Fomu za wagombea urais zaanza kutolewa Congo DRC .

Fomu za wagombea urais zaanza kutolewa Congo DRC .

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,810
Reaction score
7,696
Habari kwenu wadau.

Nchini Congo DRC Fomu za wagombea urais zaanza kutolewa. Fomu hizi zinatolewa kuanzia tarehe 25/07/2018 hadi 08/08/2018.

Hata hivyo siku ya kuanza na ya pili zimepita bila kutokea mgombea hata moja aliyechukua fomu . Hayo yanajiri huku tetesi zikivuma kuwa Kabila atagombea awamu ya tatu licha ya katiba kutomruhusu.


Vyama vingine vimeshatangaza wagombea wao rasmi lakini kuna usiri ktk chama cha Kabila cha PPRD.

Ktk hali ya kushangaza idara ya uhamiaji nchini humo imetoa taarifa kuwa RAIA mwenye uraia pacha au nchi mbili asithubutu kuchukua Fomu ya urais. Hapa analengwa Moses Katumbi, baadhi ya mawaziri serikalini na wabunge machachari wenye uraia wa aina hii.

Hata hivyo mawakili wa Mosee Katumbi wamesema mteja wao hana uraia wa nchi mbili na Italy inayohusishwa na uraia huo imemkana Katumbi. Moses Katumbi anahofiwa mno na Rais Kabila.

Nitzidi kuja na updates kila siku hadi tarehe 08/08/2018 na hata hadi uchaguzi mkuu nchini humo 23/12/2018.
MREJESHO: Marekani yamuonya Kabila asidhubutu kugombea Urais na aheshimu katiba. Hayo yamesemwa Leo kt baraza la umoja wa mataifa n naibu Balozi wa Marekani ktk umoja huo Jonathan Cohen

Updates: Kiongozi wa waasi wa zamani aliyewahi kuwa makamu wa Rais, John Pierre Bemba arejea Congo akitokea Belgium. Kabla ya hapo alikuwa akikakibiliana na mashtaka huko Hague Uholanzi ambapo hakukutwa na hatia. Hali ya taharuki yaibuka na serikali yamkataza kufika nyumbani kwake akidaiwa makazi yake yapo karibu na makazi ya Rais Kabila.


Bemba aapa ni lazima achukue fomu agombee urais ila chama PPRD cha Kabila kimeapa kumwekea pingamizi kikidai aliwahi kukutwa na hatia huko The Hague ya kuwahonga mashahidi. Huku pia ikidaiwa kesi moja haijatolewa hukumu.

Hatimaye Bemba awasilisha nyaraka zake za kugombea urais ktk ofisi za tume ya uchaguzi CENI bila kizuizi chochote.

UPDATES: Moise Katumbi adai atarejea leo nchini Congo DRC ili naye awasilishe nyaraka za kuwania urais. Serikali ya Congo yapiga maruku ujio wake na polisi wa kuzuia ghasia wamepelekwa Lubumbashi kuizuia ndege yake isitue.

Pia mahakama nchini humo imesema ikiwa Katumbi atatua, atakamatwa papo hapo kuendelea na kesi yake ya kuajiri Mamluki kumlinda na kupora nyumba za watu kinyume na sheria. Kesi hizi mbili zilikuwa zikimkabili kabla ya kukimbilia uhamishoni mwaka 2016 ambapo alikimbilia Belgium. Saivi anatokea Africa kusini ambapo alihamia huko kwa muda baada ya kuondoka Ubelgiji.

UPDATES: Ndege iliyombeba Katumbi yazuia kutua aridhi ya Congo. Ndege yatua Ndola Zambia huku Katumbi akipanga kuingia Congo kwa gari. Serikali imefunga mipaka yake na Zambia huku vikosi vya jeshi vikipelekwa mipakani kumzuia asiingie nchini humo kuchukua Fomu ya urais.

Hatimaye Katumbi arudi Zambia na amekwama nchini humo baada kuzuiwa na vikosi vya usalama vya Congo DRC kuingia humo nchini.

UPDATES: Katumbi ameruhusiwa tena kuvuka mpaka na kuingia Congo DRC huku majeshi ya UN yakiwa yamefika hapo mpakani bila kijulikana sababu zao za kuwasili eneo hilo.

UPDATES: Umoja wa vyama vinavyomuunga mkono Kabila, Common Front for Congo (CFC) vinafanya mkutano mkuu nje kidogo ya jiji la Kinshasa ili kumtaja mgombea atakayewakilisha muungano wao ktk mbio za urais. Itajulikana rasmi muda sio mrefu ikiwa Kabila atagombea au laa.

Hayo yanajiri huku waziri wa zamani nchini Congo bwana Ken Kien Mulumba naye akichukua fomu ya kuwania urais. Nitawajulisha chama chake hivi punde.

UPDATES: Emanuel Ramadhani Shadari apitishwa na muungano wa vyama vinavyomuunga Rais Kabila kugombea urais kupitia muungano huo. Shadari aliwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani. Sasa uvumi wa Kabila kugombea kwa nguvu kama Nkuruzinza wa Burundi umekwisha. Emmanuel Shadari kwa sasa ni katibu mkuu wa chama cha Rais Kabila cha PPRD.

Shadari atakiwakilisha chama chake kilichoungana na vyama vingine vingi maarufu kama Common Front for Congo ( CFC) ktk uchaguzi mkuu wa tarehe 23/12/2018.
 
Last edited:
Vital kamerrhe au moise katumbi wanafaa urais sema kagame hatoruhusu hilo lazima kabila ashinde urais otherwise itaanzishwa M23 nyingine ili nchi ivurugike hadi kagame aweke pandikizi.
Wapinzani wakiungana watatoa upinzani mkubwa na wanaweza leta matokeo chanya,ttz hawana umoja, Moise,Felix, Vital na Bemba kila mmoja anataka ,tusubiri tuone

Nilikua Kinshasa siku JK Jr anahutubia, nimerudi Lubumbashi ,kifupi JK Jr anawajuilia wa Congo man ,mpk sasa kawatega

Congo itaamuliwa na wa Congo wenyewe
 
Twende kazi
IMG_20180728_204436.jpg
IMG_20180728_204454.jpg
IMG_20180728_204500.jpg
 
Huyu naye ni walewale tu maana ni mtu wa system kwa miaka mingi hivyo sioni kama ataleta mabadiliko mara kumi wampe katumbi sema muhimu waungane maana bila hivyo kabila atawashinda asubuhi kweupe bila hata ya kuiba kura
Umeongea point nimesema huko juu wapinzani Congo hkn kitu,hata huyo Moise hkn kitu ,na Bemba kmunavyosema ni system /,project ya JK Jr

Bemba hawezi kuungana na wapinzani, Moise ana kesi ya kujibu nje ya siasa

Mbaya zaidi wa Congo man nao wanaukabila
 
Back
Top Bottom