nafikiri ni jambo zuri kufikiria namna ya kutatua matatizo tuliyonayo; muhimu zaidi ni kuzuia matatizo ambayo bado hayajatupata yasitupate.
mimi ningezungumzia kwanza kwenye nishati; tuwekeze kwenye hydroelectric power kwasababu research inaonyesha Tanzania inapata ukame kila baada ya miaka 13 kwahiyo swala kubwa sio ukame; na hydroelectric ni "expensive to install cheaper to run" tofauti na sasa nchi inaendeshwa kwa majenerator ambapo pesa nyingi sana zinatumika kununua mafuta na kulipa wenye jenereta capacity charge. huwa najiuliza nakosa jibu inawezekanaje kuendesha nchi kwa jenereta wakati mtu mwenye kipato cha wastani hawezi kumudu gharama za kuwasha jenereta masaa 12 kila siku
Lapili nadhani ni sahihi kuzalisha umeme wa gesi "plant" ikakaa chanzo kilipo, faida ya hii ni urahisi wa kuongeza"plant" kama matumizi yakiongezeka na kutumia nyaya zilezile; tofauti na bomba ambalo lina kiwango "maximum throughput" kwahiyo matumizi yakiongezeka inabidi tujenge bomba lingine.
Pili nizungumzie kuhusu madini; kwanza yauziwe hapa nchini, yakiuziwa hapa nchini fedha za kigeni zitakuja hapa nchini, pili kodi stahiki italipwa kwa mauzo (labda niulize kwa sasa hivi kodi ya mauzo yanayofanyika afrika kusini mnapataje?)
Pia kwenye madini ni wakati muafaka sasa wa kuchimba wenyewe, kwasababu watu wengi wenye ujuzi tayari wapo na mashine zinazohitajika sio ghali sana
Tatu zungumzeni na wenye fedha nje ya nchi waziwekeze hapa (inabidi hapa tukae kama taifa tusahau yaliyopita maana hata wakifungwa pesa itapotelea huko nche bora irudi nyumbani), wakifungua viwanda vitasaidia kupunguza tatizo la ajira, na kuongeza thamani ya bidhaa tunazozalisha
Nne boresheni reli nchi nzima, sasa mnakopa kujenga bandari nyingine wakati zipo tayari bandari zenye reli zinazohitaji tu kuendelezwa na mfumo wa reli kuboreshwa, kukiwa na reli nchi nzima mazao mengi ya wakulima hayataaribikia shambani.
Kikubwa zaidi ya yote ni kubadilisha mfumo wa uongozi ili watu wachache wasiwe na uwezo wa kufanya maamuzi hatarishi kwa nchi bila kuwepo kwa chombo chochote cha kuwadhibiti, mfano sidhani kama wewe mwenyewe umeshawahi kuuona mkataba wa uchimbaji jimboni kwako, mfumo uliopo wa uongozi ni hatari sana kwa mstakabali wa Taifa, Katiba mpya ikiweza kudhibiti hili basi tunaweza kusonga mbele
Mawazo ni mengi nadhani hata nyie mnayo ila shida mfumo wa maamuzi, watu wanakopa wanakopa wanakopa sisi na vizazi vyetu tunalipa bila hata kujua umekopa nini kwa faida gani, mimi naiona hii "initiative" yako nzuri lakini kwa nchi yetu ilivyosasa ni "mission impossible"