? Kuna vitu ambavyo hata nyie wenyewe bungeni mnaviona havifai lakini kwa kauli nzito mnapitisha bajeti zake. Mkulima anashindwa kufikisha mazao yake sokoni kwa ubovu wa barabara, lakini nyie mmeelekeza nguvu kwenye barabara za miji mikuu. Mnaongeza nguvu kwenye maendeleo ya miji mikuu, ili hali ile ya pembezoni mkiiacha yatima. Fedha nyingi sana zinatumika isivyo na watendaji tuliowaweka madarakani, bila kusahau mafungu yanayojitengea kuja kuwasilisha bajeti zao! Hii yote ni diversion ya funds ambazo zingetumika kwa maendeleo yetu wenyewe! Ndani ya yote haya utawala wa sheria ndio umefeli kabisa, wamebaki wanahamishiwa sehemu nyingine ili wakaharibu zaidi. Tunapiga kelele na kilimo kwanza, do we really mean it? Sekta ya kilimo ingepewa kipaumbele kama mnavyopiga makelele majukwaani mbona tungekuwa mbali? Asilimia kubwa ya waTZ siyo wafanyakazi, tena nafikiri tungeanza kusema kuwa nchi yetu inaundwa na wakulima, wafanyakazi na wasio na kazi. Asilimia kubwa ya wasio na kazi ingeweza kutupwa kwenye sekta ya kilimo, kama tungeamua kwa nia ya dhati kukipa kipaumbele, kilimo siyo lazima mahindi tu, na mboga mboga nacho ni kilimo ambacho soko lake ni zuri tu. Lakini je, yule kijana aliyeko barabarani kama mmachinga, anaweza kuwa transformed kuingia huku? Lile dirisha lenu la TIB linaweza kum-support? Thubutu! Anayekuwa supported huku tayari ana range rover!
Mkuu, kwa ufupi ungemwambia tu kwamba tunashindwa katika hayo yote kwa sababu hatuna vipaumbele. Kama unaweza kwa mfano kukomaa na kujenga daraja la kigamboni kwa mabilioni ya shilingi wakati reli zetu (hasa hii ya kati) ziko taabani basi tuna tatizo kubwa sana ambalo hasa hasa liko kwenye uongozi ambao yeye mleta mada hataki tuubadilishe kama sehemu ya ufumbuzi wa matatizo.