Mawazo yako naona bado hatasaidia tatizo la foleni Kwa jiji la DSM, swali ni mjia gani walitumia mfumo huo na kufanikiwa? Bado kila siku majengo makubwa yana jengwa city center na miundombinu ni ileile. Solution kwa wazuiwe ujenzi waa majengo makubwa city center, wizara na ofisi za serikali zihamie Dodoma, yatengenezwe masoko manne pembeni mwa mjia kama mbadala wa Kariakoo, miundombinu ipanuliwe na kuboreshwa, zijengwa fly high wayUkitazama kwa makini foleni za magari jijini kati Dar utagundua kuwa almost 60-70% ya magari ni ya watu binafsi. Utakuta foleni kwa mf inatoka manzese hadi magomeni ina magari 40 binafsi na mtu mmoja au wawili kila gari, jumla 40-70 na utakuta costa 5 tu zenye watu jumla zaidi ya 100.
Ningekuwa mimi ni Raisi au Waziri mwenye dhamana ningefanya yafuatayo kupunguza foleni.
1. Ningenunua mabasi ya serikari, 5 kila route then ningepiga marufuku gari binafsi kuingia jijini kati. Magari hayo yangeendeshwa na kusimamiwa na SUMATRA
2.Ningeanzisha congestion fee ambayo ni pesa taslim mtu atakayolipa kama anataka kuingia na gali lake mjini kati.
3.Wenye magari binafsi ningewashauri waache magari yao nje ya mji mfano, mbezi ya kimara, tegeta, buguruni, tabata, n.k. then wapande costa au magari ya serikali ambayo nauli yake ingekuwa reasonable.
Kwa kufanya hivyo;
1. Nina uhakika kama kuna foleni ya magari kutoka jangwani hadi magomeni itakuwa ina magari 20- 30 yenye watu kati ya 500- 1000, je hapo si nitakuwa nimebakiza safari kaTI YA 5-10 na kuwamaliza watu walio kariakoo wanaongoja kwenda mbezi? nina uhakika foleni haitakuwa ndefu na safari ya kufika kimara au mbezi kutoka kariakoo itachukua muda usiozidi dk90 badala ya masaa 3 ya sasa.
2. Nitawapunguzia kazi traffic kwani hawatakuwa na ulazima wa kuongoza magari kwenye mataa labda umeme ukatike.
3. Nitapunguza gharama ya maisha kwa wenye magari ya kununua mafuta ya 20,000 kila siku.
4. Nitakuwa nimeleta usawa barabarani kati ya tajiri na maskini.
5.Nitakuwa nimewapa nafasi vijana wanaokopa pesa benki na kununua magari(starlet n.k.) kuitumia pesa hiyo kwa mambo ya maendeleo kama kununua viwanja, kujenga nyumba, kununua furniture n.k.
6. Nitakuwa nimetoa nafasi za kazi kwa madereva na wafanyakazi wa magari hayo ya serikali.
7.Nitakuwa nimeondoa adha ya watu kuamka saa 10 alfajiri kutoka mbezi ili wawahi foleni.
8.Nitawapa wanandoa muda wa kuwahi kutoka kazini kwenda nyumbani kuonana na familia na kutoa malezi kwa watoto badala ya sasa ambapo wafanyakazi wanangojea foleni iishe posta saa3 usiku ndo wawashe magari yao kwenda mbezi wanakofika saa 4.30 usiku na kukuta watoto wamelala na wapenzi wao wamechoka hata hawawezi kufurahia ushirika wa familia.
9. Kwa kufanya hivyo hata barabara zangu za mabasi yaendayo kwa kasi zitakuwa na maana na maisha ndani ya bongo yatakuwa super.
Hayo ni mawazo yangu, I stand to be corrected.